Dk. Mahanga: Magufuli anadidimiza uchumi

MAKONGORO Mahanga, amesema sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji katika serikali ya awamu ya tano zina walakini mkubwa na kwamba ndiyo chanzo cha hali mbaya ya kiuchumi hapa nchini ikiwemo kuadimika kwa fedha mikono mwa wananchi.

Dk. Mahanga alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (2005-2015), kabla ya kuhamia Chadema mwaka Agosti mwaka huu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo, Mahanga ambaye ni mtaalamu wa mambo ya fedha na uchumi amesema ukusanyaji wa kodi ni jambo jema, ila lazima lifanywe kwa kujali maslahi ya wawekezaji na wafanyabiashara ambao ndiyo walipa kodi na waajiri.

“Serikali inaangalia zaidi kukusanya mapato yake bila kujali sana mazingira wezeshi ya wafanyabiashara na wawekezaji ambao ndio walipa kodi. Kwa kifupi sera na taratibu za kodi na ukusanyaji wake unaua sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo,” amesema Dk. Mahanga.

Ameongeza kuwa “hata uamuzi wa Serikali kuzuia sekta binafsi kufanya biashara na Serikali ni uamuzi mbaya sana. Utaua sekta binafsi na kupoteza ajira nyingi sana za watanzania kwani Sekta binafsi wanaponyimwa kabisa fursa za kupata kandarasi za serikali, watakosa biashara, sasa kodi ya kutosha watalipaje?”

Dk. Mahanga amesema kwa maoni yake sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji zina walakini mkubwa na maamuzi ya kisiasa yasiyozingatia utashi wa kitaalamu ndiyo umeifikisha nchi katika hali mbaya ya uchumi na mzunguko wa fedha kwa wananchi kuwa mdogo.

Pia ameonya kuwa, maamuzi ya baadhi ya matumizi ya serikali kufanyiwa Ikulu badala ya bungeni ni kuvunja Katiba na misingi ya utawala bora.

“Ununuzi wa ndege ili kufufua shirika la ndege hapa nchini ni mzuri lakini hazikupaswa kununuliwa ndege nyingi mfululizo na bila kufuata vipaumbele vya maendeleo ya nchi,” amesema.
kwanza huyu mahanga hajajibu ile tuhuma ya phd yake kua feki. anaimba ule wimbo wa hela mtaani hakuna kama ndio kuonesha hali ya uchumi mbaya wakati wataalam nchini benki ya dunia na imf wanasema uchumi uko vizuri kabisa. hii yenyewe inaonesha mahanga anaongea lugha moja na watumbuliwa na wapiga dili.
 
Mbona sisi watanzania tunakuwa wanafki kiasi hichi, kwani kuna tofauti gani ya kukusanya kodi Kati ya awamu hii na ile iliopita??? Je 18%haikuepo tangu awali?? Mbona nyie wasomi mnatuchanganya, ni heli mgesema kwasasa watanzania kulingana na uelewa wa kulipa kodi sasa serikali iwapunguzie walipa kodi 8%ili ibaki 10%hapo ntakuelewa,
 
Mtaalam wa mambo ya fedha na uchumi anatakiwa atoe uchambuzi kuhusu sera za kodi na ukusanyaji kodi unavyoua uchumi. Tunaambiwa watu walikuwa hawalipi kodi huko siku za nyuma lakini serikali ya Awamu ya Tano ikaingia na kusimamia ulipaji kodi, leo tena wataalam wanasema ukusanyaji kodi unaua uchumi. Sisi wengine ambao si wataalam wa mambo hayo tunabaki tunashangaa tu tusijue la kusema. Nadhani kama watanzania hatujui tunataka nini: watu wasilipe kodi au walipe kodi. Kama wanaonewa katika kutozwa basi watozaji wawajibike kwa kuonea.

Jiongeze kidogo. Kama kodi ilikua haikusanywi serikali ilikua inajiendesha vipi? Mishahara ilikua inalipw vipi
Mikopo kwa wanafunzi walikua wanapewa vipi mikopo?
Ujenzi wa barabara ulikua unatekelezwa vipi?
Kuajiri na kupandisha vyeo na mishahara kila mwaka walikua wanapandisha vipi?
 
Dr mahanga isijekuwa haya maneno ndo unamsababishia Mr melo kuletewa shida?????
 
Waache kulialia serikali ya JPM haijaweka sheria yoyote mpya ya ukusanyaji kodi, kitu ambacho JPM kafanya ni kuzuia pesa za magendo, sasa wale wote waliokuwa wanategeme pesa a magendo ndio wanalialia kama kasuku, someni number mnafikiri walipa kodi wa nchi hii wapo kuwafanya muishi kama wafalme! Fanyeni kazi. Kaza uzi huo huo JPM.
 
kwanza huyu mahanga hajajibu ile tuhuma ya phd yake kua feki. anaimba ule wimbo wa hela mtaani hakuna kama ndio kuonesha hali ya uchumi mbaya wakati wataalam nchini benki ya dunia na imf wanasema uchumi uko vizuri kabisa. hii yenyewe inaonesha mahanga anaongea lugha moja na watumbuliwa na wapiga dili.
Usihoji PhD za watu mkuu wenye nazo hawapendi zihojiwe. Feki zimejaa huko Lumumba kumbuka vizuri mkuu
 
Tatizo
Mtaalam wa mambo ya fedha na uchumi anatakiwa atoe uchambuzi kuhusu sera za kodi na ukusanyaji kodi unavyoua uchumi. Tunaambiwa watu walikuwa hawalipi kodi huko siku za nyuma lakini serikali ya Awamu ya Tano ikaingia na kusimamia ulipaji kodi, leo tena wataalam wanasema ukusanyaji kodi unaua uchumi. Sisi wengine ambao si wataalam wa mambo hayo tunabaki tunashangaa tu tusijue la kusema. Nadhani kama watanzania hatujui tunataka nini: watu wasilipe kodi au walipe kodi. Kama wanaonewa katika kutozwa basi watozaji wawajibike kwa kuonea.
Tatizo kodi inatakiwa ilipwe ila iwe halisi sisi tunakodi nyingi mno unnecessary na ndio zinawafanya watu wakwepekulipa. We need realistic tax regime sio ya kukamua
 
MAKONGORO Mahanga, amesema sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji katika serikali ya awamu ya tano zina walakini mkubwa na kwamba ndiyo chanzo cha hali mbaya ya kiuchumi hapa nchini ikiwemo kuadimika kwa fedha mikono mwa wananchi.

Dk. Mahanga alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (2005-2015), kabla ya kuhamia Chadema mwaka Agosti mwaka huu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo, Mahanga ambaye ni mtaalamu wa mambo ya fedha na uchumi amesema ukusanyaji wa kodi ni jambo jema, ila lazima lifanywe kwa kujali maslahi ya wawekezaji na wafanyabiashara ambao ndiyo walipa kodi na waajiri.

“Serikali inaangalia zaidi kukusanya mapato yake bila kujali sana mazingira wezeshi ya wafanyabiashara na wawekezaji ambao ndio walipa kodi. Kwa kifupi sera na taratibu za kodi na ukusanyaji wake unaua sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo,” amesema Dk. Mahanga.

Ameongeza kuwa “hata uamuzi wa Serikali kuzuia sekta binafsi kufanya biashara na Serikali ni uamuzi mbaya sana. Utaua sekta binafsi na kupoteza ajira nyingi sana za watanzania kwani Sekta binafsi wanaponyimwa kabisa fursa za kupata kandarasi za serikali, watakosa biashara, sasa kodi ya kutosha watalipaje?”

Dk. Mahanga amesema kwa maoni yake sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji zina walakini mkubwa na maamuzi ya kisiasa yasiyozingatia utashi wa kitaalamu ndiyo umeifikisha nchi katika hali mbaya ya uchumi na mzunguko wa fedha kwa wananchi kuwa mdogo.

Pia ameonya kuwa, maamuzi ya baadhi ya matumizi ya serikali kufanyiwa Ikulu badala ya bungeni ni kuvunja Katiba na misingi ya utawala bora.

“Ununuzi wa ndege ili kufufua shirika la ndege hapa nchini ni mzuri lakini hazikupaswa kununuliwa ndege nyingi mfululizo na bila kufuata vipaumbele vya maendeleo ya nchi,” amesema.
Wapi amese

Wapi amesema ukusanyaji kodi unaua uchumi?

Hayo siyo yangu
 
Jiongeze kidogo. Kama kodi ilikua haikusanywi serikali ilikua inajiendesha vipi? Mishahara ilikua inalipw vipi
Mikopo kwa wanafunzi walikua wanapewa vipi mikopo?
Ujenzi wa barabara ulikua unatekelezwa vipi?
Kuajiri na kupandisha vyeo na mishahara kila mwaka walikua wanapandisha vipi?
Hapo napo unabisha na kesho utasema walikuwa wanakusanya arrears? Mkuu si tuliambiwa kilichokuwa kinakusanywa ni kiduchu watu walikuwa wakipitisha makontina bila ushuru wa forodha au ulikuwa Cape Verde?
 
Mtaalam wa mambo ya fedha na uchumi anatakiwa atoe uchambuzi kuhusu sera za kodi na ukusanyaji kodi unavyoua uchumi. Tunaambiwa watu walikuwa hawalipi kodi huko siku za nyuma lakini serikali ya Awamu ya Tano ikaingia na kusimamia ulipaji kodi, leo tena wataalam wanasema ukusanyaji kodi unaua uchumi. Sisi wengine ambao si wataalam wa mambo hayo tunabaki tunashangaa tu tusijue la kusema. Nadhani kama watanzania hatujui tunataka nini: watu wasilipe kodi au walipe kodi. Kama wanaonewa katika kutozwa basi watozaji wawajibike kwa kuonea.
Mm nadhani uwe muelewa!!
Tatizo siyo kukusanya kodi; bali tatizo ni kodi mpya nyingi zilizo anzishwa.
Napungufu ya budget ya 2016/17 ni kuwa imejikita kukusanya mapato tu bila kujali ni nani analipa hiyo kodi? Na ni kodi ya Ngapi kwake?
Je kodi hiyo ina athari (+ve or-ve) gani ktk uchumi wa nchi?
Hivyo both Monetary + Fiscal Policies should be used to stabilize the economy!!
TATIZO LA RAIS WETU ANA LEVEL YA HOUSEHOLD ECOMOMY KICHWANI MWAKE!!
 
Nimejifunza hapa kitu....ukitaka kuijua Tanzania na watanzania vizuri usiwe kada wa chama chochote cha siasa....wanasiasa ni wanafki sana....maana ukiwa ccm chadema wakifanya kitu hutakaa ukikubali hata kidogo....ukiwa chadema huwez unga mkono kifanywacho na serikali hata siku moja....na huyu mahanga hana jipya zaidi ya kutaka kusikika
 
wanaume wa Dar.kwanini hamjajitokeza kwa wingi leo mahakamani?kumtia moyo tu mmeshndwa?,duh mungu msaidie [HASHTAG]#Maxmello[/HASHTAG]

N.B-soon JF will be closed-panapofuka moshi pana moto!

mtanzania mmoja habadiliki hata aishi na wazungu 500000!!!!!
 
Ukiangalia hii serikali ndani ya moyo wake inaona gere kwa mwananchi wa hali ya chini anapoanza ujasiriamali . Itambabaisha weee mara leseni, mara kodi, mara kodi ya bango mara hiki mara kile, ilimradi ukate tamaa uwe omba omba na mzururaji hapo ndo wanapata amani mioyoni mwao
 
Hii nchi ya ajabu sana, kuna jamaa alitaka kufungua mkahawa wa chips ,wakati anaenda kuomba lesseni ya biashara, walitaka kumfanyia hesabu ya thamani ya vitu vilivyomo kwenye mkahawa kama.

Fridge
Majiko ya kupikia
Freezer
Meza na viti pamoja na kodi ya mlango.
Ubora wa mlango wa biashara

Baada ya hapo eti ndio wampigie hesabu kwa mwaka talipa kodi kiasi gani, baada ya kuona hivyo ameamua kuurudisha mlango na kuuza vifaa vyote.

Hivi mtu ndo kwanza anaaza biashara hata hajauza maji wacha chips unampigia mtu hesabu ya kulipa kodi ?

Wenzetu system zao,unapoanza biashara hulipi kodi mwaka mzima kwa wafanya biashara wadogo, baada ya mwaka ndio unapigiwa hesabu ili next year yaani mwaka wa pili ulipe kodi.

Lakin kwanza wanakupigia juu ya matumizi yako binafsi, kama kulipia nyumba yako unayo is hi, kula mavazi, na bills nyengine, pili gharama za uwendeshaji wa biashara yako, tatu faida yako, kama haitoshelezi kukukimu maisha yako, serikali ndio inakupa wewe pesa ili uweze kuishi na biashara yako iwepo kama ni ajira kwako.

Serikali yetu haioni furaha mwananchi wake kujiajiri ili ajikwamue na umasikini, zaidi ya ku kamua.

Nchi ya ajabu hii
Kama vile unadanganya.....utaratibu wa kulipa kodi na kupata leseni ni tofauti na ulicho kiandka...kaulize kwanza ili upewe darasa...
 
Tena Mimi nikimsikia mtu aliekuwa ccm tena kwenye serikali ya awamu ya nne, anamkosoa Magufuli huwa natamani kutapika!
 
MAKONGORO Mahanga, amesema sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji katika serikali ya awamu ya tano zina walakini mkubwa na kwamba ndiyo chanzo cha hali mbaya ya kiuchumi hapa nchini ikiwemo kuadimika kwa fedha mikono mwa wananchi.

Dk. Mahanga alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (2005-2015), kabla ya kuhamia Chadema mwaka Agosti mwaka huu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo, Mahanga ambaye ni mtaalamu wa mambo ya fedha na uchumi amesema ukusanyaji wa kodi ni jambo jema, ila lazima lifanywe kwa kujali maslahi ya wawekezaji na wafanyabiashara ambao ndiyo walipa kodi na waajiri.

“Serikali inaangalia zaidi kukusanya mapato yake bila kujali sana mazingira wezeshi ya wafanyabiashara na wawekezaji ambao ndio walipa kodi. Kwa kifupi sera na taratibu za kodi na ukusanyaji wake unaua sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo,” amesema Dk. Mahanga.

Ameongeza kuwa “hata uamuzi wa Serikali kuzuia sekta binafsi kufanya biashara na Serikali ni uamuzi mbaya sana. Utaua sekta binafsi na kupoteza ajira nyingi sana za watanzania kwani Sekta binafsi wanaponyimwa kabisa fursa za kupata kandarasi za serikali, watakosa biashara, sasa kodi ya kutosha watalipaje?”

Dk. Mahanga amesema kwa maoni yake sera ya kodi, fedha, uchumi na uwekezaji zina walakini mkubwa na maamuzi ya kisiasa yasiyozingatia utashi wa kitaalamu ndiyo umeifikisha nchi katika hali mbaya ya uchumi na mzunguko wa fedha kwa wananchi kuwa mdogo.

Pia ameonya kuwa, maamuzi ya baadhi ya matumizi ya serikali kufanyiwa Ikulu badala ya bungeni ni kuvunja Katiba na misingi ya utawala bora.

“Ununuzi wa ndege ili kufufua shirika la ndege hapa nchini ni mzuri lakini hazikupaswa kununuliwa ndege nyingi mfululizo na bila kufuata vipaumbele vya maendeleo ya nchi,” amesema.
Ni Tanzania tu utakuta wanasiasa kama Mahanga wanataka serikali isikusanye kodi au wanalalmika mfumo wa ukusanyaji kodi.
Neymar JR na Messi wameshapata misukosuko ya kukwepa kodi,ingekuwa wapo Tanzania Makongoro angesema serikali inanyanyasa wachezaji wa kigeni hivyo itawakimbiza timu zetu zitakosa ubingwa.
Muwekezaji makini akiamua kuwekeza sehemu,anazingatia kodi na sheria zingine,sioni wawekezaji makini wakikimbia kisa serikali imekaza kamba katika ukusanyaji kodi.
Hawa wakina makongoro ni watu hatari sana, ndio waliotufikisha hapa,bila ya aibu anaitaka serikali ilegeze kamba kukusanya kodi wawekezaji watakimbia!
 
Hakuna viwanda.....Akina Ben Saanane na Maxence Mello ndo Viwanda vyao

Hakuna haja ya kununua ndege nyingi kwa Cash wakati wanafunzi wamekosa mikopo, Maji ni adimu sana kama Morogoro/Dodoma (maeneo ya kura nyingi za CCM) na watu wanakunywa maji machafu kwenye dimbwi

---
Watanzania tunakosa umoja, kila kundi linakaa kulalamika lenyewe. Hata kutokea mahakamani kwa wingi leo tumeshindwa... Leo ilitakiwa iwe mafuriko ya watu mahakamani na hadi Sizonje apelekewe habari.

Nafikiri ni Kweli Mwenge ni uchawi na watanzania tumekuwa mazuzu.....it is Satan...
Viongozi wa dini wafanye maombi

Kuna masuala mengi yamepita kwa urahisi na ni ya kidhalimu.

-Mswada wa habari
-Mikopo ya wanafunzi
-FAO La Kujitoa
-Sheria ya mtandao
-Jamii forum Director (tumeshindwa kwenda mahakamani kwa wingi)
Maombi yepi wakati viongozi wetu wako ndani kwa case za uwongo za ugaidi, miaka miwili hakuna ushahidi wala hukumu
 
Back
Top Bottom