Hii nchi ya ajabu sana, kuna jamaa alitaka kufungua mkahawa wa chips ,wakati anaenda kuomba lesseni ya biashara, walitaka kumfanyia hesabu ya thamani ya vitu vilivyomo kwenye mkahawa kama.
Fridge
Majiko ya kupikia
Freezer
Meza na viti pamoja na kodi ya mlango.
Ubora wa mlango wa biashara
Baada ya hapo eti ndio wampigie hesabu kwa mwaka talipa kodi kiasi gani, baada ya kuona hivyo ameamua kuurudisha mlango na kuuza vifaa vyote.
Hivi mtu ndo kwanza anaaza biashara hata hajauza maji wacha chips unampigia mtu hesabu ya kulipa kodi ?
Wenzetu system zao,unapoanza biashara hulipi kodi mwaka mzima kwa wafanya biashara wadogo, baada ya mwaka ndio unapigiwa hesabu ili next year yaani mwaka wa pili ulipe kodi.
Lakin kwanza wanakupigia juu ya matumizi yako binafsi, kama kulipia nyumba yako unayo is hi, kula mavazi, na bills nyengine, pili gharama za uwendeshaji wa biashara yako, tatu faida yako, kama haitoshelezi kukukimu maisha yako, serikali ndio inakupa wewe pesa ili uweze kuishi na biashara yako iwepo kama ni ajira kwako.
Serikali yetu haioni furaha mwananchi wake kujiajiri ili ajikwamue na umasikini, zaidi ya ku kamua.
Nchi ya ajabu hii