Dk Slaa: Wana CCM niungeni mkono nimng'oe Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Wana CCM niungeni mkono nimng'oe Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kinepi_nepi, Jul 28, 2010.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dk Slaa: Wana CCM niungeni mkono nimng'oe Kikwete Send to a friend Tuesday, 27 July 2010 22:50 0diggsdigg

  [​IMG] Dk Slaa

  Mussa Juma, Karatu

  MGOMBEA urais wa Chadema Dk Wilbroad Slaa, amezidi kupandisha joto la kisiasa nchini, baada ya jana kuomba nguvu za wana CCM wazalendo ili amng'oe Rais Jakaya Kikwete, hapo Oktoba.Ombi hilo la kuomba nguvu kutoka miongoni mwa wana CCM, limekuja kipindi ambacho chama hicho kikongwe barani Afrika, kikiwa kimepigwa na mawimbi mazito ya kisiasa, baada ya kuibuka makundi miongoni mwa vigogo wake.

  Akihutubia mamia ya wapigakura wake katika jimbo la Karatu ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru, Dk Slaa aliomba nguvu hizo akirejea mafanikio yake bungeni akisema, :"Yalikuwa ni mafanikio kwa maslahi ya taifa zima si Chadema."

  Kumbukumbu za bunge zitamuonyesha Dk Slaa kama mbunge aliyeibua kashfa nzito, ikiwemo wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ufisadi wa Meremeta na Tangold na Deep Green Finance.

  Kashfa nyingine kubwa ambazo aliziibua na kushikia bango ni pamoja na Kampuni ya Tanpower Resources, iliyowahi kuuziwa mgodi nyeti wa makaa ya mawe Kiwira.

  Tanpower Resources imekuwa ikitajwa kuihusisha familia mbili za Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na waziri wake wa Nishati Daniel Yona.

  Hata hivyo, katika kashfa hizo kubwa za kitaifa zinazohusu upotevu wa takriban sh 1trilioni, ni EPA tu ndiyo iliyochunguzwa na watuhumiwa akiwemo mfanyabiashara maarufu Jeetu Patel, kufikishwa mahakamani.

  Dk Slaa mgombea ambaye ameweza kufanyakazi hizo na nyingine kuibua ufisadi wa kitaifa, alirejea mafanikio hayo akisema ni faida kwa taifa zima hadi kwa wana CCM si upinzani pekee.

  Alifafanua kwamba, kwa taifa lilipofikia hivi sasa linahitaji mtu atakayeweza kufanya maamuzi magumu ili kuondoa hali ya kulindana.

  Mbunge huyo wa Karatu anayemaliza muda wake, alisema anaamini yeye anaweza kushughulikia matatizo makubwa ya taifa hili.

  Kwa mujibu wa Dk Slaa, tatizo la kulinda watuhumiwa wa ufisadi linatokana na kuwepo uongozi usio makini.

  Aliongeza kwamba, mafanikio ya uongozi wake yatakuwa ni kwa taifa zima hivyo akasisitiza, wana CCM wazalendo wanapaswa kumuunga mkono.

  Mwanasiasa huyo ambaye pia ameweza kuteka hisia za watu wa kada tofauti wakiwemo wasomi, alisema huu ni wakati wa kufanya mabadiliko.

  Katika siku ya pili ya mikutano yake ya kuaga wapigakura wake wa Karatu, Dk Slaa amekuwa akipaa kwa helikopta tarafa kwa tarafa.

  Ndani ya helikopta hiyo wamo pia mwenyekiti Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) Profesa Mwesiga Paregu.

  Kwa upande wake Profesa Baregu, alisema Dk Slaa hajapotea kugombea urais na kusisitiza, ni mtu mwenye uwezo mkubwa.

  Wakati huo huo, Mkurugenzi wa masuala ya bunge wa chadema, John Mrema, alieleza chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinavunja rekodi ya watanzaniua ambao watamdhamini Dk Slaa kuwania urai
   
 2. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde CCM tuungeni mkono, ni kwa ajili ya nchi yetu, tuikomboe tanzania.
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,744
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  Mungu amemtangulia katika yote. Uenende na amani ya bwana kila uendako kwa nia ya kuikomboa Tz. Wakati wa ukombozi umefika na wakati ni sasa.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ushindi ni Lazima................tuelimishe jamii ya Kitanzania.........kuwa wampigie kura Dr. Slaa
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni muda muafaka wa kumpatia Dr Wilbroad Slaa ulinzi wa uhakika kutokana na uungwaji mkono wa walio wengi kugombea urais wa Tanzania.Sasa kuna mabadiliko ya kweli ndani ya Tanzania yanakuja.
  Ulinzi kwa Dr W.Slaa ni muhimu kuliko vitu vyote kwa sasa.yuko kwenye hali ya hatari sana.Tunamuomba rais aliyeko madarakani na waziri mkuu wake wampatie ulinzi wa uhakika tusije juta baadae kabla ya uchaguzi tunampoteza kiongozi mahiri katika siasa za ushindani Tanzania.
   
 6. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180

  God forbid!
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Sky is the Limit! Amini msiamini, ccm waibe kura wasiibe, Dr Slaa will be our new President.
   
 8. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Say it again, and again and again!!!
   
Loading...