Dkt. Biteko: Kule Bukombe tuliwahi kuchagua Wapinzani tunaelewa madhara yake, nawasihi wananchi wote chagueni CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,107
Naibu Waziri mkuu Dr Biteko amesema uchaguzi wa serikali za mitaa uko Karibu hivyo Wananchi wajipange kufanya uamuzi wa busara wa kuichagua CCM

Dr Biteko amewashukuru Wananchi wa Mbogwe kwa kuichagua CCM miaka yote, "Kule Bukombe tuliwahi kuchagua Wapinzani tunaelewa madhara yake" amesisitiza Naibu Waziri mkuu

Chanzo: Upendo TV
 
Yuko sahihi kwa kiasi fulani. Tulikuwa na wabunge wa upinzani, ukafika wakati wakawa wanapinga kila kitu, mpaka miradi ya maendeleo kwenye majimbo yao wenyewe; eti kazi ya upinzani ni kupinga! Upuuzi mtu
Unapo- comment hapa ujue hadhira ya jf imeelimika, sio kwamba unawasiliana na wajinga kama wale wanaogawiwa kofia na kanga za kijani wakati wa uchafuzi. Sema kabisa mbunge gani wa upinzani alipinga kila kitu.

Tunajua wabunge wa upinzani wamekuwa wakiikosoa/ kuipinga serikali ktk yale mambo ambayo mtu yeyote mwenye akili, anayependa kuona ustawi wa taifa letu anaona wazi wanasiasa wa ccm wamekosea, tena mara nyingi kwa makusudi.

Mfano, nani asiyejua wabunge wa upinzani walivyolalamikia mikataba ya madini na gesi, wakafukuzwa bungeni, ikapitishwa na wabunge wa ccm, baadae ccm haohao wanakuja kuvunja mikataba hiyo bila kufuata taratibu na kulitia taifa katika hasara kubwa?

Tuambie huyo mbunge wa uipinzani aliyepinga mradi wa maji, afya, elimu etc ni yupi?

Kauli ya biteko inadhihirisha jinsi ccm wasivyo tayari kwa demokkrasia. Haina tofauti na kauli ya magufuli kwamba ukichagua upinzani hutapata maendeleo - magufuli alimaanisha yeye na serikali yake walikuwa wanatumia madaraka yao vibaya kubagua wananchi waliotumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wawakilishi wanaowataka, ambao sio ccm.

Ni sawa na kauli ya saa mia moja kwamba hata ukichagua upinzani, ccm ndiyo itakutawala.
 
Watatengwa kama Mbeya.Toka tumewaweka pembeni Wapinzani maendelea ya Mkoa Sasa ni kemkem.

Ni ujinga kuchagua Wapinzani ambao hawawezi kushika Dola then sijui watakuwa wanatekelezaje Ilani.
 
Back
Top Bottom