Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufikiri kila itakayoweza kutatua tatizo la upungufu wa Umeme Nchini na kama wasipofanya hivyo atahakikisha hawalali usingizi
Pia, Dkt. Biteko amekiri kuwa TANESCO inakabiliwa na matatizo ambayo yako nje ya uwezo wao lakini anashangazwa na kitendo cha kukuta Mashine ya kuzalisha Umeme katika Kituo cha Gesi Asilia ikwia imeharibika kwa miaka miwili huku chanzo cha Umeme kwasasa kikiwa ni 65%
Ameongeza kuwa TANESCO imejilimbikizia Mamlaka yote kutoka Mikoani na hakuna wanachokifanya huku akitoa onyo kwa kitengo cha Manunuzi cha Shirika hilo kuwa kijitafakari kabla hajaenda kukitembelea