Dk. Malasusa, hali bado tete

Haahaaa hapo umetumia busara kiongozi
Maana kwenye hizi maada ukitelezaa tu utajikutaa umegeuzwa mbuzi wa kafara
Tuhumaa zote zinakugeukiaa

Tena we ndo unageuka source kuu ya habari unaanza kuulizwa, wengine wanakufata PM wanahoji "ilikuajee mkuu tupe mkandaa"[emoji28] [emoji109]
 
Hahahahahaa.....

Poa mkuu. Ahsante kwenye angalizo. Ntalitumia kule kwenye jukwaa la wakubwa ili vibinti vinifuate PM nifanye mchakato wa kuviMalasusa pasi na shaka[emoji106] [emoji106] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Lakini mbona wale wapendwa wa Kaskazini ndo wengi na wanatengenezewa michongo ya kupeana kazi? Ama wa-Pwani wanatumika?
Sasa jiulize, Malasusa ni Mkaskazini?
Mkakati wa kuifanya DMP iwe na sura ya kitaifa badala ya ile ya zamani ya kuwa ya Kizaramo tu, umeratibiwa na Malasusa. Wanampiga vita sana
 
Kubenea ana mzushia huyo malasusa kwa sababu malasusa alimsaliti babu wa kujinyea chato
 
Hivi bado malasusa hajaondolewa?, tumechoka kuwasikia hao michepuko kwenye kanisa
 
Jambo usilolijua ni usiku wa giza, nilifanikiwa kusoma tuhuma hizi kwenye moja ya gazeti na kwa bahati nzuri nimejaribu kufuatilia kidogo ili kujua nini hasa kinatokea katika Dayosisi ya mashariki ya Pwani. Kwa watu ambao hawaijui hii dayosisi ya mashariki na pwani sio rahisi kuelewa haya mambo, wengi watachukulia mambo haya kwa uzito usio stahili.

Kanisa lina maadui kadhaa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisakama Kanisa . Kwa KKKT Dayosisi ya mashariki na Pwani kumekuwa na maadui wengi. Adui mmoja mkubwa ambaye ameitesa Dayosii hii ni Mambo ya Uzawa, muundo wa KKKT unasababisha kila Dayosisi iamini kuwa wanaostahili kuongoza Dayosisi ni watu wazawa wa eneo hilo, Dayosisi zote zilizopo, nyingi huongozwa na wazawa wa eneo hilo, hili ni tatizo kubwa na kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mengine lilivuruga sana kanisa (Dayosisi ya Mashariki na pwani) wakati wa Askofu Jerry Ngwamba, askofu Jerry Ng'wamba alikuwa ni Mzaramo wa Kisarawe ambapo aliiongoza Dayosisi hii akimpokea Askofu Sendoro ambaye alikuwa mpare. Kutokana na kuamini kuwa wazawa ndiyo wenye uhalali wa kuongoza Dayosisi husika kipindi hicho kilishuhudia ubaguzi na upendeleo ulioweza kuwabagua watu walioitwa "wakuja" jambo hili liliibua harakati za hao "wakuja" ambao ni wengi sana katika Dayosisi ya mashariki na pwani na kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaoabudu na kuchangia maendeleo. Watu waliposhindwa kuvumilia pamoja na tuhuma nyingine za wazi zilizoundiwa tume, zilisababisha kuondolewa kwenye Utumishi wa Kanisa Askofu Jerry Ngwamba.

Ninachotaka kuchangia katika huu uzi ni kuwa Dayosisi hii imekuwa na chokochoko nyingi na silaha kubwa ambayo nafikiri imekuwa ikitumika vizuri ili kulivuruga Kanisa ni uzushi kama huu unaofanywa na watu ambao hawakufurahi uwepo wa Utumishi wa Askofu Malasusa kutokana na ukweli kuwa sio mzawa wa Pwani. Kwa wana KKKT waaminifu wanaelewa jambo hili na ndiyo maana hawahangaiki nalo sana, viongozi au wachungaji wale ambao kwa nia moja au nyingine wana maslahi nalo ndiyo wanaohangaika.

Nafikiri ifike sehemu Dayosisi isikae kimya pamoja na kuomba lakini nilazima hatua zichukuliwe ili ukweli wa jambo hili ujulikane, Hatua za kimahakama lazima zichukuliwe ili wale wote wanaotumika kulichafua Kama wana ushahidi wa kweli waueleze na hatua zichukuliwe kwa yeyote atakayekuwa ana nia ovu dhidi ya Kanisa la KKKT.
 
Tusihukumu tusije tukahukumiwa?je sisi tunaonyoosha vidole vyetu ni wasafi kiasi gani? ? ?
Nmepitia msg zoteeee

Lkn hiii imenijaza imaniii

Nmejifunza kua


"A WISE MAN LEARNT MUCH FROM FOOLISH PERSON/STUPID PERSON BUT NEVER A FOOLISH LEARNT ANY THING FROM A WISE MAN"
 
Huenda kuna kitu unajua hebu tuthibitishie kwamba anaandamwa sababu alikwenda kwenye Sherehe zakuapishwa Magufuli......Nitarudi
 
Unajua kuna majitu humu hayajui chanzo cha hizo Kashfa yaokoteza Maneno eti...sababu alimuunga mkono Magufuli...Tatizo DMP imekuwa mahari pamavuno kwa Viongozi walafi....wengi wao wamegeuza Kanisa kama kampuni...ndio sababu ya hayo yote
 
Alwatan acha kashfa na maneno yasio na ukweli mungu atakuhukumu kwa maneno yako.
 
Ukiondoa sababu ya kuhudhuria sherehe (ambayo si inayotajwa na MwanaHalisi), hoja kuhusu tuhuma zake nako ni kuandamwa?
 
Malasusa na apelekwe mahakamani ili haki itendeke, haiwezekani ugoneke na mke wa mtu halafu utumie kujulikana kwako kumuweka ndani, DNA itatoa jibu safi litakalomsafisha ama sivyo tutabaki tukimwamini jamaa
 
Kama hii stori ni ya kweli basi huyu mchungaji noma. Analiwa na kondoo wake afu anamgaia na bosi wake.

Mi ndo maana kwenda kanisani imekuwa ngumu sana. Makanisani kumejaa full unafiki, ufedhuli, uzinzi nk.... tena ukifanywa na viongozi na makasisi.
Ndugu ukienda Kanisani kwa kumfuata MTU utaumia sana Roho...
 
Kuna watu hawajui wanachofata huko maKanisani...ndio maana Ibada ikiendelea yeye anakoroma kwa Usingizi sasa MTU kama huyo kumaliza makanisa hakuna Tatizo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…