Dk. Kijaji: Serikali haiwezi kupangia riba taasisi za fedha

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
586
huyu si mwingine naye ni Dkt Kijaji naibu waziri wa wizara ya fedha na mipango, ametabanaisha usomi wake leo alipokuwa akijibu swali la mbuge wa viti maalumu Mh, Faida Mohamed Bakar aliyeuliza swali la kwamba kwanini serikali isingilie kati masuara ya riba zinazotozwa na taasisi za kifedha yakiwemo mabenki na microfinance?,

Dkt Ashatu kijaji kwa umahiri mkubwa alijibu swali hilo kwa kusema "kuwa serikali haiwezi kuingilia masuara hayo kwakua ilishakwisha kujitoa moja kwa moja kwenye shughuli za kifedha toka mwaka 1991 ili kuruhusu ushindani huru wa kuboresha huduma katika sekta ya fedha , hivyo viwango vya riba vinavyotozwa na taasisi za kifedha hupangwa kulingana na nguvu ya soko , pamoja na gharama za upatikanaji wa fedha halikadhalika gharama za uendeshaji na sifa za mkopaji".

my take , hawa ndiyo wasomi watakaoisaidia serilikali yetu kwenda mbele zaidi nadhani hata angeulizwa kuhusu suala la upatikanaji wa sukari angekuwa na maelezo ya kina.

HEKO DKT KIJAJI HONGERA SANA .
 
Mkuu serikali ni wajibu wake kuwalinda raia wake haya mabenki yanawanyonya watanzania ambao wanachukuwa mikopo benki wanajipangia riba kubwa amabazo ni mzigo kwa wananchi.

Waziri kusema serikali haiwezi kuingilia hilo jambo ni sawa na kuchoma visu vya migongoni raia wake.

Serikali ni wajibu wake kuwasaidia raia wake siyo kushirikiana na mabenki ya kigeni kuwaibia raia lazima waweke utaratibu kwenye viwango vya riba.

Mbona serikali iliingilia Upatu baada ya kuona raia wake wanatapeliwa.
 
Huu utapeli wa mabenki kumbe umehalalishwa Na Serikali, kujibu Suala hili Kama Halina maslahi kwa wananchi ambao wamewachagua Ni kuwarejesha nyuma
 
Mkuu serikali ni wajibu wake kuwalinda raia wake haya mabenki yanawanyonya watanzania ambao wanachukuwa mikopo benki wanajipangia riba kubwa amabazo ni mzigo kwa wananchi.

Waziri kusema serikali haiwezi kuingilia hilo jambo ni sawa na kuchoma visu vya migongoni raia wake.

Serikali ni wajibu wake kuwasaidia raia wake siyo kushirikiana na mabenki ya kigeni kuwaibia raia lazima waweke utaratibu kwenye viwango vya riba.

Mbona serikali iliingilia Upatu baada ya kuona raia wake wanatapeliwa.
Kuna jamaa 1anamiliki Kichwa kwaajili yakufugia Nywele tu....Anataka sote tujue kwenye ukoo wao wamefanikiwa kutoa NAIBU WAZIRI ni upuuzi kusema Serikali haiwezi kuingilia riba za maBANK
 
Aisee, kumbe serikali haina regularities kwa taasisi za fedha! Watanzania endeleeni kuumia na riba, mabenki kamueni mpaka mwisho.
 
sifa za ajabu ajabu sana! serikali ikae kimya tu ata kama benk zinatoza riba ya 98%???

Nenda kafikirie upya then urudi na thread nyingine ya kutuomba radhi kwa kutupotezea muda kusoma misifa isiyo na chanya!!r
 
BOT ndio ina kazi ya kupanga interest rate, uyu naibu waziri ajui akisemacho wala akitendacho
 
BOT ina kazi ya kuregulate mzunguko wa pesa katika soko la pesa, mfano pesa ikiwa nyingi sokoni BOT watawambia Banks waongeze riba ili wawazuie raia kuomba mikopo na hapo mabenk yatakusanya pesa na kuzirudisha benk.Mfano wa pili ni pale pesa inapokua kidogo katika mzunguko wa pesa basi BOT watawambia Mabenki yote yapunguze riba ili watu waweze kukopa na kuongeza pesa katika mzunguko.Dk ajui asemacho wala ajui kazi ya Benk Kuu.
 
mimi nilifikiri BOT ndio wanapanga interest rate??????

BoT wanapanga interest rate indirectly kwa kupanga interest rate wanayopata mabenki ya biashara wanapoweka ela zao BoT au kukopa au kukopesha serikali/BoT. Kwahiyo unategemea kwamba interest rate ya BoT ndio iakisi interest rate wanazotoza mabenki ya biashara kwa wawekezaji. Sasa ulimwengu wa biashara bado unawaachia mabenki kujitengenezea faida kwa kuongeza interest rate kutokana na sifa za mkopaji au hali ya uchumi.
 
Back
Top Bottom