Dk Salim, Nchimbi, Tibaijuka waula CCM

Dk Salim, Nchimbi, Tibaijuka waula CCM

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
HARAKATI za kupanga safu za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimehitimishwa usiku wa kuamkia leo baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) kuchagua wajumbe wa Kamati Kuu (CC).

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya kikao cha NEC jana, walioula kuingia katika chombo hicho kikuu cha uamuzi ndani ya CCM ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na mawaziri kadhaa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Dk Salim ambaye aligombea urais dhidi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, aliteuliwa jana kuwa mjumbe wa NEC na baadaye jina lake kupendekezwa kuwa miongoni mwa waliopigiwa kura za kuwa wajumbe wa CC.

Makada 14 wa CCM, saba kutoka kila upande wa muungano walipigiwa kura katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yalitangazwa usiku wa manane.

Kutoka Tanzania Bara, waliochaguliwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa na Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana.

Kutoka Tanzania Zanzibar mbali na Dk Salim, wengine ni Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi.

Pia wamo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Abeid Daftari pamoja na Khadija Aboud. Wajumbe hao wapya wanaunda Kamati Kuu pamoja na wengine wanaoingia kwa nyadhifa zao.
Vigogo urais watoswa
Uteuzi wa makada waliopigiwa kura uliwaweka kando vigogo ambao wamekuwa wakitajwa kuusaka urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015.

Miongoni mwa waliowekwa kando ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mawaziri waandamizi wawili katika Serikali ya Rais Kikwete, Samuel Sitta (Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa).

Kadhalika, majina makubwa ndani ya chama hicho kama vile January Makamba, Martin Shigela, Willison Mukama, Mohamed Seif Khatib, Omar Yusufu Mzee na wengineo hayakuwamo kwenye orodha ya waliopigiwa kura.

Baadhi ya makada walioanguka Balozi Ali Karume, Gwaride Jabu, Dk

Raphael Chegeni, Dk Cyril Chami, Michael Lekule Laizer, Ramadhan Madabida, Hassan Wakasuvi, Dk Fenella Mukangara, Shamsa Mwangunga na Said Mtanda.
 
Habari wakuu wa jamvi...
usiku wa kuamkia leo nimeoteshwa kuwa CCM katika uchaguzi ujao 2015 wanamsimamisha ndugu salim ahmed salim na atashinda kuwa rais wetu ajaye..

baada ya kuamka nikaanza kutafakali nikaona inaweza kuwa kweli ndoto yangu ikatimia kwa sababu zifuatazo:
1. Salim. A.S hana kashifa yoyote kama viongozi wengine wanaotajwa kutaka kugombea
2. Kuchaguliwa kwake ktk CC kuna mpa nafasi kubwa.
3. Marais wa awamu mbili zilizopita wote wametoka bara hivyo sasa ni zamu ya ZNZ
 
Sababu zote hasa ya 3 hazina mashiko kwa wakati huu lakini mi sijaota ila natamani ndoto yako iwe kweli,namwamin sana yule mzee!
 
Hiyo ni ndoto tu mkuu na bora tu ibakie kuwa ndoto kwa sababu rais anayekuja TZ atatokea CHADEMA. Tumechoka sana na ccm.
 
Urais hauna zamu acha upuuzi wako. Kwa mfano jana mimi niliota nimemuoa dada yako na akanizalia mapacha je ni kweli? Ndoto ni ndoto tu. Ukweli ni kwamba urais hauna zamu tunaangalia uwezo. Kwa sasa dr? Salim ni mzee anayehitaji kufanya kazi nyepesi. Isitoshe hizi ni nchi mbili tofauti zanzibar na tanganyika. Hairuhusiwi na haiwezekeni tanganyika nchi yenye watu mil 43 wawe koloni la nchi ndogo ya watu mil moja! Huu ni upuuzi kutawaliwa na wazanzibari. Rais ni dr slaa hakuna mwingine
 
Habari wakuu wa jamvi...
usiku wa kuamkia leo nimeoteshwa kuwa CCM katika uchaguzi ujao 2015 wanamsimamisha ndugu salim ahmed salim na atashinda kuwa rais wetu ajaye..

baada ya kuamka nikaanza kutafakali nikaona inaweza kuwa kweli ndoto yangu ikatimia kwa sababu zifuatazo:
1. Salim. A.S hana kashifa yoyote kama viongozi wengine wanaotajwa kutaka kugombea
2. Kuchaguliwa kwake ktk CC kuna mpa nafasi kubwa.
3. Marais wa awamu mbili zilizopita wote wametoka bara hivyo sasa ni zamu ya ZNZ

Vipi kashasafishwa kashfa ya kumuua Karume 1972?
 
Dr. salim angekuwa Rais kwa miaka mitano tu, ili vijana wetu wajiandae kutoka hapo, angeweza kuwa presidential material in transition.
 
Hii inanikumbusha mwaka 2011 ambapo watu kadhaa walioteshwa kuhusu 'dawa' za vikombe !!
Ogopa sana maswala ya 'kuoteshwa'....
 
Tushakuwa waganga wa kienyeji...! Tunaanza kujadili ndoto? Mmmmh!
 
ndoto huwa ni matokeo ya kazi nyingi za mchana kuna jamaa alikuwa anaota anaongea na mungu akizinduka anawasimulia washikaji zake kile alichokuwa anaongea na mungu, alipofariki marafiki zake waka-compile zile ndoto wakaita korani, matokeo hasi ya hizo ndoto dunia yote inayashuhudia, chungulia afghanistan ukikutwana tv set unafungwa ukikutwa na AK47 unaonekana raia mwema, kwa hiyo ndoto sio kitu kizuri na hazifai kusimuliwa.
 
Habari wakuu wa
jamvi...
usiku wa kuamkia leo nimeoteshwa kuwa CCM katika uchaguzi ujao 2015
wanamsimamisha ndugu salim ahmed salim na atashinda kuwa rais wetu
ajaye..

baada ya kuamka nikaanza kutafakali nikaona inaweza kuwa kweli ndoto
yangu ikatimia kwa sababu zifuatazo:
1. Salim. A.S hana kashifa yoyote kama viongozi wengine wanaotajwa
kutaka kugombea
2. Kuchaguliwa kwake ktk CC kuna mpa nafasi kubwa.
3. Marais wa awamu mbili zilizopita wote wametoka bara hivyo sasa ni
zamu ya ZNZ

Mtu ambaye alishiriki kumuua Karume atakuwa vipi rais?
 
Atachaguliwa na nani?
Kupitia chama gani?
Atakuwa raisi wa nchi au kikundi fulani?
 
Back
Top Bottom