Dk. Slaa akamata nyaraka ya siri ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa akamata nyaraka ya siri ya serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 13, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Wilbrod Slaa, ameiumbua tena serikali ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kufichua waraka maalumu wenye lengo la kudhibiti na kufuatilia kwa makini nyendo za watumishi wa serikali wanaoshabikia vyama vya upinzani.

  Akihutubia juzi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nzovwe na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Dk. Slaa alisema waraka huo kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi ) unawataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kufuatilia na kupeleka takwimu za wafanyakazi wanaojihusisha na siasa sehemu za kazi.

  Alisema ili kutimiza azma hiyo wametakiwa kuorodhesha kila mtumishi kwa majina kamili, kazi anayofanya, cheo kazini, itikadi ya siasa na cheo alichonacho ndani ya chama husika lengo likiwa ni kuwapata watumishi wanachama wa vyama vya siasa pinzani nchini.

  Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kila wakati na umati mkubwa watu, alisema hatua hiyo ya serikali ni ya hatari kubwa, na akaitaka kusitisha na kuacha kuwatisha wananchi walio huru ndani ya nchi yao.

  Alisema kinachojaribu kufanywa na serikali ni kutaka kudhoofisha nguvu ya upinzani, jambo litakalosababisha kuzuka kwa vurugu.

  "Mchezo huu si mzuri na hauwezi kuvumilika hata kidogo kwa kuwa nchi hii ni yetu sote na yenye kutawaliwa kwa mfumo wa vyama vingi na hawa watumishi wanaruhusiwa kuendesha siasa wakati wa nje ya kazi, kwa nini serikali iamue kutoa waraka huu?" alihoji.

  Dk. Slaa alisema ndani ya waraka huo kuna maelekezo kuwa Katibu Tawala yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu hayo aliyopewa na wizara basi jina lake litapelekwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ili ashughulikiwe ipasavyo.

  Alisema CHADEMA itaendelea na maandamano nchi nzima kupinga baadhi ya mambo ya kifisadi ambayo serikali inayafanya na kamwe hawataogopa kufanya hivyo hata kama watakamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani.

  Aidha Dk. Slaa katika suala zima la uundwaji wa Katiba mpya alisema Chama cha Mapinduzi kupitia kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilitoa waraka uliowataka viongozi wa chama hicho ngazi zote kusimamia zoezi hilo katika kuhakikisha mawazo yote yatakayotolewa na wananchi yawe kwa manufaa ya CCM.

  Alisema alifikiri kuwa mchakato wa Katiba ni kwa manufaa ya Watanzania wote kumbe CCM inauchukulia kwa manufaa yake na si ya wananchi.

  "Tazameni, yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa yanayofanywa na viongozi hawa, badala ya kujadili mambo ya mustakabali wa nchi juu ya hali ngumu ya maisha kwa wananchi, wao wanapanga ni jinsi gani watatekeleza azma yao ndani ya Katiba mpya kwa maslahi ya CCM na si ya Watanzania," alisema.

  SOURCE:TANZANIA DAIMA
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Heee ukiwa mtumish wa Umma waraka haukupiti,
   
 3. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  isijekuwa kama kontena la kura la tunduma,kifo cha Rc au mikutano ya lacairo mwanza
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  "Ccm imebaki na mabomu na bunduki tu. Maana hata wanaozishika ni cdm damu!"- Godbless Lema
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sasa chama gani kinajengwa namna hiyo?
   
 6. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa ccm wajinga kweli, ukiwa mtumishi wa serikali halafu ni kiongozi wa ccm sawa. Ukiwa mtumishi wa serikali halafu ni shabiki tu wa upinzani si sawa, hivi hawajui kuwa mwisho wao unakuja?
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  mijitu ya ccm ndivyo ilivyo..wamegundua watumishi wa umma wanaichukia ccm kuliko wakati mwingine wowote sababu mishahara duni lakini wakubwa wanajipangia mishahara na miposho mikubwa plus mianya ya ufisadi..
   
 8. S

  Sheba JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia.

  Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.

  Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida.

  Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa.

  Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi.

  Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?

  Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huu ni uzushi wa kisiasa.ameshindwa kuwadhibiti wabunge wake wanaokula posho aka ujira wa mwia anadandia asoyajua.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ivi siku ile kwenye juice pale magogoni kwa nini alikula kona?AU ALIONA AIBU
   
 11. k

  kipinduka Senior Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu dk wa din hana jipya kwan be4 huu waraka hakuwepo mpaka leo ajifanye umesambazwa,lkn cshangai yeye c alikuwa m2mish wa kanisa ndio maana anaona mageni kwake,jaman ushaur wa bure alud kanisan akam2mikie
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Labda haufahamu UPINZANI ni nini na unafanyaje kazi. Vinginevyo Dr Slaa yuko sahihi kabisa kufahamu mbinu zote chafu dhidi upinzani. Uliwahi kusikia kashfa ya "Watergate"?
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naomba nikuulize swali kidogo tu-Kwako wewe ni halali wakuu wa mikoa kuwa wajumbe wa kamati za siasa za CCM?
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  okkkk poleni watumishi wa umma, karibuni kwenye kujiajiri
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  serikali ya CCM na wote wanao iunga mkono humu wana ni kama wameishachanganyikiwa kwabisa, wana panga mikakati ya kijinga kabisa dhidi ya CDM,...

  Ngoja niwape siri moja na ya kweli ili kui win CHADEMA... CCM na mashabiki waanze kupiga kazi na kuwatumikia wanachi kwa dhati si ujanja ujanja,..hali za maisha za wananchi ziwe nzuri na mabo kama hayo...

  Lakini kwa upuuzi huu unaoendelea hata humU JF kuwa eti ndiyo njia sahihi ya kuifanya CCM ipendwe na serikali yake, ni kuzidisha chuki tu.... yaani tunawachia mno CCM na vibaraka vyake vyote.
   
 16. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  pumbavu wewe.
  Nyaraka kandamizi kama hizi kuna ubaya gani zikiibwa.
  2015 inakuja ndo matajuta kutukandamiza watumishi.
   
 17. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ile wizara ya Tamisemi, this time ina mtaalamu kweli kweli. Ni wale mabingwa wa zamani wa mbio ndefu na ngumi nzito nzito kama kina Tyson. Anafikiria kama yuko kwenye Dunia aliyoiunda mwenyewe wala sishangai
   
 18. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wewe si ni miongoni mwa hao magamba wanaonufaika na rasilimali za nchi hii na kuwaacha watanzia wakitaabika? acha ushamba wako
   
 19. k

  kada1 Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwongo huyo, akawadanganye hukohuko kanisani alikokuwa akitumika, mzushi huyu siwezi kumuamini hata kidogo, tangu azushe issue ya kontena la kura, mfuko wa cement kuwa 5000 na mengine mengi simwamini huyu.
   
 20. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acha utumwa wa mawazo kaka. Kinachozungumziwa hapa ni SIASA MAHALI PA KAZI na sio SIASA WAKATI WA KAZI. Wewe ungetumia akili yako vizuri kufikiri, ungegundua ni nini CCM wanaogopa na ndio maana wanatunga sera za ajabu. Nakupa mfano wa walimu: wana matatizo mengi na serikali imeyafumbia macho kwa muda mrefu. Kwa kuwa imani yao kwa serikali imeshuka, si ajabu ukawasikia now and then wakisema hili na lile kuhusu harakati za CDM na ukombozi wa wanyonge. Hili ndilo linaloiumiza kichwa CCM na serikali yake.

  Kuhusu suala la Nyaraka, Dr.Slaa hajaiba waraka na hana nafasi ya kuiba waraka wowote ule serikalini. Kinachotokea ni kwamba yeye huletewa nyaraka hizi zenye nia chafu na watu waliojitolea kuinusuru hii nchi . Kinachoisumbua CCM ni mbinu chafu dhidi ya wananchi na ndio maana nyaraka hizi zinaitwa za siri, lkn ukiangalia sababu za kuwa ni siri ni UBAYA WA MAUDHUI YAKE. Hivi kwa akili yako, unafikiri mtu mwenye akili timamu atlichukia suala hili ikiwa hata Nyaraka za EPA nazo zilipatikana hivi hivi?

  Kama unaamini agizo hili ni jema na lina msingi mzuri wa kuimarisha ustawi wa jamii, ni vipi lisitolewe kama Government Notice kwenye gazeti la serikali badala yake uwe waraka wa siri?

  Ndugu yangu wewe unaathiriwa na u-CHAMA zaidi ya Utanzania. Juzi hapa tumeoneshwa waraka mwingine tena umeandikwa na CCM badala ya serikali kwenda kwa wahisani kuelezea muendelezo wa lile sakata la EPA just kuwaridhisha ilhali kwenye field fedha zenyewe hazipo hata zile zilizorudishwa zimetafunwa tena. Tuendelee kucheka na serikali au kuungana kuiumbua kwa mabaya yake?
  Kama wewe unafaidika na ufisadi baba, tusamehe. Kwangu mimi ni sawa kabisa kwani serikali inatakiwa iwe kwa ajili ya wananchi na sio wananchi kuitukuza kwa kila madudu inayofanya. Nani anaipa serikali haki ya kuwapangia wananchi vyama vya kuvifuata?
   
Loading...