Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,878
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi ametembelea Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) na kuagiza menejimenti ya taasisi hiyo kuongeza ufanisi kwani kuna watumishi wameanza kuonesha uzembe katika taasisi hiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Abbasi, ameagiza kusimamishwa kazi mameneja wawili wa idara za matangazo na usambazaji na eneo la uchapishaji ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi ya idara wanazoziongoza.
"Kila mtumishi wa umma kwa sasa na natoa wito kwa taasisi za Wizara ya Habari ambao najua wengine mlikuwa hamjazoea kuchukuliwa hatua mjue sasa ni saa za kazi; ukileta uzembe kazini utachukuliwa hatua bila kusita," alisema Dkt. Abbasi.