Dk Slaa achafua hewa kwa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa achafua hewa kwa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 11, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,870
  Likes Received: 83,348
  Trophy Points: 280
  Dk Slaa achafua hewa kwa Pinda Tuesday, 10 May 2011 21:36

  Edwin Mjwahuzi, Mpanda na Boniface Meena Sumbawanga
  Mwananchi

  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa amechafua hali ya hewa katika Jimbo la Katavi lililopo Mkoa mpya wa Katavi ambalo Mbunge wake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwaambia wananchi kuwa: "Kiongozi huyo anafurahia anasa za uwaziri mkuu."Dk Slaa alifanya mikutano mitatu ya hadhara jimboni humo jana katika vijiji vya Majimoto, Mbende na Usevya, alikozaliwa Pinda ikiwa ni mfululizo wa maandamano na mikutano inayofanywa na chama hicho katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

  Alisema Pinda anatembelea magari yenye gharama kubwa ambayo thamani yake ni Sh500 milioni huku wasaidizi wake nao wakipanda yaliyo na thamani ya Sh200 milioni wakati wapiga kura wake wana hali ngumu ya maisha.

  "Nikiangalia hali ya maisha yenu wananchi wa jimbo hili, Mkoa wa Rukwa na Katavi si haki ninyi kuendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na nyasi wakati kodi zinafujwa kila kukicha kwa matumizi ya anasa ya Serikali hii," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema mbali na anasa hiyo, semina elekezi kwa mawaziri inayoendelea mkoani Dodoma imegharimu fedha nyingi na kwamba iwapo serikali ingekuwa inawajali wananchi wake, ingeweza kujenga shule za sekondari katika jimbo zima la Waziri Mkuu kwa kutumia fedha zinazotumika katika semina hiyo.

  "Leo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wako Dodoma kwenye Semina Elekezi, wanatumia kodi za wananchi na baadaye wanarudi kuwakamua kwa kupandisha gharama za maisha na kutoza kodi kubwa," alisema.

  "Kikwete amewateua mawaziri kisha anawaandalia semina za kazi gani? Kama hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wabunge wengine? Alisema mawaziri walioshindwa kufanya kazi wajiondoe wenyewe. Kwani anajua mawaziri wake hawafai, lakini badala ya kuwafukuza anawapa ruksa wajiondoe wenyewe!"

  "Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000 ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi anayelinda usalama wenu. Lakini magari anayotumia kwenye msafara wake yasiyopungua 30 gharama yake haipungui Sh600 bilioni. Gharama ya gari analotembelea mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vitano vya afya."

  Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.

  "Inasikitisha kuona mbunge wenu anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua katika nyumba yake iliyopo Usevya badala ya kupeleka umeme ambao ungeweza kutumiwa na wananchi wote. Nyinyi wenyewe mnaona kwenye nyumba yake pale kuna umeme wa nguvu ya jua, wakati ninyi wapigakura wake mkiwa kwenye dimbwi la giza hamuoni kama ni ukatili mkubwa? aliuliza.

  Zitto amjibu Waziri Mkulo
  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema atamthibitishia bungeni, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kuwa Serikali imefilisika.Zitto alisema jana mjini Sumbawanga kuwa wataweka hadharani jinsi Serikali ilivyokopa fedha benki ili Waziri Mkulo aweze kuwajibika kutokana na kauli yake aliyoiita ya kukataa kusema ukweli.

  Alisisitiza kwamba serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15.

  "Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali katika makusanyo ya kodi zote imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha. Hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi," alisema Zitto.

  Kwa mujibu wa Zitto, Machi, mwaka huu Serikali ilikopa fedha katika Benki ya Exim na benki zote za biashara nchini na ilikuwa ikihangaika ili iweze kuwalipa wafanyakazi.
  "Mkulo atueleze ni serikali gani duniani inakopa kwenye benki za biashara kwa kuwa kitendo hicho ni hatari sana kwa nchi," alisema na kuongeza:"Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa ni Sh11 trilioni ambayo Serikali ilishindwa kufikia malengo ya Sh 1.6 trilioni kutokana na kushindwa kukusanya kodi kwa asilimia hiyo 15 isipokuwa ushuru wa forodha."
  Alimtaka Mkulo kuacha kuwaona wanaosema kwamba serikali haina fedha si wazalendo kwa kuwa wawekezaji hawatakuja nchini, bali atambue kuwa kukosekana kwa fedha si suala la uzalendo.

  "Serikali ni kweli haina fedha na hakuna suala la uzalendo katika hili. Tatizo la uwekezaji ambalo analizungumzia, linatokana na sera mbovu za CCM kwa kuwa tangu mwaka 2007, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika hapa nchini," alisema Zitto.

  Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mji wa Vwawa, Mbozi, mkoani Mbeya hivi karibuni, Zitto alisema Serikali ina hali mbaya kifedha kwa sasa kiasi cha kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi.
  Alidai kuwa hali hiyo mbaya kifedha kwa serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi Mei 7, 2011.

  Alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.
  "Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharimia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata."Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharimia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  uzalendo my foot!waendelee kupiga danadana afu wakichoka watakiri kuchacha kama wananchi wao.matmizi yamezidi mapato,ngoja waelekezane vizuri.hiyo ya solar panel imenikumbusha nilifika kijijini kwa waziri mkuu mstaafu mh tingatinga kule mvumi,makaburi yaliyoko nyumbani kwake yana hadhi ya juu kuliko majority of the neighbouring houses.na kweli kila mtu atakula kwa kamba yake,asante kaka mkullo kwa kutujuza!
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  hahaaaaaaaaaaaaaaaaa

  thats CHADEMA,hongereni sana na endeleeni na makamuzi tuko pamoja for life
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  1.."Leo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wako Dodoma kwenye Semina Elekezi, wanatumia kodi za wananchi....

  2..."Kikwete amewateua mawaziri kisha anawaandalia semina za kazi gani?

  ...Kama hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wabunge wengine?
  ... badala ya kuwafukuza anawapa ruksa wajiondoe wenyewe!"

  3..."Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000....

  4....Gharama ya gari analotembelea mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vitano vya afya"

  Thank you CDM kwenda vijijini na kusema ukweli kwa wana wa nchi
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kaza buti CDM
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  humu jamiiforums kuna mambo!! Inabidi kila mwananchi aelekezwe namna ya kuaccess JF ili twende sawa!!
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  [​IMG]


  [​IMG]
   
 8. s

  seniorita JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na bado, kwa hilo mkuu Pinda kwenye atapindika maana ukweli umewekwa wazi. Asanteni CDM kwa kusema ukweli ambao mara nyingi kwenye siasa is a taboo....sasa kazi mbele kwa mbele na hewa itachafuka zaidi indeed....
   
 9. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndo "Kasi zaidi.... Nguvu zaidi.... Ari zaidi!!!!".... Big up CDM!!
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa bado kuna wananchi masikini wa nchi hii ni kama wamepewa "LIMBWATA" na CCM kiasi kuwa hawasikii chochote hata waeleweshwe ukweli vipi. Nawengine tunao humuhumu JF. Anyway, CDM kazeni buti maana hata "LIMBWATA" nalo huwa lina expire, ikiwa ni hivyo wataelewa tuu.
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  acha waibe ukweli! ukweli ujulikane wananchi wachukue hatua wenyewe! kutakuwa na kulinda kura kwa moyo woote!
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mwaka huu serikali italia sana, kwanza siri hakuna tena serikalini kitu kinafanyika sirini kesho kipo JF, mikononi mwa wana siasa. Halafu kinachosemwa sasa siyo majungu ni ukweli mtupu hapo ndipo jasho linapoitka serikali. Kifupi serikali iache ubabaishaji, iwape nafasi wachumi waishauri nini cha kufanya na isimamie zoezi hilo kwa ukamilifu.
  Kingine viongozi wake waweke mbele maslahi ya taifa, wajue kuvurunda kwa mmoja ni kuvurubda kw serikali yote.
   
 13. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakika tutajitoa Muhanga
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kama kweli Serikali imefikia kukopa pesa kwenye mabenki binafsi ya biashara kwa ajili ya kulipia mishahara wafanyakazi wake basi hiyo inaashiria wazi anguko la uchumi wa Nchi yenu.

  jamani kuweni makini na kuondoa porojo mnapozungumzia uchumi wa nchi kwani hilo ni kama pembe la Ng'ombe
   
 15. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo inaidwa Mwaga mboga na mwaga unga. Sijui huyu Mkullo anadhani watz bado wako kwa usingizi.
   
 16. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kudadeki serikali inakopa wananchi alafu inakusanya watendaji wake dodoma izitumbue hela ilizokopa?
  Natamani kung'ata mtu sikio.
   
 17. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pipooooooooooooooooooooo.............................!!!!!

  Yaani nadhani katika watu ambao hawapati usingizi ni JK maana kila siku Presha inapanda Presha inashuka.... akifikiria CDM inavyo muumbua na serikali yake anajuuutaaaaaaaa! kwanini aliwania tena urais kwa mara ya pili
   
 18. T

  TAITUZA Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wote walewale wako wapi cuf?'mpe mchawi mwanao aleeee!tatizo watanzania tushakuwa wezi watupu, hata ateuliwe nani ni yaleyale, wizi mtupu. C zitto, c slaa c mbowe, tukiwafuatilia kiundani nao watakuwa na yao tu, watanzania sasa hv tumetengeza mstari wenye umbo la duara, kila ntu anamwibia mwenzake mfukoni, alafu baadhi yetu wako ndani ya mstari huo huo halafu wanalalamika wanaibiwa.
   
 19. T

  TAITUZA Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfano uko ofisini umechakachua umepata fedha, unakwenda kununua gari unachakachuliwa unadanganywa hili lilitengenezwa mwaka juzu kumbe ni la miaka 12 iliyop[ita, haya unakwenda tra unakwepa ushuru unasajili gari, haya unakwenda kituo cha mafuta wanakuchakachua,haya unakuja barabarani unakutana na trafimki anakutafutia kosa lolote la lazima anakuchakachua, gari badala ya kudumu matokeo yake hata miaka kumi halifiki bovu, unaanza kuwaza tena kuiba ununue jingine!
   
 20. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  pumba tupu
   
Loading...