Kama swali lako ni makubwa tu basi mie nitakutajia ni reform iliyofanyika baada ya kuwa yeye gavana, kusimamia uchunguzi wa EPA(kumbuka hakuna mshtakiwa aliyemtaja kuhusika), kupitia ajira za wafanyakazi na usimamizi wa uchumi katika kipindi hiki kigumu.
Aliyemteua Ndullu kuwa gavana ,ndio yeye ambae hakutaka Ballali ahojiwe juu ya EPA akiwa hai ilikuzuia ukweli juu ya wizi huo usijuklikane kwahiyo kwa kumteua Ndullu anajua hakuna siri yeyote itakayotoka; na ndio maana madeputygavana wawili waliokuwepo enzi ya Ballali hawajawajibishwa ingawa mmoja wao katajwa mahakamani [ RELI na MKILa] ili ku preserve status quo!! Ndullu hana ubavu wakuwazuia mafisadi wa ccm wasichote fedha BOT!! Kama asemavyo Bubu, mbona uchunguzi juu ya ufisadi wa Nimrod mkono kuchota hela BOT za uwakili hewa Ndullu hajausemea mpaka sasa?