Dk Slaa, Prof Lipumba mambo bado moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa, Prof Lipumba mambo bado moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  WAGOMBEA urais kwa tiketi ya vyama vya Chadema na CUF jana waliendelea na kampeni zao wakitumia mbinu tofauti za kujenga hoja, huku Willibrod Slaa akimtaka mkuu wa wilaya kupanda jukwaani na Prof Ibrahim Lipumba akiilaumu serikali kwa kuwabana kodi watu wa chini na kuwachia matajiri na makampuni makubwai.

  Akiwa wilayani Same, Dk Slaa ambaye anagombea urais kwa tiketi ya Chadema alimkaribisha mkuu huyo wa wilaya, Ibrahim Marwa kupanda jukwaani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Kwasakwasa na kuungana na viongozi wengine wa chama hicho, lakini alikataa.

  Marwa alisema kuwa hawezi kupanda jukwaani kwa kuwa yeye alifika katika eneo kusikiliza tu hivyo hangeweza kukaa mbele ya wananchi.

  Kitendo hicho kilimuudhi Dk Slaa ambapo alisema kuwa kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kugoma kupanda jukwaani ni kutoitendea haki Chadema na kitu hicho ni cha kichokozi.

  "Unachokifanya mkuu wa wilaya si haki na kitendo hiki ni cha kichokozi," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema kuwa kwa mujibu wa sheria mkuu wa wilaya ni mlezi wa vyama vyote vya siasa hivyo hakupaswa kugoma kukaa jukwaa kuu na viongozi wa Chadema.

  "Kikwete akipita hapa na nikiona umekaa jukwaa kuu nitalia na wewe ili mshahara wako ambao ni kodi za wananchi ufutwe na utolewe kwenye kazi hiyo," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema kuwa amefanya kazi na mkuu huyo wa wilaya wakati wa kamati za bunge katika wilaya yake na walikuwa pamoja, lakini haamini kama amegoma kukaa nao jukwaani.

  "Sikutegemea kama ungenifanyia hivyo na tumefanya kazi wote," alisema Dk Slaa.

  Akiwahutubia wananchi wa eneo hilo Dk Slaa alitumia muda mwingi kumchambua mbunge wa jimbo la Same Magharibi aliyemaliza muda wake, Dk Mathayo David Mathayo kwa kumtaka aache kuwadanganya wananchi kuwa amefanya kitu wakati hakuna kitu chochote alichowafanyia wananchi.

  "Mathayo ampishe mwanaume wa Chadema awasaidie wananchi kwa kuwa Mathayo ameshindwa kazi na amekuwa akitoa fedha kwenye shule ambazo haziwezi kuwasaidia kitu chochote,"alisema Dk Slaa.

  "Nilikutana na Mathayo bungeni baada ya kutoka jimboni kwake akaniuliza kwa nini nimemshtaki kwa wapigakura wake na mimi nikawaambia nimewaeleza ukweli na ndiyo maana Mathayo hanisalimii," alisema Dk Slaa.

  Naye Frank Kimboy anaripoti kutokas Pangani kuwa Prof Lipumba, ambaye anawania urais kwa tiketi ya CUF, ameendelea kujenga hoja kuhusu gharama za safari za mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete akisema zinatafuna fedha za walipa kodi.

  Pia alisema serikali imekuwa makini katika kukusanya kodi kwa kampuni ndogo za wazawa ndani ya nchi wakati kampuni kubwa, hasa zile za sekta ya madini zikifurahia misamaha ya kodi.

  "Tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, zaidi ya Sh11 trilioni zimepotea na hazina maelezo ya maana na nyingi zimetumiwa vibaya katika rushwa kubwa kubwa kama ile ya mkataba tata wa Richmond na kashfa nyingine ambazo bila shaka mtakuwa mmezisikia,” alisema Prof Lipumba.

  Alisema serikali ya CCM imeshindwa kuwajibika kutoa maelezo kuhusu matumizi ya zaidi ya Sh 11.8trilioni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Alisema kuwa fedha hizo huenda zimetumika kwa shughuli tofauti na matumizi ya serikali au ziliibwa na wanasiasa wasiokuwa na maadili.

  Mojawapo ya matumizi mabaya ya fedha hizo alisema Profesa Lipumba na manunuzi ya ndege ya rais ambayo ni ghali inatumia mafuta mengi kiasi cha Sh9 milioni kwa saa moja inapokuwa angani.

  "Kutokana na safari nyingi alizozifanya Rais Kikwete nje ya nchi, mnaweza kuona ni kiasi gani cha fedha za walipa kodi kilivyoteketea," alisema Lipumba.

  chanzo.Dk Slaa, Prof Lipumba mambo bado moto
   
 2. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tukichagua ccm wakati hu inakula kwetu
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyo Mkuu wa Wilaya hana "confidence". Ina maana hata Chadema ikimkaribisha chakula hatakula kwa sababu ni upinzani? Sasa alihudhuria hapo ili akasikilize nini?
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ibrahim Marwa, baada ya kupoteza ubunge mwaka 2005 mbele ya mwana-ccm mwenzake Vedastus Mathayo, alijikuta amepoteza mwelekeo kisiasa.
  Bahati iliyoje, JK akamkumbuka kwenye ufalme wake, akamteua kuwa DC. Alibaki na mshangao kwa kuwa hakutarajia hisani hiyo, sasa leo kukaribishwa jukwaani ili aketi na wanasiasa wenzake, tena chadema wanavyowaheshimu viongozi wa kiserikali lakini yeye kakataa kata kata. Tatizo lake ni kwamba hajiamini, anajishuku kwamba anaweza kutengenezewa zengwe na wenzake halafu JK akimtosa atakula wapi? Mwenzenu analinda kibarua chake, na bahati mbaya sana hajitambui ndio maana kaogopa kukaa jukwaani, mumsamehe bure huyo "wakunyumba".
   
 5. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Prevention is better than cure; use the principle whenever unsure of anything. Heri nusu shari kuliko shari kamili!
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  It is now high time for Dr.SLAA's advisors to insert clearly to him that he should now concentrate on sensatization to voters on how they should prepare themselves to be keen on guarding their beloved votes.

  Ni kwamba;
  • ni vema DR.SLAA awaelezee zaidi wapiga kura ile haki yao ya kulinda kura na haswa kipengere cha uhuru wa kukaa mita 100 toka eneo la kituo cha kupigia kura
  • Walinde kura usiku na mchana waachane na usingizi hadi matokeo yatoke
  • Dr. sasa aelezee zaidi atachokifanya kwa watanzania na apunguze kulipua mabomu ikiwezekana alipue tu mapya na yenye impact kubwa kama hili la DC kukaa mchangani kama alivyofanya mgombea wake jana alipoomba kura makete
  • Elezee zaidi serikali yake itakuwaje udogo wake hadi chini mimi naona hili la ufisadi limetosha lisije baadae likowa-bore voters ni maoni yangu sijui wewe
  Nawasilisha
   
 7. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Kama SLAA atashindwa si kwa kuibiwa kura, itakuwa ni kwa sababu ya mikoa hii mitatu. SHINYANGA, TABORA NA MWANZA. Ina watu wengi mno vijijini halafu hawajui chochote kuhusu chama kingine cha siasa, wengine hata ukiwauliza ataje jina la mgombea uraisi mmoja tu wa mwaka huu, kama adhabu ni kuchinjwa akishindwa ni obvious utamchinja. Siku hawa watu wakiamka kama ambavyo wamasai wameamka sasa hivi, nchi yetu itaokoka. Hii mikoa watu ambao ni waelewa ni wanaoishi mijini pamoja na walioko karibu na migodi. Kwenye maeneo ya karibu na migodi hata babu mwenye miaka 90 ambaye hajui hata aeiou ukimuuliza kitu cha siasa anakujibu kama profesa wa chuo kikuu, kule mambo yamewadondokea sana ndiyo maana kila mtu ameshaamka!
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Musiogope kabisa,SLAA anatumia muda mwingi kunadi sera na ilani safi ya chadema...na mabomu lazima yaendelee kulipuliwa ili wachanganikiwe kwan hata ccm huwa wanaongea yao..thic iz politics
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180

  Umechemka mikoa uliyotaja tayari ilishawahi kukaa chini ya upinzani vinginevyo huna kumbukumbu nzuri za mfumo wa vyama vingi Tanzania, kumbuka
  • Mzee mapesa ameanza kuwa mbunge wa magu-Mwanza 1995,
  • Bariadi-shinyanga imewahi inaendelea kuwa chini ya upinzani
  • Kisesa-Shinyanga imewahi kuwa chini ya UDP na Erasto tumbo
  Shinyaga ni sehemu chungu sana kwa mwaka huu hata chama tawala hakijagusa huwezi kuamini ni Dr.Slaaa pekee ndo kagusa kwani anajua siri iliyoko shinyanga hiyo ni HIMAYA YA BOB NYANGA MAKANI-usipimeUsijiaibishe ndugu: changuza utabaini mjomba
  Taja maeneo kama singida dodoma just to mention but few
  Nawasilisha  • Urambo-Tabora imewahi kuwa chini ya NCCR -Mageuzi
   
 10. C

  Chuma JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  SLAA alitakiwa kujua kufika tu kwa Mkuu wa Wilaya ktk Mkutano wake ni Heshima kubwa. Hivi ni Wakuu wa Wilaya gani wanahudhuria Mikutano ya Kisiasa ya vyama vya Upinzani?...Kumkaribisha ni vema, lkn kama kakataa si vema kuanza kurushiana maneno...!!!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ajitayarishe kuondoka ofisini baada ya tarehe 31.10
  Kwa hili hana uchaguzi. Ngoja basi tutaona!
   
 12. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naomba niandike kwa herufi kubwaaaaaaa. UNAAKILI SANAAAAAAAAAAAAA, NIMEPENDA MAONI YAKO!!!!!!!!!, SASA TUNAHITAJI MIKAKATI ITAKAYO FANIKISHA UCHAGUZI NA KUJENGA NCHI. UFISADI ASIONGELEE TENA BALI AONGELEE JINSI ATAKAVYO WAKWAMUA WANANCHI NA LINDI LA UMASKINI UNAOZIDI KUONGEZEKA, MFANO MAJI BARABARA, UMEME, ELIMU, AFYA, TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO, KUDHIBIT MAPATO KAMA TRA WANAVYOIBA, KUZIBITI WAWEKEZAJI WANAOTOROSHA DHAHABU HUKO KAHAMA KWA KUJA NA HELIKOPTA, NA MENGINEYO.............................
   
 13. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nadhani mkuu wewe ndio ulitakiwa kuchunguza zaidi kabla ya kuandika hii post yako.

  Sioni sababu ya kuwa bias hata kama wewe ni msukuma au mzaliwa wa mikoa hii iliyotajwa. Kwanza takwimu zako, majina na mpangilio inaonesha wazi kuwa unachanganya mambo. Pili, kuwa au kuwahi kuwa chini ya upinzani hakuifanyi sehemu husika kubadili takwimu zilizopo wala hicho sio kipimo cha ubora wa ufahamu wa watu wa sehemu husika.


  Ukweli ni kwamba, sehemu hizi za Shinyanga, Mwanza mpaka Tabora ki-jiografia ni kubwa sana kwa maana ya square metres za eneo. hivyo kutokana na hilo kumechangia sana eneo hili kuwa na idadi kubwa ya wakazi kiasi cha kuifanya miundo mbinu na mahitaji muhimu kuwa yasiyotosheleza mahitaji husika. Tatu ni kwamba sehemu kubwa ya maeneo haya shughuli kubwa ni Ufugaji, Uvuvi na kilimo. ukichanganya na mila za makabila husika utakubaliana na mimi kuwa kipaumbele cha Elimu kwao hakipo, ndio maana takwimu zinaonesha kwamaba Wasukuma ni wengi kuliko kabila lolote tanzania, ila ndio kabila lenye wasomi wachache sana ukilinganisha na makabila mengine.


  Pointi iliyopo hapa ni kwamba, endapo hii rasilimali watu katika mikoa hii itatumiwa vizuri, haina shaka itakuwa na impact kubwa sana katika mabadiliko yanayohitajika. Anachosema Makanyaga ni kwamba kama chama cha siasa kitatumia vizuri hii rasilimali watu katika mikoa hiyo, kitakuwa kimejikusanyia kura nyingi sana. Ikumbukwe kwamba watu hawa wengi wamejiandikisha hasa baada ya kuambiwa kujiandikisha huko kutaambatana na utambuzi wa raia halisi wa tanzania ( Vitambulisho vya uraia) Hivyo Slaa na Chadema kwa ujumla wasilipuuze wala kulisahahu eneo hili maana lina hazina kutoka na na wingi wa watu wenye ufahamu mdogo juu ya maendeleo ya kweli ya nchi yao.
   
 14. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lu-ma-ga naona sasa unachanganya mambo, Chama tawala kutogusa huko haimaanishi kuwa hilo ni eneo CHUNGU kama ulivyoliita hapo up-stairs, Ila inatokana na mipango iliyopo maana wanajua kuwa hapo imelala hazina ya ushindi. Tunachotaka sisi ni kwamba Dr. Slaa na chadema yetu kwa ujumla ilitambue hili ikiwezekana wafanye liwezekanalo ili mradi waliweke tena hili eneo katika ratiba ili kuhakikisha hatupotezi kura au rasilimali kura zilizopo. If we really want changes lazima tujipange maana kampeni ni karata the way unavyo zichanga na kuzipanga vyema ndio unavyo tengeneza nafasi nzuri zaidi ya kushinda gemu.
   
Loading...