Dk. Magufuli umemsikia mzee Malecela?

Dk. Magufuli umemsikia mzee Malecela?

Hizo ni fix za mchana za mzee wa kigogo.
Azimio la Arusha haliko hivi, ni uongo wa kumpaka mafuta Magufuli kwa mgongo wa chupa.

Mambo muhimu yaliyokuwepo kwenye azimio la Arusha.
1/Serikali kutaifisha mali, makampuni na taasisi binafsi ili ziendeshwe na serikali tu.
2/Kiongozi wa umma kutoruhusiwa kumiliki mali nyingi, kufanya biashara au kuwa na kazi zaidi ya moja.
3/Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa.
4/Kumiliki mali kwa pamoja.
5/Kuupiga vita uwekezaji na ubepari.

Sasa labda Mzee Malecella atuambie tu, kipi hapo Magufuli ametekeleza?
Hajui huyo anayemsifia ana mijengo ya maana kule Dom akiipangisha Taasisi za serikali
 
Hizo ni fix za mchana za mzee wa kigogo.
Azimio la Arusha haliko hivi, ni uongo wa kumpaka mafuta Magufuli kwa mgongo wa chupa.

Mambo muhimu yaliyokuwepo kwenye azimio la Arusha.
1/Serikali kutaifisha mali, makampuni na taasisi binafsi ili ziendeshwe na serikali tu.
2/Kiongozi wa umma kutoruhusiwa kumiliki mali nyingi, kufanya biashara au kuwa na kazi zaidi ya moja.
3/Kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa.
4/Kumiliki mali kwa pamoja.
5/Kuupiga vita uwekezaji na ubepari.

Sasa labda Mzee Malecella atuambie tu, kipi hapo Magufuli ametekeleza?
Huyo Mzee akafie mbali huko, siyo yeye na Mwinyi wake walienda wakakaa Zanziba na kuleta Azimio la Zanziba akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Ndiye aliyekuwa mshauri mkuu wa Mwinyi; hadi Mwalimu akamwandikia Kitabu na kumpa laana iliyomkaa hadi leo; halafu anajifanya mshauri, "anawashwa washwa" huyu au hajayasikia maneno ya anayejipendekeza kwake!!!
 
..
paulo hakuanzisha ukristo, ukristo ulianzishwa na wapagani huko antiocia..matend 11;26...
Biblia imezungumzia ukristo mara3 tu..
jina halisi la wafuasi wa YESU ni watoto wa Mungu. yohana 1;12..ambao hao ni watakatifu waliopo duniani.
so wafuasi wa Yesu jina wanaloitwa ni watoto wa Mungu,watakatifu au wanafunzi wa YESU na si wakristo....ndamaana wakristo anaruhusu ushoga,kulewa n.k
ila watoto wa Mungu, watakatifu hawaruhusu hayo mambooo....
na si kila mtu ni mtoto wa Mungu,no
bai kila mtu ni mtu wa Mungu.
yohana 1;12-wale waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa MUNGU..yaani waliompokea Yesu tu..rumi 10;9
Huna hata aibu kufichua ujinga wako [emoji12] njoo kule jukwaa la Imani/deen ili upate ilimu ghaibu [emoji4]
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Rais wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee John Chigweyemisi Malecela hakutaka kumung'unya maneno kabisa badala yake ameweka bayana msimamo wake akisema kinachofanywa sasa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni utekekezaji wa misingi ya Azimio la Arusha.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na kushika Wizara kadhaa toka Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne sauti yake huwa nzito pale anapoamua kuunguruma.

Amesema Serikali ya Rais Dk John Magufuli inapigania usawa, haki na maslahi ya umma na kutaka rasilimali za nchi ziwanufaishe Wananchi huo ni ni utekekezaji wa matakwa ya sera za Azimio la Arusha .

Mzee Malecela akasisitiza kuwa malengo na shabaha kuu ya kuasisiwa Azimio la Arusha tarehe Februari 5, 1967 ilikuwa ni kusimamia misingi ya usawa wa watu , mlingano wa vipato, maadili , miiko ya uongozi , kukata mirija ya unyonyaji na kuhimiza uzalendo.

Mzee huyo hakutamka matamshi hayo barabarani au kwenye kijiwe cha kahawa, ameyasema hayo mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka aliyemtembelea ili kumjulia hali nyumbani kwake huko kilimani Dodoma

Ameitaja misingi iliowekwa kwenye Azimio hilo lazima iheshimiwe kwa kiwango kile kile kwani ndiyo moyo unaoliendelesha Taifa letu na kulipa heshima mbele ya mataifa mengine.

Mzee Malecela akaeleza ni upuuzi wa mwisho kwa kiongozi au mwanasiasa yeyote kuponda siasa ya Ujamaa na Kujitegenea au kulibeza Azimio ambalo liliweka misingi ya usawa wa watu, ulinzi wa rasilimali na haki ya kila raia.

Limeweka dira ya utawala na uendeshaji mzima wa masuala muhimu katika medani za kisiasa na kiserikali huku likiwataka viongozi, Wafanyakazi , Watumishi wa umma na Wananchi kuishi kwa nidhamu, umoja na upendo .

Mzee Malecela aliyewahi kupachikwa la "greda" akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara akasema kuwepo tofauti kubwa ya kiuchumi na vipato vya Watu kwa kiwango kikubwa, huweza kuzua tafran, misuguano, kuzusha mivutano na Watu kutazamana kwa chuki na uhasama .

Akizungunza bila kumtaja mtu au Wizara yoyote ya Serikali akasema uzalendo, kuheshimu miiko na kuishi kwa kufuata utaratibu na maadili ni mambo yanayojitajika mahali popote pale kwa viongozi wa Serikali, Wanasiasa na kila Mwananchi.

Mwanasiasa huyo aliyepata kuwa mkuu wa mkoa kwenye mikoa kadhaa nchini anaeleza bila kuheshimu miiko na maadili au kutofuata utaratibu na mtu au kiongozi kukosa uchungu na uzalendo mambo yanaweza kuendeshwa hovyo bila usahihi.

Ni wazi na dhahiri matamshi haya ya Waziri Mkuu Mstaafu na mwanasiasa mwenye maono na mtazamo mpana, yanampa uhalali Rais Dk. Magufuli kuendelea na mpango mkakati wake lakini pia yakiwataka mawaziri, Wakuu wa Mikao na Wilaya kujitambua kama wenye dhamana na wajibu wa pamoja.

Hata hivyo ukitazama katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatamka bayana kuwa nchi yetu itaendelea kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea chini ya misingi ya Azimio la Arusha .

Kwa kuyatathmini matamshi ya Mzee Malecela amewakumbusha watendaji dhamana wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Wakuu wa Mikao, Makatibu tawala wa mikoa, Wakuu wa wilaya na Makatibu tawala wa wilaya pamoja na Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, kutokujisahau katika kumsaidia Rais .

Wakati huu ambao azma kuu ya Serikali ya awamu ya tano ikiwa ni kujenga viwanda kuelekea maendeleo ya uchumi wa kati, kauli hii nzito ya Mzee Malecela lazima ichukuliwe kwa umuhimu wa kipekee.

Kadhalika ina mhakikishia Rais kuwa anayoyafanya si yake peke yake, ni malengo ya kisera ya nchi vile vile ni utekelezaji wa sera za msingi katika kulinda rasilimali za nchi, Maliasili , kupinga vitendo vya rushwa , ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi.

Aidha Mzee Malecela akayataja mafanikio ya vyama vya TANU na ASP yalitokana na nguvu za makundi Vijana pamoja na Wanawake ambao walifanyakazi kwa bidii kuelekea uhuru na baada ya kujitawala.

Akasema jumuiya mbili za UVCCM na UWT zimekuwa zikifanya kazi kubwa ambayo imerithiwa toka jumuiya za TANU Youth League , ASP Youth League na UWT.

Kiongozi huyo mkongwe nchini anaitaka UVCCM na UWT kuwa wadau wakuu na watetezi wa chama tawala, , wakosoaji kwa kutumia nguvu ya hoja lakini pia ndiyo majeshi ya chama na uhai wake.

Akaeleza kazi ya UVCCM pamoja na kushiriki siasa wana kazi ya kutafuta habari mbaya zinazolenga kuichafua Serikali, kuwakabili maadui wa nje na ndani kwani jeshi hilo lazima lifanye kazi ya kusaka ushindi nyakati za uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar.

Dk Magufuli kaza buti wazee wako nawe bega kwa bega. Songambele, kanyaga twende, mbele kwa mbele usikubali kusikiliza mayowe watu wanaokutaka ugeuke nyuma na kuwa jiwe.

No Way Back, Aluta Continua ....

Sent using Jamii Forums mobile app
grader? yeye ndiye ajiita tingatinga na siyo huyu. huyu labda awe tingatinga jr
 
Wakati wakiongea kuhusu Ujamaa nankujitegemea wakiweka kibwagizo cha Azimio la Arusha wao ndiyo wamezidi kujilimbikizia Mali,wizi,ufisadi ,rushwa,utesaji,Utekaji,na Mauaji hahahahahajja hata kwa dawa hili ni Azimio la Chattle la Visasi na Chuki wakwende zao
 
Mhmh kutumia mbinu za mwaka 1967 kuleta maendeleo 2017 tena kwa azimio ambalo liliongeza umaskini miongoni mwa watanzania si sawa.
Kwa masikio yangu nilimsikia Mwalimu Nyerere akisema katika Utawala wake hakuna kitu "Crazy" alifanya kama Azimio la Arusha! Leo hii Mzee huyu aliyewahi kuwaambia Watanzania waende Jehanamu! Kisa kudai kuna ma tatizo ya Usafiri nchi hii mnamfagilia. Huyo Mzee hata Mwalimu alimwandikia kitabu cha kumsuta matendo yake. Mnaoshabikia Ujamaa na Azimio la Arusha ni "Millennials" hamjui historia ya Tanzania mnasoma tu kwenye Wikipedia! Waulizeni walioishi enzi hiyo todate:.
 
Nyerere kasema Ujamaa na Ukristo vimeshindwa

Rejea habari zilzochapishwa katika gazeti la Msemakweli toleo nambari 013 la Jumapili Juni 7-13, 1998 yenye kichwa cha habari,"Nyerere adai Ujamaa na Ukristo vimeshindwa" likinukuu mahojiano yaliyofanyika katika kipindi cha maswali na majibu katika television ya CNN.

Nyerere alisema, "Ujamaa umeshindwa kama vile Ukristo ulivyoshindwa.

Ukristo ulianza yapata miaka 2000 iliyopita na kila Jumapili niendapo Kanisani nakuta watu bado wanahubiri.

Na kwa kweli sina hakika kama kuna nchi hata moja tunayoweza kuiita taifa la Kikristo."

Katika toleo hilo mwandishi wa Msemakweli akiripoti maoni ya Wakristo mbalimbali juu ya madai ya Nyerere.Wakristo wengi, wakiwemo Maprofesa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo,walijitahidi sana kuutetea Ukristo kuwa haujashindwa bali Ujamaa ndio ulioshindwa peke yake.

Moja ya sababu zilizotolewa ni kuwa Ujamaa umeshindwa kwa vile umetokana na mawazo ya mtu (Nyerere), wakati ukristo haujashindwa kwa sababu haukuanzishwa na mtu bali na Yesu (ambaye Wakristo wengi hudai ni Mungu aliye hai).

Nyerere anaitwa baba wa Taifa na ni mtu wa kimataifa na hivyo maneno yake yanakuwa na uzito wa aina yake katika jamii. Sidhani kama Nyerere alitoa madai haya kwa mzaha tu.

Nyerere ni muasisi wa ujamaa wa Tanzania na amebahatika kushuhudia ukisambaratika mbele ya macho yake, pamoja na juhudi zake za kuhakikisha ujamaa unadumu. Vile vileNyerere ameshuhudia waasisi wa mfumo huu duniani Urusi au Soviet Union ya zamani ikisambaratika bila hata risasi moja kufyatuliwa.

Sina sababu yoyote ya kutilia mashaka matamshi ya Nyerere ambaye, pamoja na kuwa ni muumini mzuri sana wa kanisa Katoliki, vile vile ametoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Ukristo hapa Tanzania.

Naamini ametoa matamshi hayo kwa kutumia uzoefu wake wa kitaifa na wa kimataifa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa. Kutokana na uzoefu huu Nyerere yuko katika nafasi nzuri sana ya kuchambua na kuongelea masuala haya.

Imeleweka wazi kuwa Ujamaa ni mfumo wa maisha ambao uliasisiwa na kina Karl Marx na Lenin, hawa ni binaadamu kama mimi na wewe.

Je, Ni kweli kuwa Ukristo (Christianity) ulianzishwa na Yesu, Mungu aliye hai? Biblia inatueleza kuwa Ukristo kwa mara ya kwanza ulianza pale Antiokia ambayo iko katika bara la Ulaya (soma Matendo ya mitume 11:26) miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa amekwisha kamilisha kazi aliyotumwa na Baba yake hapa duniani.

Ikumbukwe hapa kuwa Yesu hakuwahi kufika Antiokia katika maisha yake yote ya hapa duniani. Na aliwakataza kabisa wanafunzi wake kupeleka mafundisho yake nje ya Israel (soma Mathayo: 10:5-6).

Hakuna hata sehemu moja katika Biblia tunapofahamishwa kuwa Yesu alileta mfumo mpya wa maisha hususan Ukristo. Yesu mwenyewe anatufahamisha kuwa hakuja kutangua mfumo alioukuta uliokuwepo toka wakati wa nabii Musa (ambao sio Ukristo), bali kuutimiliza (Mathayo: 5:17-20). Na kwa Wayahudi peke yao, na wala sio kwa Wazungu au Waafrika au Wahindi au makabila mengine (Gentiles) ya ulimwengu huu (Mathayo 14:21-28).

Ukristo umeasisiwa na Sauli ambaye ndie Paulo. Katika mazingira ya kutatanisha bila ya kuwepo ushahidi wa kuaminika, Paulo alidai kupewa Utume na Yesu mwenyewe katika Njozi.

Kwa ajili ya majadiliano haya naomba tukubali kuwa Paulo alikuwa Mtume. Lakini bado hii haimpi hadhi ya Uungu, bado anabaki kuwa binaadamu kama wengine.

Katika nukta hii tukumbuke kuwa Paulo hakuwahi kukutana na Yesu katika uhai wake. Na ni vema vile vile tukakumbuka kuwa huyu ndio yule Paulo aliyekuwa mstari wa mbele katika kuwatafuta na kuwaua wanafunzi wa Yesu.

Vile vile tisisahau kuwa huyu ndie Paulo aliyekufa kwa kukatwa kichwa karibu na Roma kati ya mwaka 61B.K. na 68 B.K. Bibilia haituelezi kuwa Paulo baada ya kufa alifufuka na hivyo kuushinda umauti kama inavyodaiwa kwa Yesu, hivyo kupata hadhi ya uungu.
Mkuu una Kitu kizuri kwanini usianzishe thread ya haya mambo kwa mapana
 
hivi hakuwa miongoni mwa viongozi wa ccm waliokutana zanzibar na kuamua walivyoamua? leo tena kasema hivi? akumbuke msemakweli ni mpenzi wa Mungu, unafiki utamsaidia leo lakini jioni nayo imekaribia muda umeenda sana.
 
Back
Top Bottom