Nchi hii tunacheza michezo ya hatari kweli. Hainiingii akilini kama tunaweza kuthubutu kushabikia kitendo cha mtu kuiba nyaraka ya serikali wenyewe tunasema 'akamata'. Kuiba nyaraka ya serikali ni jambo la hatari kwa uhai wa taifa lolote haijalishupi umefanywa na nani? Leo Dr. Slaa anaiba nyaraka ya Serikali na tunamshangilia. Mbinu hii itatumika dhidi ya Serikali ya CHADEMA siku itakapojaaliwa kuingia madarakani. Mchezo huu ukiendelea, hakuna Serikali itakayotawala. Kitendo hiki kinadhoofisha Serikali na sio kitendo ch kushabikia hata kidogo, na ndio maana kuna sheria ya bunge dhidi ya kitendo hicho. Bahati nzuri Serikali yenyewe in huruma huruma hivi.
Lakini la pili ni kuwa, tunataka sasa kuhalalisha ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa. Hii ni hatari nyingine. Kitendo cha kunajisi utumishi wa umma na siasa, aidha kusaidia Chama Tawala au Chama cha Upinzani ni kitendo cha hatari na kukemea. Watumishi wa umma wakifanya kazi kisiasa hakuna maendeleo yatakayopatikana na hatari ya hujuma aidha dhidi ya wapinzani au serikali inaweza kuwa kitu cha kawaida. Sioni tatizo lolote kuhusu Waraka huo wa kukataza watumishi wa umma kutoshiriki shughuli za siasa. Waraka haukatazi mtumishi wa umma kuwa mwanachama, kinachokatazwa ni kuwa kiongozi wa chama au kufanya shughuli za chama cha siasa mahala pa kazi. Waraka huu unawasaidia pia CHADEMA kuliko tunavyotaka kuaminishwa. Watumishi wa Umma wakiamua kutumika dhidi ya CHADEMA ustawi wa Chama hicho utakuwa mashakani. Inawezekana walioko kwenye utumishi wa umma wakawa CCM wengi kuliko CHADEMA kama ambavyo inawezekana pia wakawa CHADEMA wengi kuliko CCM. Lengo la Waraka huu ni kulinda maslahi ya umma wote na haki yao ya kupata haki na huduma kutoka katika utumishi wa umma bila kujali itikadi. Pengine nielezwe humu ni nchi gani na wapi ambapo utumishi wa umma wanaruhusiwa kujihusisha na siasa za vyama mahala na wakati wa kazi? Kwa nini sisi tuwe wa kwanza?
Tusikubali kutumiwa kuhalalisha mbinu haramu kwa sababu tu ya kutaka kufikia maslahi yetu ya kisiasa. CHADEMA wakumbuke, mbinu hizo hizo zitatumika dhidi yao wakiwa madarakani.
Ndugu yangu Sheba utaniwia radhi kwa lugha nitakayoitumia kupingana na hoja zako.
1. Usifikri Dr. Slaa ni mjinga na wala Watanzania ni wajinga. Unapaswa kuelewa kipi hasa kinachostahili kuwa siri ya serikali katika maana halisi na kipi hakistahili. Ipo sheria zinazotumika kulinda siri za serikali na hivyo anayezitoa na anayesitumia anastahili kushtakiwa kwa mujibu wa sheria hizo( kwa sasa sina muda wa kuzirejea). Mwamvuli wa sheria hizo usitumike kutuletea uposhaji kama wa kwako. Dr. Slaa hata siku moja hatashtakiwa kwa sheria hizo kwa maana yako ya uelewa wa siri za serikali. Hizo zinazotajwa kuwa ni siri ya serikali ilistahili kuitwa upumbavu wa serikali.
Wakati fulani Dr. Slaa alipokuwa mbunge alisema anazo nyaraka za serikali na ushahidi kuhusu wizo wa EPA na Richomodn nk. Aliibuka waziri mmoja kwamba Dr. Slaa atachukuliwa hatua za kisheria kwa kukutwa na nyaraka za serikali. Upande mwingine Spika akasema kuwa ushahidi wa Dr. Slaa ni feki kwa sababu ameutoa kwenye mitandao. Kuhusu kushtakiwa, Dr. Slaa aliwaambia wakamshtaki lakini hakuna hata mmoja aliyefanya hivyo. kwa suala la Richmond hakuna asiyefahamu yaliyotokea. Hakuna mahala popote duniani ambapo wizi unaendeshwa na serikali halafu useme ni siri isipokuwa hapa Tanzania.
Matumizi ya serikali yanapitishwa na bunge katika vikao vya bajeti, huu uchukuaji wa fedha kutoka benki kuu kwa ajili ya matumizi yasiyoeleweka ndiyo siri ya serikali? Bwana Sheba kama una akili ambayo imeacha kufikiri tafadhali usitumie kutoa mawazo kama hayo kwa Watanzania wenzako. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubalina na upumbavu wako.
Waraka wa serikali kwa Makatibu Tawala kuhusu suala la kuandikisha watumishi na vyama vyao ni aina ya upumbavu mwingine wa serikali. Watumishi wanaongozwa na kanuni na miongozo ya kiutumishi. Maagizo kama hayo hayana sifa ya kuwa nyaraka za siri za serikali kwa sababu yana malengo mabaya na yana harufu ya Chama tawala kinachotamani kubaki madarakani kwa nguvu na siyo kwa ridhaa ya wananchi. Kama kanuni za utumishi hazikutaka watumishi watoe taarifa zao za uanachama katika vyama vya siasa, kumetokea nini hadi makatibu tawala waagizwe kufanya kazi ya kishushushu kazi ambayo hata TISS imewashinda kuifanya kwa ajili ya maslahi ya umma?
Kila mwananchi analo jukumu la kuilinda serikali iliyo halali. Kwa sasa Serikali hii ya CCM inaonekana haipo kwa ajili ya maslahi ya umma na wautu hawana hamu ya kuiona inaishi. Kama serikali inaamua kuwanyanyasa wananchi iliopaswa kuwatumikia kuna mategemeo yoyote ya kulindwa. Ni serikali ipi duniani iliyo kwa ajili ya wananchi wake inawaacha wezi wa mali za umma wanashindwa kupelekwa hata mahakamani? Ni serikali ipi inayodai wananchi waipelekee ushahidi wa wizi wa fedha za umma kama vile yenyewe haina vyombo vya kuweza kuwajua? Ni serikali gani duniani iliyo kwa ajili ya maslahi ya umma inashindwa kuwashtaki watuhumiwa hata pale ilipopelekewa ushahidi?
Ndugu Sheba, hiyo siri ya serikali unayoitaka iwe siri haistahili kuwa siri kwa wananchi wa Tanzania. Hivi wewe (mke) ukilietewa siri ya mkuwa mumeo ana hawara utaichuliaje? Huyo aliyekuletea siri utamwona ni mtu mbaya? Kwa mantiki hiyo, kama Wananchi wa Tanzania ndiyo wanye mamlaka ya mwisho juu ya nchi yao, unadhani siri inayohusu serikali kuwaibia wananchi mali zao na kuibaka demokrasi yao inastahili kuwa siri, na kuwa ni kitu kibaya wananchi kuifahamu?