Dk. Slaa kurejea ofisini CHADEMA

Dk. Slaa kurejea ofisini CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Dr Slaa hana mpango wa kurejea CHADEMA

Source: Mimi nimeongea nae
Lool! tunamsubiri tuu arudi maana sisiem wanaongea mengi sana......mwaka huu lazima kieleweke tuu, MABADILIKO HOYEEEEEEEE.....UKAWA JUUU
 
Bora arudi tu..maana hakuna namna..UKAWA inazama kwa kasi ya ajabu..
 
Lool! tunamsubiri tuu arudi maana sisiem wanaongea mengi sana......mwaka huu lazima kieleweke tuu, MABADILIKO HOYEEEEEEEE.....UKAWA JUUU

Hapa sishangilii kwa nguvu mpka nisikie yupo UFIPA na picha zimepigwa........ila kiukweli moyoni siku imeanza kuwa njema.

Dr. Slaa ni nembo ya Chadema. Nitafurahi kumwona akirudi. Lakini ikiwa kuna mapungufu ambayo anaona hayawezi kurekebishika hakuna namna inabidi apumzike tu kama dhamira inavyomtuma

Dr Slaa rejea ofisini usiwasikilize Maccm na washirika wao maana wamedhamiria kuimaliza safari yako kisiasa kwa aibu kubwa. Wewe ni mtu unayeheshimika na unalipenda taifa hili hebu wapuuze wote wanaokutaka utekeleze gari stand ili wapate fursa ya kuiba spares navkukwamisha safari.

Nyie nyumbu juzi tu mlikuwa mnamtukana yeye na familiayake...leo mnasema anarudi?? Wanafiki wakubwa nyie
 
karibu kamanda ili wana wa lumumba wawashwe zaidi
 
Naiona ccm ikitumbukua katika korongo lisilo na ukomo
karibu ofisini mh sana Dr Slaa.
ukawa ni mpango thabiti wa Mungu kwa wakati huu muafaka.
.
 
duh mnaumwa sana ugonjwa haueleweki, kapigeni ramli ilikujua nini kimewasibu, maana ukweli hamtaki kuukubali
 
Vyombo vya habari kadhaa vimeendelea kuripoti kuhusu Katibu Mkuu wa Chama, Dk. Slaa Kwa namna mbalimbali, Kwa leo vipo vilivyohabarisha kuwa atarejea Ofisini leo.

Naomba kusaidia katika hilo ili kupunguza usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wanahabari (ambao wanataka kujua itakuwa saa ngapi), wanachama, wapenzi, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA kwamba;

Kurejea kwa Dk. Slaa ofisini baada ya kumaliza likizo ya kutafakari aliyokubaliana na chama, hakutakuwa kwa siri.
Haitafanywa siri kwa sababu; kwanza hata mapumziko yake hayo hajafanywa siri. Ufafanuzi ulitolewa Kwa uzito mkubwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe.

Pili hakuwezi kuwa siri kwa sababu vyovyote vile kwa viwango vya habari, hiyo itakuwa ni habari kubwa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania.

Tatu; haitakuwa siri Kwa sababu wanachama watapenda kushiriki jambo hilo.

Hivyo basi mara Dk. Slaa atakapomaliza mapumziko ya kutafakari na akarejea ofisini, Kwa uzito ule ule uliotumika kusema kuwa yuko likizo aliyokubaliana na chama, tutawataarifu Watanzania wote, vikiwemo Vyombo vya Habari ili visiendelee kuandika tetesi ambazo zinawasababishia usumbufu wananchi na waandishi wengine.

 
Hata mh.Lipumba tunakuhitaji sana kuliko wewe unavyo dhani Tz kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom