Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,221
- Thread starter
- #41
Kweli kabisa mkuu.Umemaliza kila kitu Mkuu Jidu La Mabambasi 👏👏👏
Tutaongea vyote lakini tatizo liko pale pale, Ucheleweshaji wa malipo.
Tatizo la Wizara ya Maji inaidhinishiwa Bajeti na Bunge labda 820B lakini zinazotolewa hazizidi 300B, mwisho wa siku lawama zinakwenda kwa Watendaji eti Vilaza.
Wanadhani utatumika muujiza gani kutekeleza miradi pasipo na fedha kutolewa kwa wakati?
Zamani wasimamizi wa miradi walikuwa wanapewa hela ya kusimamia ~Supervision siku hizi unakuta hakuna hela za Supervision wanapata, inafikia muda Project Manager hawezi kwenda site kwa kukosa Dizeli au hata Usafiri. Kwa muktadha huu ni ngumu kupata matokeo Chanya kwenye Sekta.
Ukitaka kuona hili angalia miradi ya Tanroads, unakuta jamaa wana magali hata 3 kwenye mradi mmoja then angalia ya Maji uone kichekesho.
Me nadhani matatizo ya Sekta ya Maji yanatengenezwa kutoisha ili kuwafanya Watawala waendelee kupata Kura za kwenye Chaguzi zao.
Halafu utafikiri haya matatizo wanasiasa hawayaoni.
Ndiyo maana tunaisfia Wizara ya Ujenzi na kuiponda hii ya Maji katika kutekeleza miradi kwa weledi.