Mfungeni Silaa, muzidi kjipotezea 2015, japo najua hiyo mbinu italenga kumuweka ndani mpaka uchaguzi wa 2015 utakapopita
Mimi naamini kabisa hawa watu watamtia Slaaa ndani: kwamba amekosa au la. Hii ni njia ambayo Mungu amepanga Tanzania ikombolewe. Ili watu waweze kuichukia serikali dhalimu, ni lazima ifanye jambo litakalowaudhi wengi kiasi kwamba hapatakuwa na mjadala.
Na hii ndiyo historia inavyofundisha. Wakimfunga Slaa, basi lile tumaini pekee la watanzania litakuwa limefifia. Na hapo ndipo patatokea kukata tamaa. Na hakuna mpiganaji mzuri kama aliyekata tamaa! Ndo hapo ule msemo " umekwisha ewe Babeli, malaya, ...." utakapofanya kazi.
Na ndipo jiwe toka kusikojulikana litakapokuja na kupondaponda ufalme huu dhalimu wa CCM. Na hapatabaki jiwe litakalosimama: Si Mwinyi, Mkapa, Msekwa wala Malechela watakaonusurika! Naam anguko litakuwa kubwa zaidi kwa wale waliojiingiza na familia zao ! Kilio kitakuwaje kwa JK na Riz One! Ole wake Makamba na January! Ole wa kina Kawawa na wengineo! Siku zinakuja za kulia na kusaga meno! Umekwisha ee CCM......umekwisha huna pa kushika! Utanasukaje kwenye kashfa hizi: EPA, Meremeta, IPTL, Net Group, TRL, Dowans,TTCL ,Kiwira, Mwananchi GM, Uporaji Tanzanite, Kilombero Sugar, Mgororo Paper Mills.........utajinasuaje na wizi wa Richmond, Rada, Ndege, Utajitoaje kwenye uporaji ATCL, NBC, NMB ewe CCM?