Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Rais wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee John Chigweyemisi Malecela hakutaka kumung'unya maneno kabisa badala yake ameweka bayana msimamo wake akisema kinachofanywa sasa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni utekekezaji wa misingi ya Azimio la Arusha.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na kushika Wizara kadhaa toka Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne sauti yake huwa nzito pale anapoamua kuunguruma.
Amesema Serikali ya Rais Dk John Magufuli inapigania usawa, haki na maslahi ya umma na kutaka rasilimali za nchi ziwanufaishe Wananchi huo ni ni utekekezaji wa matakwa ya sera za Azimio la Arusha .
Mzee Malecela akasisitiza kuwa malengo na shabaha kuu ya kuasisiwa Azimio la Arusha tarehe Februari 5, 1967 ilikuwa ni kusimamia misingi ya usawa wa watu , mlingano wa vipato, maadili , miiko ya uongozi , kukata mirija ya unyonyaji na kuhimiza uzalendo.
Mzee huyo hakutamka matamshi hayo barabarani au kwenye kijiwe cha kahawa, ameyasema hayo mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka aliyemtembelea ili kumjulia hali nyumbani kwake huko kilimani Dodoma
Ameitaja misingi iliowekwa kwenye Azimio hilo lazima iheshimiwe kwa kiwango kile kile kwani ndiyo moyo unaoliendelesha Taifa letu na kulipa heshima mbele ya mataifa mengine.
Mzee Malecela akaeleza ni upuuzi wa mwisho kwa kiongozi au mwanasiasa yeyote kuponda siasa ya Ujamaa na Kujitegenea au kulibeza Azimio ambalo liliweka misingi ya usawa wa watu, ulinzi wa rasilimali na haki ya kila raia.
Limeweka dira ya utawala na uendeshaji mzima wa masuala muhimu katika medani za kisiasa na kiserikali huku likiwataka viongozi, Wafanyakazi , Watumishi wa umma na Wananchi kuishi kwa nidhamu, umoja na upendo .
Mzee Malecela aliyewahi kupachikwa la "greda" akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara akasema kuwepo tofauti kubwa ya kiuchumi na vipato vya Watu kwa kiwango kikubwa, huweza kuzua tafran, misuguano, kuzusha mivutano na Watu kutazamana kwa chuki na uhasama .
Akizungunza bila kumtaja mtu au Wizara yoyote ya Serikali akasema uzalendo, kuheshimu miiko na kuishi kwa kufuata utaratibu na maadili ni mambo yanayojitajika mahali popote pale kwa viongozi wa Serikali, Wanasiasa na kila Mwananchi.
Mwanasiasa huyo aliyepata kuwa mkuu wa mkoa kwenye mikoa kadhaa nchini anaeleza bila kuheshimu miiko na maadili au kutofuata utaratibu na mtu au kiongozi kukosa uchungu na uzalendo mambo yanaweza kuendeshwa hovyo bila usahihi.
Ni wazi na dhahiri matamshi haya ya Waziri Mkuu Mstaafu na mwanasiasa mwenye maono na mtazamo mpana, yanampa uhalali Rais Dk. Magufuli kuendelea na mpango mkakati wake lakini pia yakiwataka mawaziri, Wakuu wa Mikao na Wilaya kujitambua kama wenye dhamana na wajibu wa pamoja.
Hata hivyo ukitazama katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatamka bayana kuwa nchi yetu itaendelea kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea chini ya misingi ya Azimio la Arusha .
Kwa kuyatathmini matamshi ya Mzee Malecela amewakumbusha watendaji dhamana wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Wakuu wa Mikao, Makatibu tawala wa mikoa, Wakuu wa wilaya na Makatibu tawala wa wilaya pamoja na Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, kutokujisahau katika kumsaidia Rais .
Wakati huu ambao azma kuu ya Serikali ya awamu ya tano ikiwa ni kujenga viwanda kuelekea maendeleo ya uchumi wa kati, kauli hii nzito ya Mzee Malecela lazima ichukuliwe kwa umuhimu wa kipekee.
Kadhalika ina mhakikishia Rais kuwa anayoyafanya si yake peke yake, ni malengo ya kisera ya nchi vile vile ni utekelezaji wa sera za msingi katika kulinda rasilimali za nchi, Maliasili , kupinga vitendo vya rushwa , ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi.
Aidha Mzee Malecela akayataja mafanikio ya vyama vya TANU na ASP yalitokana na nguvu za makundi Vijana pamoja na Wanawake ambao walifanyakazi kwa bidii kuelekea uhuru na baada ya kujitawala.
Akasema jumuiya mbili za UVCCM na UWT zimekuwa zikifanya kazi kubwa ambayo imerithiwa toka jumuiya za TANU Youth League , ASP Youth League na UWT.
Kiongozi huyo mkongwe nchini anaitaka UVCCM na UWT kuwa wadau wakuu na watetezi wa chama tawala, , wakosoaji kwa kutumia nguvu ya hoja lakini pia ndiyo majeshi ya chama na uhai wake.
Akaeleza kazi ya UVCCM pamoja na kushiriki siasa wana kazi ya kutafuta habari mbaya zinazolenga kuichafua Serikali, kuwakabili maadui wa nje na ndani kwani jeshi hilo lazima lifanye kazi ya kusaka ushindi nyakati za uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar.
Dk Magufuli kaza buti wazee wako nawe bega kwa bega. Songambele, kanyaga twende, mbele kwa mbele usikubali kusikiliza mayowe watu wanaokutaka ugeuke nyuma na kuwa jiwe.
No Way Back, Aluta Continua ....
Sent using Jamii Forums mobile app