Tatizo la wabongo bana....mbona mawaziri wa finland wanaenda kazini na baskeli?rais wa uswis hakai ikulu,anakaa kwake,rais wa uruguay anapanga foleni hospitali!nyerere alishirikiana na wananchi kulima....sasa ukishapata u director hapa bongo...ni kuinyonya nchi mpaka basi!..dr.pole anyways!Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?
Unaponiita Mshamba hua una maanisha nini? kwamba mimi naishi shamba au sijawahi kufika mjini au una maanisha nini?
Soma Thread vizuri
Wadau, hapa chini nakuleteeni kilio cha Dk. Kilahama. Ameniomba niwasilishe ujumbe huu kwa wadau akiamini JF ipo kila mahali. Tafadhali usomeni na tuone namna ya kumsaidia.
Kupitia huduma ya mitandao ya kijamii, Dk. Felician B. Kilahama, anayo masikitiko makubwa sana kutokana na kitendo cha baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema walisababisha apoteze begi lake lililokuwa na vifaa vyake muhimu. Hali hii ilitokea tarehe 06 Julai 2014 akiwa njiani kutoka Iringa na ilikuwa kati ya Morogoro na Picha ya Ndege-Kibaha ilipodhihirika kuwa hilo begi ambalo lilikuwa na vifaa muhimu likawa halipo sehemu ambako alilihifadhi.
Vifaa hivyo ni pamoja na laptop, camera (canon ndogo), kisanduku cha miwani ya kusomea kikiwa na miwani pamoja na modems za internet mbili- Voda na Zantel; funguo za nyumbani, simu yenye njia mbili - Tigo na Zantel, flash discs kadhaa, nyaraka muhimu na dawa kadhaa za kisukari na BP. Hali ya kuibiwa kwa begi hiyo ilijulikana baada ya kufika Picha ya Ndege, Kibaha na kijana mmoja akawa anateremka hapo na akasema ameibiwa computer yake. Ndipo Dk. Kilahama aliposhtuka na akaangalia sehemu aliyokuwa amehifadhia begi lake ikawa halioni na kutafuta kila sehemu bila ya mafanikio. Hivyo kuashiria kuwa limeibwa.
Pia Msafiri mwingine naye akaona sehemu alipoweka computer yake haipo! Kikawa ni kilio. Inasemekana wanaume wawili waliteremkia sehemu ya Mlandizi na kwa kuwa ilikuwa saa tatu usiku na ilikuwa giza; lakini baadhi ya abiria waliowaona wakiteremka na mabegi yanayodhaniwa kuwa ni hayo yaliyotea.
Kwa hali hiyo wakazi wa Mlandizi wanaombwa kuwa wadadisi kwa watu watakaoonekana wakiuza vitu kama hivyo. Waliochukua vitu hivyo wanefanya kitendo cha kinyama na ni dhahiri kuwa hawatatumia vitu hivyo, bali wataviuza. Wakazi wa Mlandizi na maeneo mengineyo wanatahadharishwa kuwa waangalifu katika hili. Watakaoona dalili zozote za picha au nyaraka zinazomhusu Dk. Kilahama watoe taarifa katika Kituo cha Polisi au kwa viongozi wa eneo husika.
Pia ikitokea kuwa nyaraka au dawa zimetupwa mahali tafadhali peleka kwa viongozi au kituo cha polisi au piga simu 0783 007400 au 0756 007400. Tafadhali sana tushirikiane katika hili na tufichue wahalifu wa aina hii.
NB. Dk. Kilahama ni Mkurugenzi wa Misitu mstaafu katika Wizara ya Maliasili na Utalii
ushamba wako ni wewe kuona mtu kutumia public transport ni tatizo, ungekuwa umetembea nchi za watu usingesema hayo maneno yako ya kejeli kwa Dr. K. kusafiri na private CAR huku kuna usafiri wa kuokoa matumizi yasiyo na sababu kuna tatizo gani, ushamba wako uko hapo.
unashangaa nin sasa kwani kupanda gari la abiria ni ajabu? kwani yeye siyo abiria .kwel ndio maana hii nchi hatuendelea na hatutaendelea kama tutakuwa na kizazi kama chenu.wakati nchi zilizoendelea watu kama professa wanapanda baskeli.
R.I.P vifaa vya Dr kilahama.
Ndugu yangu we acha tu, hayo ndio mawazo ya vijana wetu wa sasa. Yaani anashangaa mtumishi mstaafu kupanda basi, tena la elfu 35 anadai!!. Hivi kwa mawazo kama haya huyu kijana apewe uafisa wa idara ya wanyama pori unadhani atalifanyia nini taifa lake. Tuna kazi sana kutoka hapa tulipo ni kwa sababu sasa hivi ufisadi umekuwa kama pumzi. yaani mtu bila kufikiria kukwiba haamini kama maisha yake yatakuwa. Tuna kazi sana kubadiri hii mentality kwa vijana wetu.
si umeambiwa ni mstaafu!!!Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?
si umeambiwa ni mstaafu!!!
Tatizo la wabongo bana....mbona mawaziri wa finland wanaenda kazini na baskeli?rais wa uswis hakai ikulu,anakaa kwake,rais wa uruguay anapanga foleni hospitali!nyerere alishirikiana na wananchi kulima....sasa ukishapata u director hapa bongo...ni kuinyonya nchi mpaka basi!..dr.pole anyways!
Tatizo sio gharama za kununua vitu vingine, ila taarifa zilizo ndani ya laptop na hizo flash Hazina bei Mkuu! Hazinunuliki lakini ni muhimu mno Kwa mwenye Mali.atanunua vingine
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?
huyu ni mtetezi mkubwa sana wa misitu. Namkubali na nahisi hata kustaafu kwake kuna walakiniAliifanyia nn nchi hii kipindi cha uongozi wake? Isije kuwa wananchi wamerudisha mali alizowaibia
Tatizo sio gharama za kununua vitu vingine, ila taarifa zilizo ndani ya laptop na hizo flash Hazina bei Mkuu! Hazinunuliki lakini ni muhimu mno Kwa mwenye Mali. Wakati mwingine wezi ni Lazima wawe na utu, wachukue hizo computer lakini wanyinye hizo taarifa na kuzikabidhi mahali Fulani.
Nawaza ni kiasi gani ningeumia endapo ningenyanganywa hii iPad"
Kwahiyo Akiwa mstaafu ndo nini?
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?
Naendelea Kushangaa na ninaomba mnisaidie kushangaa nyie wenzangu,
mtu mwenye hadhi ya ukurugenzi kisha doctor anapanda gari la abiria ya tsh 35,000?
tatizo nini hajapewa gari? hajapewa dereva?
Acha Kujifanya unaijua sana nchi hii.mkurugenzi wa mali asili na utalii upande basi? sifanyi hata siku moja