Dkt. Bashiru atoa maagizo kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DKT. BASHIRU ATOA MAAGIZO KWA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA WILAYA

Leo tarehe 23 Novemba, 2019 Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiwa njiani akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar Es Salaam amepita na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa CCM Kibaha Mkoani Pwani.

Akikagua ukumbi huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Makatibu wa CCM wa Mikoa Wilaya nchini kuhakikisha viwanja vyote vya CCM vilivyopo katika maeneo yao kuhakikisha vinapata hati halali ya umiliki.

"Napenda kutumia wanachama na viongozi mliopo hapa kutoa maelekezo, viwanja vyetu vyoote nchi nzima ambavyo tumevitambua na tutakavyovinunua lazima vipate hati, na ninawaagiza Makatibu wa mikoa na wilaya nchi nzima wawasiliane na ofisi yangu, tumeshaweka utaratibu mzuri wa namna ya kumudu gharama kila kiwanja kiwe cha Chama au Jumuiya zake kipimwe na kipate hati kutegemea na maeneo kilipo, ardhi zote yawe mashamba, viwanja ni lazima tupate hati za kudumu za mila na za makazi" Dkt. Bashiru ameeleza

Aidha, Katibu Mkuu akizungumza na baadhi wanachama hao na viongozi waliojitikeza kumpokea, ameeleza kuwa,

"Haya mafanikio makubwa yanayopatikana hata kabla ya kufika mwisho wa utekelezaji wa Ilani yetu ni kutokana na matokeo ya Serikali za CCM kutimiza ahadi zake na pia kuwa na viongozi shupavu na jasiri wanaofanya maamuzi sio maneno matupu".

Hivyo kuwataka wananchi wote kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika kipindi hiki ambapo nchi inaendelea kujengwa kwa kasi kubwa kama ambavyo wanashuhudia ukamilishaji wa miradi mbalimbali yenye tija na manufaa makubwa.

Mapokezi hayo yamehudhuriwa na Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Ndg. Ally Makao na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mama Assumpter Mshana.

Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Bashiru kaishiwa sijui mtu ukiingia huko ccm wanakupa kinywaji gani
 
Huyu Bashiru anapwaya ameajiki makatibu wa ccm wilaya ni majizi matupu hata hakuyachunguza kabsa
 
Back
Top Bottom