nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
ALHAMISI, MEI 23, 2013 06:04 NA JOHN MADUHU, MWANZA
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Wilaya ya Busega, Dk. Raphael Chegeni amesema wanachama wa chama hicho wenye nia ya kuwania nafasi hiyo wanapaswa kujitokeza mapema wananchi waweze kuwapima kama wanatosha. Dk.
Chegeni alisema CCM inapaswa ibadilishe kanuni zake juu ya viongozi wanaotaka kuwania nafasi za juu za dola kuepukana na utaratibu wa kumchomoa mgombea kwenye bahasha katika dakika za mwisho.
Aliyasema hayo siku moja baada ya Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye kukanusha taarifa zilizodaiwa kumkariri Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete akiruhusu wanachama wa chama hicho wanaowania urais kuanza kujipitisha
Dk. Chegeni alisema jana kuwa utaratibu wa kumchomoa mgombea dakika za mwisho ili asimame kupitia chama hicho umekuwa ukikigharimu chama.
Alisema hiyo ni kwa vile unakuwapo muda mfupi kwa wananchi kumfahamu na kumfanyia tathmini ya kina kama anafaa kuwa kiongozi wao wa ngazi ya juu.
Watanzania wanahitaji Rais mchapa kazi, mahiri wa kupambana na rushwa na mwenye kuthubutu hivyo kutangazwa mapema kutakisaidia Chama cha Mapinduzi kuweza kuibuka na ushindi kwa kuwa atakayechaguliwa atakuwa ana vigezo vyote.
Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Kenya wananchi wa nchi hiyo walipata nafasi ya kuwafahamu wagombea wao mapema na kuwachuja kwavigezo walivyo navyo na hivi sasa nchi hiyo ina Rais aliyepatikana kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wenyewe.
Mbali ya wananchi kuwajua mapema wagombea walipata nafasi ya kuwashuhudia katika midahalo iliyokuwa imeandaliwa .tuondoe uoga na wasiwasi, alisema Dk. Chegeni.
Dk Chegeni pia alivigeukia vyama vya siasa vya upinzani navyo viwe na utaratibu wa kutangaza wagombea wao mapema ili kutoa fursa kwa wananchi kuwapima na kuwapigia kura.