Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
Na Victoria Msina, Uturuki
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu ameshinda tuzo ya mwaka huu ya Gavana bora kwa Afrika inayotolewa na jarida maarufu la Emerging Markets.
Kila mwaka gazeti hilo linalochapishwa jijini London, Uingereza, hutambua mafanikio yaliyofanywa na watendaji wakuu wa benki kuu na mawaziri wa fedha na kuwapa tuzo wakati wa mikutano ya Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Gazeti hilo linaongoza kwa kuandika habari zinazohusu mikutano ya Benki ya Dunia, IMF na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Limekuwa likifanya hivyo kwa miaka 18 sasa.
Sherehe za kutoa tuzo hiyo zitafanyika leo katika mji wa Binbidirek Cistern, Istanbul, Uturuki, ambako Gavana anahudhuria mikutano ya kimataifa.
Tuzo aliyopata Gavana Ndulu inatokana na kura za maoni zilizokusanywa kitaalamu na gazeti la Emerging Markets kutoka kwa magavana wa benki kuu wa nchi za Afrika na Ulaya, wawekezaji, wachumi na wachambuzi wa kimataifa.
Profesa Ndulu ametambuliwa kutokana na jitihada kubwa alizozifanya kuiongoza Benki Kuu ya Tanzania tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete Januari 2008.
Katika kipindi hicho, Gavana huyo amehakikisha kuwa hali ya uchumi wa nchi umetengemaa kwa kuhakikisha hali ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni na masoko ya fedha iko imara. Hadi mwishoni mwa mwaka 2007, viwango vya riba vya dhamana za serikali za muda mfupi vilikuwa vinapanda na kushuka kila wakati. Hata hivyo, hali hiyo imebadilika na kuwa tulivu, huku viwango vya riba vikishuka. Chini ya uongozi wa Profesa Ndulu, Benki Kuu haitegemei sana kuuza dhamana za serikali peke yake.
Kwenye upande wa ubadilishanaji wa fedha za kigeni, Julai 2007, mtu alihitaji kuwa na Sh 1,300 kupata dola moja ya Marekani. Hali hiyo imebakia karibu hivyo hivyo kwa kipindi cha miaka miwili ambapo sasa dola moja ya Marekani inabadilishwa kwa kati ya Sh 1,310 na 1,320.
Huko nyuma, viwango vya kubadilishana fedha za kigeni vilikuwa vinaongezeka kwa karibu asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka na kufanya thamani ya shilingi iwe inashuka tu.
Chini ya uongozi wa gavana Ndulu, akiba ya fedha za kigeni, katika kipindi cha miaka miwili imeongezeka kutoka dola za Kimarekani bilioni 2.4 hadi kufikia dola bilioni 3.6, sasa, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa hapa nchini.
Magavana wa benki kuu barani Afrika, wachumi na wawekezaji, pia wametambua jitihada za Prof. Ndulu kusimamia mzunguko wa fedha. Ukiondoa chakula, mfumuko wa bei uko katika asilimia 2, utendaji ambao pia unapongezwa na IMF.
Profesa Ndulu ametambuliwa pia kutokana na jinsi alivyosimamia kwa utaalamu mkubwa wa changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza wakati wa uongozi wake wa BoT, zikiwemo mdororo wa uchumi wa kimataifa na ufisadi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA).
Akizungumzia kuchaguliwa kwake kupata tuzo hiyo, Gavana Ndulu alisema: Tuzo hii inatokana na viwango vya utendaji kazi vya Benki Kuu. Ninafurahi kutambuliwa. Tuzo hii ni tuzo ya Benki Kuu ya Tanzania.
Mhariri wa Emerging Markets, Taimur Ahmad, anasema: Tuzo hii ni alama ya wazi kabisa ya imani ambayo wewe (Prof. Ndulu) umeijenga kwa wadau muhimu.
Washindi waliopita wa tuzo ya Gavana wa Mwaka wa Benki Kuu barani Afrika ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Zambia, Dr Caleb Fundanga na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria, Prof Charles Soludo.