Dk Slaa apata wakati mgumu Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa apata wakati mgumu Kigoma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Oct 10, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Send tonday, 10 October 2010 08:32 0diggsdigg

  [​IMG] Dk Willibrod Slaa

  Joyce Mmasi, Uvinza
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema Dk Willibrod Slaa jana alikumbana na wakati mgumu pale alipoelezwa waziwazi kuwa hawawezi kumchagua mgombea ubunge aliyesimamishwa na chama hicho Jimbo la Kigoma Kusini, badala yake watampa kura David Kafulika wa NCCR Mageuzi.

  Kafulila aliyefukuzwa kazi makao makuu ya chadema na kuamua kukihama na kujiunga na NCCR-Mageuzi mapema mwaka huu, anagombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini.

  Wananchi hao wa Uvinza, walisema hawatamchagua mgombea ubunge wa Chadema, Asanali Muslim badala yake watampa Kafulila wa NCCR Mageuzi wakati wanamfukuza (Chadema) Dk Slaa alisema ni hawezi kushindana naye kwa ni mdogo kwa cheo huku akimfananisha na sisimizi.

  Wakazi hao walimwambia Dk Slaa kuwa chaguo lao la ubunge ni Kafulila wa NCCR Mageuzi ingawa kura zao za urais watampa yeye.
  Wananchi hao walipiga kelele za kumkataa mgombea wa Chadema alipoitwa jukwaani na Dk Slaa ili atambulishwe kwa wapiga kura.
  Dk Slaa alipowauliza wananchi kama watamchagua Muslim walijibu kwa sauti kubwa wakisema: "Tunamtaka Kafulila aliyewahi kuwa Afisa uhusiano wa Chadema kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi".

  Baadaye Dk Slaa alianza kunadi sera zake na kuwataka watu watakaompigia kura yeye kuwa rais wanyooshe mikono na wote walinyoosha.

  “Naona hapa kura ya urais zipo. Lakini huku (akimpigapiga bega Muslim) hakuna. Hapa Muslim unatakiwa urudi mara kumi,” alisema Dk Slaa.
  Wakati akijiengua kutoka Chadema, Kafulila alizua mvutano ndani ya chama hicho huku Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe, akijitokeza hadharani kumuunga mkono.
  Dk Slaa jana alizungumzia suala hilo akisema"Nasikia Kafulila anapita huko mitaani akitamba kuwa anaungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wetu, Zitto Kabwe. Nitamleta hapa kwenu (Zitto) aje athibitishe kama madai haya ya Kafulila ni ya kweli,” alisema Dk Slaa.
  Hii ni mara ya pili kwa Dk Slaa kukubalika na wananchi lakini wabunge wake kukataliwa mbele yake.
  Mara ya kwanza ilikuwa katika jimbo la Kyela mkoani Mbeya ambako Dk Slaa alilazimika kumnadi mgombea wa CCM, Dk Harrison Mwakyembe badala ya mgombea wa Chadema ambaye pia alikuwa anamnadi Mwakyembe.

  Akihutubia katika mkutano huo jana, Dk Slaa aliwaahidi wakazi mji wa Uvinza kuwa akifanikiwa kuingia madarakani, atashughulikia mgogoro wa muda mrefu kuhusu mafao na haki za waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha chumvi Uvinza waliopunguzwa baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa.

  Aligusia pia uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho kutumia nishati ya kuni katika uendeshaji wake na kuahidi kuhamasisha matumizi ya makaa ya mawe.Dk Slaa anayeendelea na mikutano ya kampeni mkoani Kigoma, pia aliahidi kuhakikisha mkoa huo unapata umeme wa uhakika utakaounganishwa na Gridi ya Taifa.
  Awali mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe alisema kuwa ujanja na mbwebwe alizokuwa nazo Bungeni, zilitokana na Dk Slaa na kwamba ndiye aliyekuwa mwalimu wake.
  "Ujanja na mbwembwe zangu Bungeni nilizipata kupitia mwalimu wangu Dk Slaa,'' alisema Zitto na kuongeza; "Katika majimbo kumi yaliyopo mkoani Kigoma, ninaomba wapinzani
  Wakati huo huo, Elias Msuya na Jackline Laizer

  wanaripoti kuwa, Chadema kinadai kwamba kimebaini wapigakura hewa milioni tatu walioandaliwa kwa ajili ya kuibeba CCM.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na meneja wa kampeni za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hii inatokana na ukweli kuwa idadi ya wapiga kura iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), hivi karibuni, hailingani na idadi halisi ya Watanzania ambayo sasa inafikia milioni 40.6.

  Hii ni kauli ya kwanza kutolewa na chama cha siasa tangu Nec itangaze siku tano zilizopita, kuwa watu wenye sifa ya kupiga kura waliomo kwenye daftari la wapiga kura, ni 19.6 milioni.

  Kwa mujibu wa Nec watu hao watatakiwa kupiga kura katika vituo 52,000 vilivyowekwa nchi nzima kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.

  "Idadi kamili ya Watanzania ni 40.6 milioni, kati yao walio na umri chini ya miaka 15 ni asilimia 44.4 sawa na watu 18.1 milioni huku walio chini ya umri wa miaka 18 wakiwa zaidi ya milioni moja. Hivyo waliobaki ndiyo wana umri zaidi ya miaka 18. Lakini kuna watu milioni tatu ambao wamechomekwa na Nec kupiga kura," alidai Profesa Baregu.

  Kwa mujibu wa Profesa Baregu, hata wale wenye sifa ya kujiandikisha kupiga kura kuna uwezekano kuwa asilimia 10 hawakujiandikisha kabisa. Kama ni hivyo alisema, idadi sahihi ya wanaotakiwa kupiga kura ni watu 16.6 milioni siyo 19.6 milioni.
  Profesa Baregu alieleza kuwa kutokana na utata huo Chadema itapeleka malalamiko yake kwenye mkutano wa Tume ya Taifa ya uchaguzi na vyama vya siasa uliopangwa kufanyika kesho.

  Lakini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Lewis Makame alipinga madai hayo akisema sio ya kweli.

  Jaji Makame alilieleza gazeti hili jana kuwa idadi ya watu inayotumiwa kwa sasa inatokana na sensa iliyofanyika mwaka 2002 hivyo kwa muda wote huo kuna watu walioongezeka.

  “Kwani sensa inayotumika kwa sasa ni ipi? Sasa tangu mwaka 2002 hapo kati kati watu si wameongezeka? Mtu yoyote anayejua kuwa ametimiza masharti ameandikishwa,” alisema Jaji Makame.

  Jaji Makame amewataka watu wenye shaka na takwimu hizo waende ofisini kwake kuthibitisha kwenye daftari la Tume la Wapigakura badala ya kulalamika mitaani.
  Naye Moses Mashalla anaripoti kutoka Arusha kuwa, Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei ameponda matokeo ya utafiti wa Redet yanaoonyesha kuwa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni.

  Mtei aliwataka Watanzania kuu upuuze utafiti huo kwa kuwa una lengo la kuwashtua na kuwakatisha tamaa.

  Mtei alisisitiza kuwa matokeo ya utafiti huo yalikuwa hayana dira bali yalilenga kuwakatisha tamaa watu wanaojipanga kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya uongozi nchini.


  Source mwananchi.


  My Take

  Nakumbuka Zitto alimpigania sana Kafulila yamkini alijua atakuja kuwa mbunge mtarajiwa
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kafulila niiimsikiliza midahalo yake ni mzuri huyu Muslim hawezi kujieleza vizuri
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  .... Hakuna taabu yoyote ni mpiganaji kambi ya wapinzani.. Anahaki ya wananchi wake..
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  chadema hapa naona washapoteza jimbo..its good kwani hata huyo kafulila ni from pinzani, ingekuwa mbaya sana kama angetokea CCM
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kigoma wana akili sana. Sijui kwa nini hawajaendelea. Nimeligundua hili kupitia mchakato majimboni. Wamchague tu kafulila akafanye kazi nzuri na zitto humo mjengoni
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Really? kweli miafrika ndivyo ilivyo..
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimelipenda jina la Mwandishi na Sehemu alipo................


  Joyce Mmasi, Uvinza.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  To me ningesikitika kama wangesema watampa MCCM kura zao as long as ni NCCR kanyaga twende
   
 9. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Watagawana kura huko na CCM wataibuka washindi.
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Why a red bolded quote kaka?
   
 11. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Ndio shida iko hapo.sasa utashangaa kura za kafulila na muslim zinazidi za ccm kwa mbali,lakini anashinda wa ccm
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Why calling a guy by his religion? Hatupo Nigeria.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakijaharibika kitu maadam Kafulila anawakilisha Upinzani tunamtakia kila la kheri isipokuwa tu tatizo ni kwamba ushindani umegeuka kuwa baina ya Chadema na NCCR - Mageuzi hivyo yeye na Muslim watagawana kura wakati mgombea wa CCM akipita mlango wa nyuma.
  Kuna uwezekano mkubwa wote wakapoteza jimbo hilo kwa CCM...
   
 14. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio umechapia big time, huyo jamaa habari inasema anaitwa Asanali Muslim. Sasa kosa la RayB ni nini hapo? Don't be too sensitive.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280

  La ajabu, REDET na SYNOVATE yote haya hawayaoni kwa sababu JK na CCM hawataki wayaone
   
 16. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Madam wamemkubali Rais, Kafulila naye ni Mtanzania atakuwa sehemu ya wapiganaji katika Bunge letu. Ili mradi wasimpe CCM
   
 17. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni wakati wa wananchi kuonyesha kiu ya mabadiliko ya kweli, tumechoshwa na ahadi zisizotekelezeka. Tubadilishe band labda nyimbo pia zitabadilika.
   
 18. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Bad officials are elected by good citizens who do not vote
   
 19. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  naomba tuelewe Uvinza ni nyumbani kwa Kafulila ndipo alipozaliwa na ndipo wazazi wake walipo kwa maana hiyo hayo yalitegemewa lakini upande mwingine wote wa kigoma kusini wanamtaka Moslim kwa maana hiyo tusitoe taarifa kwa eneo dogo tu la uvinza
   
 20. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kuwa wana kigoma kusini na kaskazini wameonyesha kuwa wanaupeo sana ktk maswali waliyokuwa wanauliza kwa wagombea wao.Cha msingi hapa upinzani uchukue jimbo bila kujali CHADEMA au NCCR. cha msingi hapa ni kutowadharau chama cha jembe na nyundo hawa jamaa wana wanachama wao wasiopenda mabadiliko kwa kuogopa yasemwayo na viongozi wa mf. mabadiliko yataleta vita. pia hawa jamaa wa ccm ni mabingwa wa kuchakachua kura hivyo si wakubezwa maana kigoma kusini wapinzani wanagawana kura wasipoangalia CCM wataibuka kidedea wadai wameibiwa muhimu hapo ni ku join team
   
Loading...