Dk. Slaa amshukia IGP Mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa amshukia IGP Mwema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkodoleaji, Jun 27, 2011.

 1. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]na Abdallah Khamis

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, kutoa ufafanuzi wa zaidi ya sh bilioni 220 zilizopotea katika idara mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
  Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, mwishoni mwa wiki alipohutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Kampala, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
  “Ninamshauri Mwema kama anataka siasa avue magwanda yake na aje tufanye siasa kwa kuwa sasa ameamua kuisemea serikali, nilifikiri angetumia muda wake kwa ajili ya kutolea ufafanuzi ripoti ya CAG ya April 2010 iliyowasilishwa bungeni Machi na Aprili mwaka huu inayoonyesha kiasi cha zaidi ya bilioni 220 kutojulikana zimetumikaje ndani ya jeshi lake,” alisema.
  Alisema kati ya fedha hizo, sh milioni 800 zimepotelea katika Jeshi la Magereza peke yake, huku wafungwa walio katika magereza nchini wakikosa huduma zinazostahili ikiwamo kupata chakula bora, na kiasi kilichosalia ni katika idara mbalimbali ya jeshi la polisi.
  Aliongeza IGP amekuwa na ujasiri wa kukemea wanasiasa huku akishindwa kuonyesha ujasiri wa kujiuzulu katika nafasi yake kutokana na kushindwa kuchukua hatua kwa maovu yanayofanywa katika maeneo mbalimbali yanayolindwa na jeshi lake, linalopokea kodi ya Watanzania waliofanywa kuwa na hali duni na serikali ya CCM.
  “Hivi wizi wote wa EPA, Meremeta na matukio mengine yaliyofanyika maeneo hayo yote si yanalindwa na Jeshi la Polisi? Kwa nini asiyatolee ufafanuzi na badala yake anaona wanasiasa wanataka kuvuruga amani. Kama kuyasema haya ni kuvuruga amani basi ninajua hapa mpo usalama wa taifa na polisi nendeni mkamwambie sisi tutayazungumza kila siku na aje atukamate,” alisema Dk. Slaa.
  Mbali na hilo, Dk Slaa aliwatahadharisha viongozi wa dini kuepukana na ghilba za jeshi hilo kuwatumia kama kivuli cha kuficha maovu ya serikali iliyo madarakani.
  Alisema IGP anaona kitendo cha wanasiasa kuzungumzia upungufu wa serikali iliyo madarakani kama uchochezi, bila kujua vyama hivyo vipo kisheria kwa ajili ya kuikosoa serikali pale inapoenda kinyume na matarajio ya Watanzania.
  Akizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru, Dk. Slaa alisema dhana nzima ya Uhuru uliokuwa ukielekezwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa sasa umekuwa ni kama hadithi ya kusadikika.
  Huku akinukuu baadhi ya vifungu toka katika kitabu cha ‘Binadamu na Maendeleo’ kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere, Dk. Slaa alisema Mwalimu alielezea uhuru katika njia tatu ambazo ni Uhuru wa Kujitawala, Uhuru wa kutosumbuliwa na njaa maradhi na umaskini pasipo sababu za msingi na uhuru wa mtu binafsi.
  Alisema uhuru wa kutosumbuliwa haupo katika nchi yetu kwa kuwa hii leo kuna maeneo mengi watu wanataabika kwa njaa, maradhi na umaskini uliokithiri huku serikali ikijinadi kwa takwimu zisizoweza kumsaidia Mtanzania wa hali ya chini.
  “Mwalimu alisema katika kitabu chake hiki (anakionyesha kitabu hicho) na hii ilikuwa ni hotuba yake ya mwaka 1968 kuwa maendeleo si kuwa na takwimu za ujenzi wa barabara, nyumba nyingi na mazao hizo ni nyenzo za kuendea maendeleo, sasa tuangalie haya yanayosemwa ni maendeleo kama yamemnufaisha Mtanzania aliyeko vijijini?” alihoji Dk. Slaa.
  Aidha, alisema maadili ya uongozi nchini yaliondoka enzi ya utawala wa Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi, hivyo kusema tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru bila kuwa na mlingano wa mapato na kile kinachoitwa maendeleo ni kujidanganya.
  Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed, aliwataka Watanzania wasihadaike na kelele zinazopigwa kwamba kuna vyama vya upinzani vina ajenda ya udini, kwa kile alichokieleza kuwa ni propaganda zinazotumiwa kwa lengo la kuwagawa Watanzania wasizungumzie matatizo yao.
  Alisema hali ngumu inayopigiwa kelele na vyama vya upinzani ni kwa manufaa ya watu wote bila kujali dini zao na kwamba inahitajika nguvu ya pamoja kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa. Source: Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huyu slaa kila siku ni tuhuma tu! Hana kitu kipya cha kutueleza wananchi?
   
 3. N

  Nzogupata Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima utaponda tu kwakuwa zinawasaidia kujenga miskt. Kwani unataka uhalalishe wizi kwa jeshi linalohangaika kusema intelijensia kila siku nakusindikiza misafara ya mahindi nje ya nchi?

  Yawezakana zinzfznyz biashara ya mahindi huko holili
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unataka serikali isifiwe kwamba imefanikiwa ili iweje? maendeleo ni haki yetu na ni wajibu wetu. Kama hatujafanyikiwa basi tunapaswa kujilaumu.
   
 5. h

  hans79 JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  acha kaul mfu,watawala wanakwepa majukumu yao kwa undumilakuwil ulowajaa vichwan mwao.Dr Slaa ananena ukwel,CAG alitaka ufafanus toka serikalin had leo kimya,je kwan wanampa majukumu huku wanaogopa maumivu?achanen na unafik nchi ina hal mbaya
   
 6. delabuta

  delabuta Senior Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe unataka aisifiee kwa lipi kunyanyasa wananchi we kibaraka kaa pembeni usawa mbaya huu , hiyo amani mnayotudanganya nayo mwisho wenu magamba umefika.
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Nitarudi asanteni.
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ishu za misikiti zinatoka wapi? Wewe fahamu jamaa kaishiwa hoja! Hana jipya! Kila siku ufisadi ufisadi!
   
 9. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wewe kwa akili yako bila slaa ungejua mambo mengi machafu yanayofanywa na viongoz wako?
  Ndugu yangu hata kama haujui kusoma hata kuangalia picha uwezi?
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani muafaka uliosimamiwa na Horst Kohler si umemeliza uhasama wa kisiasa kati ya cdm serikali na ccm kwa upande mwingine? au kuna kingine jamaa wanataka?
   
 11. Jean chill

  Jean chill Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hatakiwi kuacha kuwatuhumu mafisadi hadi pale ufisadi utakapokoma. Na kwa hili anaonyesha yeye ni jasiri asiye babaika. Unataka aje na jipya lipi wakati hayo ya kale yenyewe hayajatekelezwa? Kwa mfano: Umeahidi utaninunulia gari, keshokeshokutwa unasema meli, then ndege, wakati mgari lenyewe bado? Hakuna kukoma hadi kieleweke waelewa maana yake? (Ukiona hivo jua hakijaelewwka bhanaa) Slaa endelea kuwatuhumu watuhumiwa hadi wakome kufisidi.

  Asante!
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kuwa makini wewe , inaonyesha ni jinsi gani ulivyo na mzaha
   
 13. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dr Slaa si mtu wa kawaida kawaida aisee, moto mwingine huu!...
   
 14. h

  hans79 JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  ufisad umeisha tz?fikir kabla ya kutenda,una maslah na ufisad ndo maana unajambajamba tu.
   
 15. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Kazi kuu ya UPINZANI ni kupinga serikali pale inapofanya vibaya. Serikali imeshindwa kusimamia vizuri utendaji wa Jeshi la Polisi. Kwanini UPINZANI usishutumu hilo? Kama UPINZANI unashutumu serikali kila siku ni kwa sababu serikali hii ya sasa inafanya makosa kila siku.

  Ama unashangaza. Zitumike vibaya shilingi bilioni 220 kisha usitake Slaa ashutumu? Unaelewa kweli shilingi bilioni 220 zilivyo nyingi? Ni fedha za kutosha kujenga madarasa 22,000 ya gharama ya shilingi milioni 10 kila moja!

  Ni huu wizi wa kila siku wa vigogo wa CCM ndio umefanya Tanzania tukawa wa mwisho sana kwenye vitu kama Elimu hapa Afrika Mashariki. Soma takwimu hizi hapa chini kama hutakasirika na kuishutumu serikali kama anavyofanya Slaa.

  According to the Ministry of Education and Vocational Training statistics, Tanzania secondary school gross enrolment rates stand at five per cent while Kenya stands at 26 per cent, Uganda 12 per cent, Zambia 28 per cent and Zimbabwe 44 per cent

  http://www.theeastafrican.co.ke/news/Tanzania+seeks+science+and+maths+teachers+from+EA/-/2558/1185108/-/item/1/-/11h4719/-/index.html

   
 16. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ina maana huoni mazuri ya serkali yetu! Kuna vya kupinga lakini siyo kila kitu
   
 17. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimefurahishwa na hii sentensi"hatuwezi kupima maendeleo kwa takwimu". Eti barabara ,shule UDOM tumejenga! Swali kubwa hapa ni kwa miaka hamsin ya uhuru tumefanya nin na hawa maadui watatu' maradhi,ujinga na umasikin.Kama elimu inayotolewa sio bora,watu wakiugua wanenda kwa babu au kutibiwa nje ya nchi na zaidi ya watanzania milion 12 wapo chin ya mstari wa umasikin,miaka 50 ya uhuru ina mushkeri.Mwema atolee jawabu upotevu wa hizo pesa maana zingesaidia kuwashinda hao maadui watatu.
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hatuwezi kusema ueisha, lakini Serikali ni makini na inalishughulikia hilo swala! Umeona suala la mafisadi lilivyoshughulikiwa! Tumeona watu wakiwajibishwa. Tumeona watu tena waliokuwa viongozi wakubwa serikalini wakipelekwa mahakamani.
   
 19. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Pole sana. The opposition is not supposed to be an independent assessor of government. Ndio maana inaitwa UPINZANI. Si kazi ya upinzani kutangaza mazuri ya serikali. Huelewi hayo?
   
 20. A

  Akiri JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  we unataka uelezwe kitu gani jambo la upotevu wa 220bn unaona ni kitu kidogo, hawa vijana wa nape vp? ebo!
   
Loading...