TAMU YA LEO
Member
- Mar 26, 2020
- 8
- 3
Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro limetajwa kushindwa kupiga hatua za kimaendeleo kwa miaka kumi kwa kukosa mwakilishi sahihi wakutatua changamoto zilizopo.
Kutokana na hali hiyo mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia chama cha mapinduzi(CCM)Dkt Charles Kimei amesema sasa ni muda muafaka wakuleta maendeleo ambayo kwa muda ni kama yamedumaa.
Dkt Kimei alisema changamoto ni nyingi ila kwa utashi alio nao ataweza kuzitatua na kupunguza makali ya maisha kwa wanavunjo kama ilivyo dira ya serikali ya awamu ya tano.
''Changamoto zilizopo zinaenda kupata ufumbuzi ninazijua na ndio maana naomba mnitume nikawe mwakilishi wenu haya si maisha ya wana Vunjo ni kuwa hatuna mtu sahihi''alisema
Dkt Kimei alisema miongoni mwa mambo yanayowakwamisha wanavunjo ni pamoja na miundombinu duni katika masoko,sanjari na uelewa duni wa fursa za mikopo yenye riba nafuu.
Alisema endapo atachaguliwa ni lazima ahakikishe kuweka nguvu katil kuboresha mambo hayo ili kuweza kuwavusha wananchi kutoka sehemu moja hadi nyingine kiuchumi na kimaendeleo.
Mgombea udiwani kata ya Mwika Kusini(CCM)Dan Pius alisema muda umefika sasa kwa wananchi kufanya maamuzi sahihi ambayo yana tija kwa siku zijazo.
Alisema serikali haijashindwa kuleta maendeleo ila tatizo lililokuwepo ni kukosa watu sahihi na makini wenye uchungu wa kimaendeleo ambapo wengi hawayafikirii hayo hutafuta maslahi binafsi.
Mwisho.