Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
DJ Khaled anafahamika kwa kuwa mtu anayeongea sana lakini si pale anapokuwa mbele ya Beyonce.
Mkali huyo anazunguka na Queen Bey kwenye ziara yake ya Formation.
Ameliambia gazeti la The New York Times kuwa heshima aliyonayo kwa Bey ni kubwa mno kiasi cha kuwa muoga wa kuongea sana akiwa nay ili asije akaharibu.
“Nakuwa mkimya sana. Muda wote ambao nimewahi kuonana naye ni pale ninapokuwa na kaka yangu Jay Z, na huwa nasema “Hi,” na kuangalia upande mwingine haraka na ni kama nakimbia,” alisema.
“Sitaki tu kuongea sana. Siwezi nikaharibu.”