Dk. Mwakyembe amrushia Sugu kijembe

Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,220
4,059
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amejibu mapigo ya Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Mr. II, kwamba hana ubavu wa kumng'oa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2015 katika jimbo hilo.

Dk. Mwakyembe amesema hayo ikiwa ni siku tano baada ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mkutano katika kijiji cha Njisi Boda Kasumulu ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho kuzungumza na wananchi katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Katika mkutano huo Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi, alisema atahakikisha anamung'oa Dk. Mwakyembe katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa sababu ameshindwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wakulima wa kokoa katika suala la bei kutokana na kuwa na maslahi na makampuni yanayonunua zao hilo.

Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi hana ubavu wa kumng'oa mwaka 2015 hata kama atavaa ‘hereni' masikio yote mawili kwa sababu wananchi wa jimbo la Kyela wanafahamu mambo ya maendeleo aliyowaletea katika kipindi cha miaka mitano ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo.

"Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuning'oa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao," alisema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.

Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi kama mwanasiasa mchanga anayechipukia anapaswa kutambua kuwa hawezi akapata umaarufu kisiasa utakaomfanya aendelee kuaminiwa na wananchi wa Mbeya mjini kwa kwenda kwenye majimbo mengine.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Mwakyembe hii vita ya maneno ni vema ikaishia hapo, au kama wao wameitisha mkutano na wewe nenda kafanye wa kwako kuweka mambo sawa...hilo la kusema Sugu ni mwanasiasa mchanga linatosha hizo persona attacks tena kuwa hata akivaa hereni masikio yote mawili yanaweza yakatrigger mambo mengine, maana bila shaka na wewe sio msafi kwenye oersonal affairs sbb kila binadamu ana "dark side" yake
 
Hii ndege wote walie akilia bundi uchuro...!
Kweli matatizo hayafungwi nepi kama sio stress za maisha nadhani huyu Mwakyembe anasumbuliwa na adult age.
 
Hakika Mwakyembe hafai tena kuwakilisha wana-Kyela.

Huyu alitumia mamilioni ya kodi yetu kwenye kamati yake ya richmond, akaja na maazimio lukuki, lakini yote serikali ikayapuuza na kuyatupilia mbali. Serikali hiyohiyo iliyoponda kazi ya kamati yake ikamhonga uanibu waziri naye akakenua meno. Angekuwa mkweli ndani ya nafsi yake angekataa uteuzi ule uanomfanya awe sehemu ya hii irresponsible govt.

Fisadi sawa na anaowatuhumu ufisadi.
 
Huyo Mbiliyi sio mwanasiasa kwanza ni mwehumwehu tu hana lolote yeye akusanye hizo pesa za pension akipata aendelee na mziki wake.
 
Hii ndege wote walie akilia bundi uchuro...!
Kweli matatizo hayafungwi nepi kama sio stress za maisha nadhani huyu Mwakyembe anasumbuliwa na adult age.
haupo sahihi inamaana tumeshamsahau mwakyembe mda huu,amakweli mfali mbuzi binadamu atakuudhi tu
 
Kumbe Sugu ana vaa heleni sikioni! Mmmmmh hii ni aibu kwa watu wa mbeya mjini! Mbunge ana vaa heleni!
 
Hakika Mwakyembe hafai tena kuwakilisha wana-Kyela.

Huyu alitumia mamilioni ya kodi yetu kwenye kamati yake ya richmond, akaja na maazimio lukuki, lakini yote serikali ikayapuuza na kuyatupilia mbali. Serikali hiyohiyo iliyoponda kazi ya kamati yake ikamhonga uanibu waziri naye akakenua meno. Angekuwa mkweli ndani ya nafsi yake angekataa uteuzi ule uanomfanya awe sehemu ya hii irresponsible govt.

Fisadi sawa na anaowatuhumu ufisadi.

Siasa za bongo zinachekesha! Hii ni sawa na ya Dr Slaa kusema wabunge wanalipwa hela yingi baada ya kuacha ubunge naye anataka alipwe kama Mbunge! Slaa ni Fisadi sawa na anaowatuhumu Ufisadi!
 
Sasa huu mwaka umekua wa kutupiana maneno tuu na matatizo yetu bado yanakuwa sugu, huo mwezi wasita unaelekea baada watu wafikirie ni jinsigani kuboresha badget ijayo ilete maendeleo miezi ijayo. Siye tunapotezeana mda tuu na maisha ya wafisadi khaa...
 
Huyo Mbiliyi sio mwanasiasa kwanza ni mwehumwehu tu hana lolote yeye akusanye hizo pesa za pension akipata aendelee na mziki wake.
Kama siyo mwanasiasa, anaiwakilishaje Mbeya? sasa hivi ndio amegain popularity ndani ya mbeya kuliko hata alivyokuwa anagombea!
 
<p>
Mvaa heleni Sugu anataka kupambana na Mwakyembe(Phd) hopeless kabisa!
</p>
<p>&nbsp;</p>
Mwakyembe kimeo kama weye na mnafiki mkubwa,phd ya kufuga wizi then kapewa alichomlinda shoga yake jk,fisad huyo alitumwa kusema ukwel mengine aliyaficha faida kwa nini?mnafikiwe alisema mkuu mkoa anamzuia kuleta maendeleo kyela,leo je?aache unafiki na atajuta kwa unafikie roho za maskin zalia juu yake.
 
Mr2 aka SUGU aka 2proud ........ mbeya waachane na siasa wakalime viazi,
 
Back
Top Bottom