Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,461
Wadau, hapa chini nakuleteeni kilio cha Dk. Kilahama. Ameniomba niwasilishe ujumbe huu kwa wadau akiamini JF ipo kila mahali. Tafadhali usomeni na tuone namna ya kumsaidia.
Kupitia huduma ya mitandao ya kijamii, Dk. Felician B. Kilahama, anayo masikitiko makubwa sana kutokana na kitendo cha baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema walisababisha apoteze begi lake lililokuwa na vifaa vyake muhimu. Hali hii ilitokea tarehe 06 Julai 2014 akiwa njiani kutoka Iringa na ilikuwa kati ya Morogoro na Picha ya Ndege-Kibaha ilipodhihirika kuwa hilo begi ambalo lilikuwa na vifaa muhimu likawa halipo sehemu ambako alilihifadhi.
Vifaa hivyo ni pamoja na laptop, camera (canon ndogo), kisanduku cha miwani ya kusomea kikiwa na miwani pamoja na modems za internet mbili- Voda na Zantel; funguo za nyumbani, simu yenye njia mbili - Tigo na Zantel, flash discs kadhaa, nyaraka muhimu na dawa kadhaa za kisukari na BP. Hali ya kuibiwa kwa begi hiyo ilijulikana baada ya kufika Picha ya Ndege, Kibaha na kijana mmoja akawa anateremka hapo na akasema ameibiwa computer yake. Ndipo Dk. Kilahama aliposhtuka na akaangalia sehemu aliyokuwa amehifadhia begi lake ikawa halioni na kutafuta kila sehemu bila ya mafanikio. Hivyo kuashiria kuwa limeibwa.
Pia Msafiri mwingine naye akaona sehemu alipoweka computer yake haipo! Kikawa ni kilio. Inasemekana wanaume wawili waliteremkia sehemu ya Mlandizi na kwa kuwa ilikuwa saa tatu usiku na ilikuwa giza; lakini baadhi ya abiria waliowaona wakiteremka na mabegi yanayodhaniwa kuwa ni hayo yaliyotea.
Kwa hali hiyo wakazi wa Mlandizi wanaombwa kuwa wadadisi kwa watu watakaoonekana wakiuza vitu kama hivyo. Waliochukua vitu hivyo wanefanya kitendo cha kinyama na ni dhahiri kuwa hawatatumia vitu hivyo, bali wataviuza. Wakazi wa Mlandizi na maeneo mengineyo wanatahadharishwa kuwa waangalifu katika hili. Watakaoona dalili zozote za picha au nyaraka zinazomhusu Dk. Kilahama watoe taarifa katika Kituo cha Polisi au kwa viongozi wa eneo husika.
Pia ikitokea kuwa nyaraka au dawa zimetupwa mahali tafadhali peleka kwa viongozi au kituo cha polisi au piga simu 0783 007400 au 0756 007400. Tafadhali sana tushirikiane katika hili na tufichue wahalifu wa aina hii.
NB. Dk. Kilahama ni Mkurugenzi wa Misitu mstaafu katika Wizara ya Maliasili na Utalii