Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Nadhani hizi ni fikra ambazo watanzania wengi zinatawala vichwa vyetu and I think it is because our judgement is somewhat clouded by fear rather than wisdom. I do think like you kua ni vema kukaa kimya yaishe lakini pia najiuliza kama kila likitokea la kutokea option ni kukaa kimya yaishe je Tanzania, samahani, Tanganyika, ingalikua huru leo??? Nadhani jibu ni hapana kwani kama mzee Nyerere angekaa kimya na kuacha wakoloni waendelee kutesa na kuadhibu na kufanya yale waliyofanya kama ambavyo vitabu vya historia vinatuambia walifanya, basi waingereza wangeendelea kutawala na labda kungetokea mgawanyiko mwingine ambao labda ungeitwa "(name of the city)" conference, na yangeendelea mengine tusioweza kuyadhania sasa. Nikijaribu kufananisha scenario hii ya dokta na enzi ile ya ukoloni namwona dokta ni mtanzania anaelazimishwa kulima shamba la bepari na bepari mwenyewe ndio huyoo mtesi wake (kwa fununu za kitaa ni .........). So.,,, let him speak If he wishes to, he might be the nowdays Nyerere coz we already have the nowdays "Mangungo Msovero"z. Everything falls in place kama ambavyo ilitokea kwenye historia.
 
Ukweli haufichiki Ulimboka mwenyewe ndiye atakayetufungua macho, juu ya matukio kama alilofanyiwa yeye ili kuzima haki za walio wengi. Keep it up Dr. freedom is coming today and not tomorrow!
 
tushapigwa changa la macho hapa! hamna cha kufungulka wala cha kuji open hapa!
 
ukweli haujifichi hata huyo ulimboka mwenyewe akija na habari za kutengeneza itajulikana tu, kwasababu ukweli hautengenezwi kwenye kinywa cha mtu wenyewe unajitagemea, kwa hiyo kama serikali itajidangaya kumsomesha ulimbok ili atudanganye kana mwakyembe auibu itabaki juu yake
 
Sikubaliani na wewe, ni lazima aseme ukweli ili isije ikatokea tukasikia tena kirahisirahisi kwamba Radhia Sweety ameuawa msitu wa pande na watu wa Ikulu, kwasababu tu huwa anachangia kwenye mijadala ya JF against Serikali


watu kama nyie ndo inabidi mteketekee kwa moto.. Kumbuka kwamba hakuna watu,mtu au kundi lolote..imewah shndana na dola. Mnamjaza ulimboka kiburi!akifa mtaipa familia yake ugali.
Ulimboka kwa mema yako na familia yako nakushauri tulia tulii.
 

Wewe Great thinker, Mwanahalisi aliandika habari za uchunguzi wake binafsi kama gazeti,na mpaka sasa
zaidi ya kulifungia gazeti hakuna aliyekanusha habari hizi watanzania tukamwelewa,na kama hazikuwa na
ukweli wafanyakzi wa tigo kwa nini walifukuzwa kazi?Think Twice"
 
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.
Kwa nini tigo imefukuza wafanyakazi wake unataka kuniambia taarifa za mawasiliano zilizotolewa ni za uzushi?
 
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.


Mbona hizi ni kama vile pumba tupu?

Mzee mwenzangu Kichuguu, hizi ligi umeanza lini?
 
Last edited by a moderator:
Kumbe hakuna anayejua chochote kuhusu Dr Ulimboka kutekwa anayejua ni yeye peke yake...kumbe Gazeti la Mwanahalisi linastahili kufungiwa kwa uchochezi, Kubenea acha kukurupuka Dr Ulimboka anawakana sasa...

R.I.P MWANAHALISI.

mbona umepanic gafla??
Subiri mapichapicha ndo yanaanza sasa.
 
Kama akili yake inafanya kazi sawia,angenyamaza na kuendelea na shughuli zake na kumuachia mungu yote maovu aliyofanyiwa na aliyoyafanya tena anatakiwa amshukuru sana mungu kwa matendo yote aliyomtendea na akumbuke kabisa mungu ana makusudi fulani na yeye ama aishi ili aone matokeo ya yale aliyokuwa akiyatetea au ajutie matokeo ya yale aliyokuwa akiyapigania,pia akumbuke kipigo alichokipata katika hili la kutetea maslahi ya madaktari kama kuana impact yoyote katika jamii hasa wale wapendwa wao walioenda mbele za haki kutokana na harakati zake,lakini pia akumbuke kuwa serikali ina mkono mrefu zaidi ya wa kwake katika kuhakikisha kuwa watu wake wanaishi kwa amani pamoja na yeye na kufurahia uhuru wao.na pia akumbuke kuwa watesi wake hawakushindwa kumtoa uhai kabisa wangeweza kufanya hivyo pasipo shaka lolote,ila mungu aliweka mkono wake kuwaepusha wasifanye hivyo kwa sababu fulani ambayo mungu pekee ndiye anayoijua na bado wapo na wanaweza kutekeleza mpango wao saa yeyote kama wakiona siri zao zinatoka nje,na mwisho akumbuke kabisa kuwa maisha ni karama ya mwenyezi mungu anaweza kuchukua karama yake wakati na saa yeyote anapoitaka na hakuna anayeweza kumzuia na kuishi ni kutimiza matendo yale yanayompendeza mungu.Tafakari chukua hatua.
 
ulimboka na yeye kama mwanasiasa tu,kama hataki kueleza ukweli bora akae kimya kuliko kuuza magazeti kwa habari ambazo hazina mantiki.!
 
hata wakimuua yanaweza kuwa makusudi ya mungu vile vile hakuna jambo zuri zaidi kwa sasa kama kuzunguza kilichotokea mbona mnaogopa sana kufa.
 

Ha haa, sidhani kama ulifikiria kwa makini kabla ya kuandika hii makitu.
 
kwa nini tigo imefukuza wafanyakazi wake unataka kuniambia taarifa za mawasiliano zilizotolewa ni za uzushi?
wakati mwingine ukikipenda kitu kiovu automatical unajikuta nawe unakua mwovu bila kujua macho anayo,masikio anayo,akili anazo lakini vyote havimsaidii sasa kama sio kufunikwa na uovu ni nini?
 


Wewe Ritz ndo hujaelewa kauli ya Dr. Ulimboka. Mimi naona alikuwa na maana watu wasiwahoji ndugu zake kama njia mbadala ya kupata habari

Kwa upande mwingine sina shaka na uchunguzi wa Kubenea. Alivyofanya Kubenea ndo hasa ilitakiwa ifanyike. Kwenda kwenye makampuni ya huduma za simu na kupata nakala ya mwenendo wa simu zilizoingia na kutoka simu ya Dr. Ulimboka siku ya tukio na siku chache kabla

@ Ritz unaielezeaje ile ya Ramadhani Ighondu(afisa kutoka Ikulu) kuwasiliana na mwenyekiti wa Mabwepande?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…