Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hana mpango wa kugombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.Juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alikaririwa akisema kama Dk Slaa ataamua kuwania ubunge katika jimbo hilo, chama kitaheshimu uamuzi wake akisema: Katika suala la kugombea, utashi binafsi ni jambo la msingi... kama Dk Slaa ataamua kugombea ubunge Arumeru Mashariki, tutaheshimu uamuzi wake.
Mbowe alisema Dk Slaa amekuwa akiombwa kugombea ubunge katika maeneo mengi ikiwemo Igunga na chama hakikuwahi kumlazimisha kwani jambo la kwanza ilibidi mwenyewe aonyeshe utashi binafsi wa kutaka kuwania kiti hicho.Dk Slaa aliwahi kuombwa akagombee Igunga lakini hakwenda. Hii ni kwa sababu anakubalika karibu kote nchini, hivyo kama atakuwa na utashi binafsi kwanza, nadhani taratibu za chama zitatumika tu kufikia uamuzi, alifafanua.
Lakini akizungumza katika mahojiano maalumu na Kituo cha Televisheni cha Mlimani jana, Dk Slaa alisema hafikirii kuwania ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa kuwa kazi yake ni kukijenga chama kitaifa ili kiweze kupata wabunge wengi.
Alisema hawezi kujifunga kwenye jimbo moja wakati alishasema kuwa kazi yake ni kutetea wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa kukijenga chama chake.Siwezi kujifungia kwenye jimbo moja, nilishasema kazi yangu ni kukijenga chama ili kiweze kupata wabunge wengi, alisema Dk Slaa.
Source: Mwananchi
Maoni yangu
Namshkuru sana sana Dk. Slaa kwa kufanya maamuzi haya yenye busara, ni ukweli usiopingika kuwa hata angeamua kugombea asingeshindwa, ila tatizo lililopo ni hawa wenzetu wangefanya michezo yao ya kila aina ili Dk. apoteze ushindi ili wapate ya kusema. Dk. endelea kukijenga chama ili 2015 tuwe na wabunge wa kutosha na hata ikibidi tuishike nchi.