Elections 2010 Dk Slaa apata wakati mgumu Kigoma

naomba tuelewe Uvinza ni nyumbani kwa Kafulila ndipo alipozaliwa na ndipo wazazi wake walipo kwa maana hiyo hayo yalitegemewa lakini upande mwingine wote wa kigoma kusini wanamtaka Moslim kwa maana hiyo tusitoe taarifa kwa eneo dogo tu la uvinza

Nashukuru kwa kutoa ufafanuzi huo maana mimi sio muumini wa kuamini mtu akizomewa basi ameshindwa uchaguzi tukumbuke mzee makweta mwaka 2005 alizomewa akashinda pia kama ulipoeleza mgombea kazomewa wapi ikiwa kazomewa nyumbani kwa mpinzani wake bado ananafasi cha muhimu hapa ni kuwa CHADEMA n NCCR kigoma kusini wakae wajadili upepo wa kisiasa unavumia wapi maana na hofu CCM wanaweza kufanya mambo yao maana upinzani wanatoleana macho wenyewe na wanasahau CCM.

Ushauri kwa CHADEMA wakumbuke jinsi CCM walivyowashinda jimbo la BUSANDA katika uchaguzi mdogo.TINGATINGA mzee MALECELA anakiri upinzani ulikuwa unanguvu sana hivyo aliamua kutumia mbinu za medani kwa kuzama vijijini na kuomba kura kupitia nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu. hivyo CHADEMA wakiweza kuichukua mbinu hiyo ya wapinzani wao BUSANDA inaweza kuwatoa.

Cha muhimu wapinzani waunganishe nguvu amasivyo jimbo hilo lipo hatarini kubaki CCM
 
hiyo ya kafulila siyo ishu sana maana ndiye chaguo lao.
lakini hii ya umati kusema kuwa URAIS tutakupa (Slaa) lakini ubunge kwa..... naamini kuna watu mahala fulani presha inapanda, presha inashuka
 
Back
Top Bottom