Dk. Kilahama aibiwa, aomba msaada JF

kuna walakini hapa huenda kuna nyaraka muhimu sana kwenye hizo vifaa vyake so wenye shida na hizo documents wame amua kuzichukua wakazifanyie kazi....nchi ngumu sna hii....
 
Wewe endelea kuchapa usingizi tu yaani mtu mkurugenzi mstaafu wa wizara ya misitu maliasili na utalii unamchukulia simple kama mama ntilie mstaafu.

we bwana we unakua kama hujui wastaafu wa nchi yetu wanavyoishi kwa shida? watu walikua mawaziri lakini hata pa kulala hawana wacha mchezo.
 
Aliifanyia nn nchi hii kipindi cha uongozi wake? Isije kuwa wananchi wamerudisha mali alizowaibia
 
Mmm,
Pole zao;
Watakuwa hao vijana waliwasoma wakajua kuwa
mawazo yao yapo mbali na mabegi yao wakaamua
kujisevia;
 
daah!wezi sio kabisa yani acheni wauliwe wakikamatwa
 
Pole kwanza.Sasa wewe kwa akili yako mtu gani akuibie alafu aje kurudisha?
 
mlete doctor kwenye tv ya asili awaone wezi wake na watarudisha wenyewe.

au subili albadili ya mama wema sepetu ikianza kufanya wale masheikh wakabidhiwe jukumu la pili.

tatu si vibaya mdau mkitangaza hata reward kwa atakayefanisha kupatikana vitu hivyo.

simu zake kama ni za kisasa anzeni na kitengo cha it kwenye hiyo mitandao mzitrack.
 
na kama pale mlandizi watazipata tu, ni eneo dogo, labda wakauzie bagamoyo, na kama alikuwa kwenye basi uwa wanasema chunga laptop yako na mizigo yako ya ndani, na je wakati wanashuka taa hazikuwahswa kwenye gari?

pole kwa wote hao walioibiwa, hawa wezi wanarudisha watu nyuma sana, ndio maana jana vijana wawili wezi walipigwa sana 77 mule ndani, eti unategemea utakimbilia wapi, hawa wezi waliothibiitishwa ni wezi wapigwe tu.
 
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?

unashangaa nin sasa kwani kupanda gari la abiria ni ajabu? kwani yeye siyo abiria .kwel ndio maana hii nchi hatuendelea na hatutaendelea kama tutakuwa na kizazi kama chenu.wakati nchi zilizoendelea watu kama professa wanapanda baskeli.
 
pole sana Dk Kilahama. Dk Kilahama ni mtu ambaye alikuwa muadilifu sana kwenye utumishi wa umma.
Mungu amjalie apate vitu vyake
 
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?

Angepanda ndege mngelalamika pia.

Huna hata jema
 
Wewe endelea kuchapa usingizi tu yaani mtu mkurugenzi mstaafu wa wizara ya misitu maliasili na utalii unamchukulia simple kama mama ntilie mstaafu.

Ni bora ukae tu kimya jamaa wamekuzidi hoja. Claim yako haina mashiko, sanasana inakuexpose kama mtoto ambaye hajakuwa bado ufahamu wake wa maisha upo chini.
 
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?

why not using public transport? mimi acha waseme nikiwa bongo napanda zangu dala dala kama kawa haimaanishi kuwa sina gari au uwezo wa tax, bali maamuzi tu..ishi upendavyo usiishi watakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…