Dk. Magufuli ajitosa Katiba mpya, awabeza CHADEMA | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Magufuli ajitosa Katiba mpya, awabeza CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mdau wetu, Dec 18, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema lazima Katiba mpya izingatie matakwa ya wananchi ili kuliweka taifa katika hali ya utulivu.

  Amewataka Watanzania kutoiga vurugu zilizotokea kwenye nchi za Libya, Sirya, Tunisia na Misri badala yake waendelee kuwa wavumilivu huku akiwaomba kutotumia maandamano kama suluhu za matatizo ya kiuchumi yanayolikumba taifa na watu wake kwa sasa.

  Dk. Magufuli alisema hayo juzi alipohutubia maelfu ya wananchi wakati wa uzinduzi wa Kivuko cha mv Kome II, uliofanyika kwenye Kata ya Nyakarilo, Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema, Mwanza.

  Kivuko hicho kimejengwa na kampuni kutoka Uholanzi na kimegharimu zaidi ya sh bilioni 1.6 katika matengenezo yake ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa visiwa vya Ntama, Kome, Lugata na Nyakarilo.

  Waziri huyo aliitaka tume maalumu ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba mpya itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete itekeleze jukumu hilo bila kuchakachua maoni ya wananchi.

  "Hili la Katiba mpya ni jambo mhimu na nyeti…tunataka Katiba ijayo ikidhi matakwa ya Watanzania. Tume itakayoundwa na rais kukusanya maoni ifanye hivyo bila konakona fulani fulani," alisema Dk. Magufuli.

  Waziri huyo pia aliwabeza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Kikwete kuhusu Katiba mpya na kusema taratibu zote zilifuatwa na muswada ulipelekwa na kupitishwa bungeni licha ya wengine kutoka nje.

  "Mwanzoni wabunge hao hao walisema hawamtambui rais, lakini sasa wamekuwa wa kwanza kukimbilia Ikulu kuzungumza na rais wasiyemtambua…kuona hivyo rais kawapa chai, juisi na soda wakanywa, kesho yake akasaini muswada wa kupata tume ya Katiba mpya," alisema Dk. Magufuli.

  Kuhusu kivuko hicho, alimwagiza Wakala wa Serikali wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kuhakikisha wanawafukuza kazi watumishi wazembe na wasiojali kazi zao na kwamba vivuko vyote lazima vifanyiwe matengenezo ya mara kwa mara.

  Katika hatua nyingine alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Leonard Kadashi, kuhakikisha mkandarasi anayejenga barabara ya kutoka Sengerema kwenda Nyakarilo anakamilisha mradi huo ndani ya muda vinginevyo afukuzwe kazi.

  "Wakati nakuja huku nimekuta mkandarasi ndiyo anatengeneza barabara hii. Na nimeambiwa walianza usiku baada ya kusikia nakuja. Nataka mchezo huu ufe mara moja na barabara hii ikamilike ndani ya muda unaotakiwa.

  "Nakuagiza wewe wakala wa barabara mkoa ukimuona huyu mkandarasi analeta uzembe mfukuze kazi maana hadi sasa tulishafukuza makandarasi kama hawa 2,800, sitaki lelemama katika kazi," alisisitiza Dk. Magufuli.
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #41
  Jun 3, 2018
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 34,413
  Likes Received: 42,426
  Trophy Points: 280
  Haya sasa kaburi limefukuliwa
   
 3. Yamakagashi

  Yamakagashi JF-Expert Member

  #42
  Jun 3, 2018
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 5,416
  Likes Received: 9,265
  Trophy Points: 280
  Dah sasa hivi kamuulize kama yeye ndiye aliyesema kwamba swala la katiba mpya ni la muhimu na nyeti na tume isichakachue maoni ya wananchi

  Walahi tutakuokota Mabwepande au chuma kitakuhusu
  Long live Jf
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #43
  Jun 3, 2018
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,299
  Likes Received: 2,622
  Trophy Points: 280
  Bado
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #44
  Jun 3, 2018
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 27,433
  Likes Received: 5,733
  Trophy Points: 280
  Kumbe mambo ya Libya na Kuwait aliyasema zamani sana kina sadamu wa libya na gadafi wa kuwait hahaaaaa.
   
 6. titimunda

  titimunda JF-Expert Member

  #45
  Jun 3, 2018
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 5,586
  Likes Received: 6,105
  Trophy Points: 280
  Enzi hizo kabla hujasajiliwa lumumba fc
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...