Dk. Mwakyembe amrushia Sugu kijembe

Dk. Mwakyembe amrushia Sugu kijembe

Hakika Mwakyembe hafai tena kuwakilisha wana-Kyela.

Huyu alitumia mamilioni ya kodi yetu kwenye kamati yake ya richmond, akaja na maazimio lukuki, lakini yote serikali ikayapuuza na kuyatupilia mbali. Serikali hiyohiyo iliyoponda kazi ya kamati yake ikamhonga uanibu waziri naye akakenua meno. Angekuwa mkweli ndani ya nafsi yake angekataa uteuzi ule uanomfanya awe sehemu ya hii irresponsible govt.

Fisadi sawa na anaowatuhumu ufisadi.

Wananchi wa Kyela ndio wanaomjua mwakilishi wanayemtaka, na kwa sasa ni Mwakyembe.

Ukizifanya siasa za Afrika kwa kuzira hautafanikisha lolote zaidi ya kujiua mwenyewe kisiasa na hilo halitamsaidia Mwakyembe wala mwananchi wa kawaida,anachopaswa kufanya ni kuendelee kupigania anachokiamini from within na ameendelea kufanya hivyo so far, ni rahisi sana kufanikisha anachokiamini akiwa ndani kuliko kupiga vuvuzela tu akiwa nje huku sauti yake ikiwa haina impact yoyote kwenye vikao vya maamuzi, amechagua fungu jema..
 
Kama siyo mwanasiasa, anaiwakilishaje Mbeya? sasa hivi ndio amegain popularity ndani ya mbeya kuliko hata alivyokuwa anagombea!

Amegain umaarufu kwa lipi mkuu?
 
PhD= Poor Hair Distribution, sasa watazame wote wenye hizo phd uone nywele zao
 
Phd ya Mwakyembe=uongo+unafiki. Huyu alitumia Phd yake kulaghai watu eti Mkuu wa mkoa anazuia maendeleo! Ni Phd ya Mwakyembe ambayo mwaka jana imegundua kwamba Kyela kuna maembe ya msimu. Phd inatuambia eti Kakao ni kidogo hivyo hatuwez kuwa na kiwanda. Hapa akiulizwa maendeleo aliyoyafanya, atakwambia amejenga daraja<hana hoja nyingine>. Hiyo ndiyo Phd ya Mwakyembe.
 
Mwakyembe kipi bora mvaa hereni au kiongozi alieficha ukweli wa kashfa ya richmon kwa kuogopa kuiumbua serikali!?
Hereni siyo tatizo sana tatizo ni tabia ya mtu mbona wagogo wanava hereni inamaana wajinga!?
 
Malafyale ni mmoja ya watu waliompiga sana vita Mwakalinga aka Mtanzania wa JF kabla ya uchaguzi. Pamoja na kuwaeleza maelezo ya uhakika, ila wao bado walilala mstari mmoja kumtetea Mwakyembe. Wengi walimchagua Mwakyembe kwa sababu kadhaa:

1. Kuwakomoa Mafisadi ambao ilisemekana walikuwa wakitaka kumuondoa na kummaliza kisiasa.

2. Kumkomoa Mwakipesile ambaye ilisemekana kuwa alikuwa akimfanyia fitina Mbunge....

3. Kwa sababu wabunge wengi zamani walikuwa kwa miaka 10 , sasa Mwakyembe na kusoma ile ripoti kwa nini wamuondoe?

4. Wengi waliahidiwa vitu kibao na kuna Kibabu kiliweka sahihi hadi makaratasi kuwa kitapata gari ila sasa imekula kwake na kazi wamekifukuza kiaina. Ushahidi wote ulichomwa moto na hakubaki hata na copy............. Mnyakyusa Mjinga kumbe!!!!!

Sasa ona wanavyosema hawa vijana wake wa Tusk Force wa Jamiiforums kwa sasa:

Ni kweli kabisa kuwa Dr Mwakyembe anakupambana na zomea zomea kila akikatisha baadhi ya mitaa Kyela mjini;na hali ilikuwa tete zaidi juzi stand ya mabasi wakati wakazi wa Kyela walipofunga stand hiyo kwa sababu ya kukithiri kwa uchafu na kuwepo kwa madimbwi yanayotiririsha maji machafu kwenye maeneo yao ya biashara!

Juzi ilikuwa ni mkutano kati ya wananchi,DC,DED na Mbunge lkn wote hao viongozi hawakutokea na kuzidisha hasira za wananchi;walihaidi kuwa sasa mkutano huo utafanyika jana(sina taarifa kama nao ulifanyika au la)!

Wananchi sasa bila kuogopa wanamuhoji Mwakyembe ahadi za serikali hasa kuhusu barabara ya Kyela-Matema beach ambapo Rais JK mwaka 2005 aliwahaidi wana Kyela na kuirudia tena ahadi hiyo mwaka 2010 bila matekelezo yeyote yale;pia wanamkumbusha kuhusu ahadi ya meli mpya waliyowahaidi wana Kyela lkn majibu yake ni negative!

CHADEMA ikiongeza juhudi kidogo tu hasa za kuanza kumtafuta potential candidate wao Kyela basi pasipo shaka yeyote ile wanachukua jimbo hili kiurahisi kabisa;uzuri zaidi ni kuwa Dr Mwakyembe kaisha tangaza kuwa HATAGOMBEA mwaka 2015 hivyo kulifanya jimbo la Kyela"kutokuwa na mwenyewe"!

Mwakyembe ni mtatanishi, si lolote si chochote.

Hebu soma walioshangilia ushindi wa Mwakyembe mwaka jana na leo wanasema nini? Nyambala bado upo? Bado wachekacheka kama mwaka jana? Hahahaaaaa 🙂

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/68676-kyela-elections-2.html
 
Mwakyembe kachemka.
Hivi kwa mtu mwenye uhakika na mambo yake kuna haja ya kujadili kitu unachofikiri ni kidogo. Tena nampa onyo kali mwakyembe, asidhani sie wananchi hatuoni, na kwa taarifa yake mvuto wake umepungua sana baada ya
1. Kuzibwa mdomo kwa kupewa unaibu
2. Kulumbana juu ya dowans na bado akashindwa na pia kutishiwa kufukuzwa uwaziri kama atakua haiungi mkono serikali. amefyata hadi vyombo vya habari havimfuati tena sbb hana jipya la kuongea
3. Kudhalilishwa na uteuzi unaoendelea serikalini hasa kwa wale aliowatuhumu kuwa mafisadi

Tunampa muda tu, umaarufu bongo kuu-maintain kazi. Umechuja na mvuto huna. tutakutana 2015
 
Malafyale ni mmoja ya watu waliompiga sana vita Mwakalinga aka Mtanzania wa JF kabla ya uchaguzi. Pamoja na kuwaeleza maelezo ya uhakika, ila wao bado walilala mstari mmoja kumtetea Mwakyembe. Wengi walimchagua Mwakyembe kwa sababu kadhaa:

1. Kuwakomoa Mafisadi ambao ilisemekana walikuwa wakitaka kumuondoa na kummaliza kisiasa.

2. Kumkomoa Mwakipesile ambaye ilisemekana kuwa alikuwa akimfanyia fitina Mbunge....

3. Kwa sababu wabunge wengi zamani walikuwa kwa miaka 10 , sasa Mwakyembe na kusoma ile ripoti kwa nini wamuondoe?

4. Wengi waliahidiwa vitu kibao na kuna Kibabu kiliweka sahihi hadi makaratasi kuwa kitapata gari ila sasa imekula kwake na kazi wamekifukuza kiaina. Ushahidi wote ulichomwa moto na hakubaki hata na copy............. Mnyakyusa Mjinga kumbe!!!!!

Sasa ona wanavyosema hawa vijana wake wa Tusk Force wa Jamiiforums kwa sasa:

Pole sana mkuu lakini Mwakyembe bado yupo yupo sana...
 
Huyo Mbiliyi sio mwanasiasa kwanza ni mwehumwehu tu hana lolote yeye akusanye hizo pesa za pension akipata aendelee na mziki wake.

wewe na mwakyembe siku zenu zinahesabika hakika Mwakyembe ni Mchafu kama Rostam na Lowassa mimi ninasema kama inakuma sana kamwambie coz Ccm tumewachoka jamani mbona hamuelewi?
 
Siasa za bongo zinachekesha! Hii ni sawa na ya Dr Slaa kusema wabunge wanalipwa hela yingi baada ya kuacha ubunge naye anataka alipwe kama Mbunge! Slaa ni Fisadi sawa na anaowatuhumu Ufisadi!

Hapa ni thread ya Mwakyembe na Sugu, Dr. Slaa kaingiaje humu! Uwezo wako wa kufikiri unawalakini, wewe ni sawa na yule kijana wa kwenye kongamano la kwanza la katiba pale chuo kikuu. Watu wako serious wanazungumzia mchakato wa katiba yeye analeta habari za maharage na sukari. Inawezekana ndo wewe tumeshakuzoea. Post zako zote ni za kifarafara tu!
 
"Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuning'oa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao," alisema Dk. Mwakyembe."

Mmmmmmmh huko Kuchana mistari ndio kufanya vitu gani??? Hizo Personal Attack hazisaidii sana Mh.Mwakyembe..Kwani kama watu wakiamua kukuweka uchi na kuyaanika yale uyafanyayo hapo kwako Cleopatra heshima yako haitatetereka?
 
Kumbe Sugu ana vaa heleni sikioni! Mmmmmh hii ni aibu kwa watu wa mbeya mjini! Mbunge ana vaa heleni!
sonko.jpg



Huyu wa Kenya utasemaje tena yeye kavaa ndani ya bunge.
 
Mhmm hata kama nikivuta bangi mwezi mzima siwezi kufananisha Mwakyembe na Sugu! Hata bangi iwe kali kiasi gani sinto ona kama wanafanana

Mimi naongezea hata kama akivaa hereni sikio zote na akasuka nywele hawezi kumfikia Mwakyembe, mjue kuwa mtu kuwa CDM haitoshi kumpa uwezo stahili, mnaongea ugoro na kupiga chafya.
 
Mwakyembe TEAM mko wapi????

Malafyale, Kasyabone tall, solomon David, Nsesi, Nguvumali, Next Level, Mwafrika, Kanda2, Shalom et el.....

Njooni mje msaidie Mzoga wenu wa Kisiasa huko Kyela.......... Shombo kali hadi ikipita watu wanaizomea......

Nigeria wanaosha Samaki kwa sabuni ya unga ili wampike, labda na nyie mjaribu kumfua Mbunge wenu ili watu wampende......

Yes, KYELA OYEEE!!!!!!!

 
Last edited by a moderator:
Soma maelezo ya Giddy Mangi hapo chini............

Sio mageni haya, tuliyasikia sana haya kabla ya uchaguzi wa 2010, lakini wananchi Wakyela wakafanya tofauti kabisa..

Tofauti na wakati ule, Mwakyembe sasa anaweza akaiagiza halmashauri ya wilaya ya Kyela ifanye kitu na ikatekeleza, na anaweza pia akaiagiza tanroad ifanye kitu na ikatekeleza, tegemea kumuona Mwakyembe wa 2015 mwenye vingi zaidi vya kuwaonyesha wananchi wa Kyela kuliko yule wa 2010, wait and see..

Mwayembe awachimba

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=23967

Dr. Mwakyembe: Barabara za Wilaya ni usanii mtupu. | StarTV Tanzania &#8211; Brightens Your Day
 
sonko.jpg



Huyu wa Kenya utasemaje tena yeye kavaa ndani ya bunge.

Unafananisha watu kwa sura au kwa anachozalisha kwa ajili ya mahitaji ya Jamii?!! Kama unadhani kuvaa hereni si hoja ungemtumia huyo mvaa hereni wako wa Kenya kuainisha aliyofanya baada ya kuwa Mbunge (Alikuwa na manufaha gani, ufanisi gani, mabadiliko gani, nini faidi na uwezo mahususi aliokuwa nao n.k) hii inge weza kuwa kama utetezi wako juu ya Mvaa herini wako wa Mbeya; Hata hivyo bado unaweza kupinga maneno ya Mwakyembe kwa kuthibitisha kuwa huyu wako siyo Mwanasiasa Mchanga bali Jabali kwa ushahidi wa Ujabali wake si kwa kutuonyesha wavaa hereni wengine waliowai kuwa wabunge!!

Mwakyembe hajasema kuwa huyo Jamaa si Mbunge, wala hajasema kuwa hafai kuwa Mbunge kasema mambo ya kisomi kabisa kuwa huyo ni mwanasiasa mchanga na hata akivaa hereni sikio mbili hatoweza kumng'oa kyela! Kama wewe unadhani ni uongo basi mwambie avae hereni sikio mbili tuone kama atamg'owa Mwakyembe Kyela!!
 
Back
Top Bottom