Dk Slaa azindua kampeni Kalenga

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Iringa. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa jana alizindua kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, Grace Tendega, huku akionya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuongezewa posho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kalenga, Dk Slaa alisema chama hicho kimemtuma Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe kuhakikisha posho haziongezwi.

“Naomba kabla ya kuendelea nitoe salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amebaki Dodoma kutokana na kuteuliwa kwenye Kamati ya Uongozi inayoshughulikia masuala yote ya Bunge la Katiba. Kamati ile inashughulikia masuala yote likiwamo la posho na tumemwambia mwenyekiti wetu ahakikishe posho haziongezwi,”alisema Dk Slaa na kuongeza:

“Yeye ndani ya kamati yupo peke yake na wengine wote ni CCM, tutahakikisha anawashinda, wakimshinda sisi tutatoka nje,”alisema.

Katika kampeni hizo, Dk Slaa alisisitiza kampeni hizo za ubunge zifanywe kwa amani na kwamba chama chake kitakuwa cha mwisho kuona damu ya wananchi wa Kalenga inamwagika.

Alisema katika kampeni nyingi zilizopita Chadema imekuwa ikisingiziwa kuwa ndiyo imekuwa chanzo cha vurugu, lakini ukweli ni kwamba hizo ni propaganda za chama tawala.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Kimila wa Kabila la Wahehe (Mtwa) ambaye alihudhuria kampeni hizo, Abdul Sapi Mkwawa alimtaka mgombea wa chama hicho, Grace Tendega kufanya kampeni zake kwa amani huku akisisitiza kuwa hilo ndilo ombi lake.

“Mimi nimeitwa na nimekuja sababu mimi ni kiongozi wa watu wote, ninatoa baraka zote kwa dada yangu Grace, ninamwombea kwa Mungu aendelee na kampeni zake kwa amani hadi atakapomaliza,”alisema Sapi.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao aliwataka wakazi wa Jimbo la Kalenga kutokubali kununulika na kusisitiza kuwa wakati umefika wa kujikomboa kutoka kwenye ukoloni wa CCM.

Alisema atakuwa wa kwanza kushangaa kama wananchi hao watamchagua kiongozi ambaye hajui matatizo ya Kalenga kwa kuwa muda mwingi ameishi nje ya Kalenga.

Naye Mgombea wa Jimbo hilo, Grace aliwaomba wakazi wa jimbo hilo wamchague ili aende bungeni kushughulikia matatizo yao.

Mwananchi
 
Kumekucha Kalenga tnaomba kampeni za kistaarabu watuu wenye midomo michafu kama Lusinde hawatakiwi huko.
 
huyu mama grace yuko chini ya uangalizi wa hawa viongozi wa chadema:
1. lema- mbakaji wa dada flora wa uk.
2. slaa- mporaji mke wa mtu bi. josephine mushumbus. ametelekeza mke na watoto.
3. mbowe- anazini na mbunge wake wa viti maalum mpaka kazaa nae. ametelekeza mke wa ndoa na watoto.
JE, huyu mama yuko salama kweli?
 
kama slaa kaweka maguu na gongo zake kule mjue hamuwezi shinda hata robo ya kura
 
huyu mama grace yuko chini ya uangalizi wa hawa viongozi wa chadema:
1. lema- mbakaji wa dada flora wa uk.
2. slaa- mporaji mke wa mtu bi. josephine mushumbus. ametelekeza mke na watoto.
3. mbowe- anazini na mbunge wake wa viti maalum mpaka kazaa nae. ametelekeza mke wa ndoa na watoto.
JE, huyu mama yuko salama kweli?

......Kwa mawazo yangu...siasa za aina hii si wakati wake huu.....tujaribu kubalika kidogo......Kwa mawazo yangu
 
Wataisoma namba ccm.vp dentist nae ameenda iringa?ila kule nafikiri ataenda maana kuna tembo kule.
 
Hongereni sana Makamanda, nawatakia kila la heri na ushindi mnono. Wanakalenga fanyeni kama Arusha maccm yakileta hela kula pesa kura CHADEMA
 
Ndugu Hapo chini nime QUOTE, Hotuba ya Dr Slaa – Iringa Kutoka Gazeti la Mwananchi, Kinacho shangaza ni kuwa huyu Kiongozi ama kweli siasa zake ni za uchochezi, Posho imeombwa na wabunge wenyewe, na Serekali haina nia ya kuongeza, Kama huo usemi wake una ukweli wowote si kwanza wao "wangetoa Tamko la kichama kuwa ‘WABUNGE WAO WOTE HAWATACHUKUA NYOGEZA YOYOTE YA POSHO, NA HUO NDIO MSIMAMO WA CHAMA CHAO NA ATAKAYE VUNJA AMRI ATACHUKULIWA SHERIA YA KICHAMA" Badala ya kuingiza siasa mbovu kwenye mambo ya campaigne. Jee Slaa hakuna alijualo isipokuwa kuandama { tutahakikisha anawashinda, wakimshinda sisi tutatoka nje,"alisema."}

" Dk Slaa azindua kampeni Kalenga
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kalenga, Dk Slaa alisema chama hicho kimemtuma Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe kuhakikisha posho haziongezwi.
"Naomba kabla ya kuendelea nitoe salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amebaki Dodoma kutokana na kuteuliwa kwenye Kamati ya Uongozi inayoshughulikia masuala yote ya Bunge la Katiba. Kamati ile inashughulikia masuala yote likiwamo la posho na tumemwambia mwenyekiti wetu ahakikishe posho haziongezwi,"alisema Dk Slaa na kuongeza:
Yeye ndani ya kamati yupo peke yake na wengine wote ni CCM, tutahakikisha anawashinda, wakimshinda sisi tutatoka nje,"alisema."
 
Jitambue ww usiwe kama mfilisifu wa busara ucyejua kuwaza yako
huyu mama grace yuko chini ya uangalizi wa hawa viongozi wa chadema:
1. lema- mbakaji wa dada flora wa uk.
2. slaa- mporaji mke wa mtu bi. josephine mushumbus. ametelekeza mke na watoto.
3. mbowe- anazini na mbunge wake wa viti maalum mpaka kazaa nae. ametelekeza mke wa ndoa na watoto.
JE, huyu mama yuko salama kweli?
 
Kalenga,itipingi,ibanagosi,iban gamoyo,lupalama, igaluwaya,msombwe,kitapilimwa,welu,ifunda,ihemi,ulanda,tosamaganga na sehemu zote za jimbo la kalenga,chagueni maendeleo kwa kumpigia kura ndugu Grace Semvanda mla bagia na mishikaki mwenzetu.Huyu mla keki hatatusaidia kitu.
 
Wana Kalenga nao wanahitaji Chopa msiwabague Mbona Arumeru mlizipeleka! Slaa Leo anahubiri Uchaguzi wa Amani baada ya Dkt Jakaya kututaka kuacha Unyonge, Hongera Jabali la Siasa za Tanzania Mtukufu Dkt Jakaya Kikwete.
 
huyu mama grace yuko chini ya uangalizi wa hawa viongozi wa chadema:
1. lema- mbakaji wa dada flora wa uk.
2. slaa- mporaji mke wa mtu bi. josephine mushumbus. ametelekeza mke na watoto.
3. mbowe- anazini na mbunge wake wa viti maalum mpaka kazaa nae. ametelekeza mke wa ndoa na watoto.
JE, huyu mama yuko salama kweli?

TANGU KUANZA KWA 2014 hii NDIYO POST YA KIJINGA , YA KISHAMBA NA YA KIMASIKINI ZAIDI KWENYE JUKWA HILI ! UMEJIDHALILISHA SANA !
 
Back
Top Bottom