Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,080
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Madaktari wa Hospitali ya Apollo, nchini India bado wanaendelea na uchunguzi wake dhidi ya ugonjwa unaomkabili Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu msemaji wa familia ambaye ni mbunge wa jimbo la Lupa (CCM) mkoani Mbeya, Victor Mwambalaswa, alisema bado haijafahamiki ni lini Dk. Mwakyembe atarudi kwa kuwa bado madaktari wake wanaendelea na uchunguzi.
Alisema kilichokuwa kimebainika kwenye seli nyekundu (Red bone marrow) katika mwili wake, madaktari walitegemea kukuta kimeisha ila walivyomfanyia uchunguzi bado wamekuta tatizo lipo.
Mwambalaswa alisema kutokana na hali hiyo madaktari wake wanaendelea na uchunguzi mpaka hapo watakapokamilisha suala hilo.
Alisema hali ya Dk. Mwakyembe inaendelea vizuri kwani huwa anawasiliana naye mara kwa mara.
Dk. Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi, Oktoba 9 mwaka jana, alilazimika kupelekwa katika Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu zaidi ambapo alirudishwa mwishoni mwa mwaka.
Baada ya kurudishwa hivi karibuni Februari 19 mwaka huu alisafiri tena kuelekea hospitalini huko kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi dhidi ya ugonjwa unaomsumbua.
CHANZO: NIPASHE