Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
Tutashiriki midahalo yote ya uchaguzi. Kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama, Dk. Slaa inaweka wazi namna ambavyo CHADEMA kitashiriki midahalo mbalimbali inayohusu uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu, malengo yakiwa ni kuwapatia ufahamu wa kutosha wananchi kwa ujumla ili wafanye maamuzi sahihi kutokana na uelewa wa masuala ya uchaguzi, pia kuwafikia wapiga kura wa aina mbalimbali kupitia njia tofauti.
Huku akihoji kama kinachoandaliwa na CEOrt ni kongamano au mdahalo, Katibu Mkuu Dk. Slaa amesisitiza mambo muhimu yanayoweka ushiriki bora wa CHADEMA katika midahalo ya uchaguzi, amesema;
1. CHADEMA inaendeshwa kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi sasa taratibu
zetu hazijafikia kupata aspirants wa urais (watangazania).
2. Kama kuna waliopata aspirants, CHADEMA bado mchakato wetu unaendelea.
3. Midahalo inafanywa kwa msingi wa ilani. CHADEMA ilani yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi, yaani Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa tunazungumzia ilani ipi?
"Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika."
Kauli ya Dk. Slaa kupitia Gazeti la Mwananchi ambalo lilitaka kujua ushiriki wa CHADEMA kwenye mdahalo wa wagombea urais kama ulivyokuwa umetangazwa kupitia facebook na watu CEOrt.
Makene