DJ JOH wa 93.1 Marekani acheza Ngoma za Diamond!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Haya sasa naona taratibu ule ubishi wa kuwa nyimbo za Afrika hasa Tanzania hazichezwi kwenye vituo vya Radio za Marekani unaelekea kuisha!

Dj Joh wa 93.1 Marekani akihojiwa na Millard Ayo amezungumzia nafasi ya wasanii wa Afrika kusika katika vituo vya Radio vya marekani!! Amelezea Mengi lakini amekiri mara ya kwanza ili apate hiyo kazi ilibidi adanganye na alikataa kuwa yeye si mtanzania kutokana na ubaguzi lakini baadae alikuja kukubari kuwa ni mtanzania baada ya kazi zake kuanzwa kupendwa! Alienda Marekani kwa ajiri ya kusoma lakini alifika hatua akaanza kuwa Dj lakini hakuruhusiwa kuplay nyimbo za kiafrika kwani hakuwa anaruhusiwa!!

Anasema yeye ni anapenda Afro Pop na anaupenda sana mziki wa Diamond!!!! Kwa mara ya kwanza alijitosa na kuanza kuplay nyimbo za akina P-squre,Wizkid na Diamond!!! Anasema siku hiyo alipokea comments nyingi sanaaa zilizo mpongeza na kufanya yeye kuongeza juhudi ya kuplay nyimbo za kiafrika hasa Za diamond

Anasema siku ambayo hatoisahau ni siku Alio play nyimbo za Diamond na baada ya kipindi alipigiwa simu na Mtu ambae ni Mmarekani na alimuuliza kuwa Diamond kamfahamia wapi ndipo Dj Joh alipo sema yeye ni mtanzania na anamfahamu Diamond!!! Yule mmarekani alimwambia yeye Kwa Afrika Diamond ndo Msanii anaye mvutia na kwenye Gari yake muda mwingi huwa anasikiliza nyimbo za Diamond japo haelewi lugha!!! Dj Joh amesema kuwa Yule mmarekani alimwambia wiki ijayo nina harusi yangu na ninaomba uje Uwe Dj kwenye Harusi yangu na Nyimbo za Diamond uwe nazo nyingi!! Hapo Dj Joh anasema alifurahi nakuona kuwa mziki wetu sasa unakuwa!! Dj Joh amesema number don't lie kwani ni wengi walio mpigia simu na kumpongeza na kumtaka kumjua Diamond!!!

Mbali na hilo kuna siku Diamond alipost video ilionesha sehemu fulani Marekani watu wapo kwenye shuhuri wakisikiliza Nasema nawe!! Millard ayo ameongeza na kusema kuwa pia kuna kituo kingine cha Radio marekani kinachoitwa CSB nacho hucheza nyimbo Za Diamond!!!

Ni wazi sasa mziki wetu umefika mbali!!! Kuna siku niliwahi sema Diamond nyimbo yake na Neyo itachezwa sana kwenye Vituo vya Radio vya Marekani lakini watu walinipinga sana humu na sasa limeanza kujidhihirisha Kabla hata ya hiyo collabo
 
yeah kwasababu huyo jamaa nae mtanzania anaonesha uzalendo
 
Hadi raha kufahamu habari hizi, madale naenda kuweka kambi nje hadi na mie niingie nione sinki la gold....eeeeee kutaliii tu kwa mume wa Zari
Ahahaaaaaah...
Watu mna MANENO...
Umenifanya nicheke kwa nguvu...
Nafikiri nimeonekana HAMNAZO kidogo hapa nilipo..!
JF bhana...
 
Marekani nyimbo za Tanzania zinapigwa ila katika party za watanzania. Huwezi kwenda kwenye party za Nigerians ukasikia wimbo wa Tanzania hiyo ni bahati tu. Huyu jamaa anapiga hizo nyimbo ni kwa sababu ni mbongo tena anapiga kwa kuibia. Tusidanganyane, Marekani kupiga wimbo wa Kiswahili redioni unamwimbia nani? Wale kule wamekaa kibiashara zaidi si kihasara. Labda hiyo iwe redio ya community kwani wao huwa wana vipindi kadhaa kwa wiki (kila jumamosi au jumapili) kwa lisaa au masaa kadhaa hizo redio (za community events) hupiga nyimbo za nje na hazina sifa kihivyo. Tuache kudanganyana jamani. Watanzania wanaoishi Marekani can attest to this.
 
Ziishie huku huku ukipeleka insta utakutana na ile team nyingine ndo itakuwa balaaaa!
 
Sababu ni USA tu, muziki yake pendwa ilishakubalika kitambo
 
Marekani nyimbo za Tanzania zinapigwa ila katika party za watanzania. Huwezi kwenda kwenye party za Nigerians ukasikia wimbo wa Tanzania hiyo ni bahati tu. Huyu jamaa anapiga hizo nyimbo ni kwa sababu ni mbongo tena anapiga kwa kuibia. Tusidanganyane, Marekani kupiga wimbo wa Kiswahili redioni unamwimbia nani? Wale kule wamekaa kibiashara zaidi si kihasara. Labda hiyo iwe redio ya community kwani wao huwa wana vipindi kadhaa kwa wiki (kila jumamosi au jumapili) kwa lisaa au masaa kadhaa hizo redio (za community events) hupiga nyimbo za nje na hazina sifa kihivyo. Tuache kudanganyana jamani. Watanzania wanaoishi Marekani can attest to this.
We unaishi Marekani sehemu gani??
 
unabishana na millard ayo alioweka kambi mwezi sasa marekan aya tuambie ww unaishi marekani ipi ambapo ujawahi ckia hata radio mmoja ikipiga nyimbo.za Tz
 
Nilikuwa Florida just mwezi uliopita kwa miezi 3. Niliishi huko miaka ya nyuma pia. Ninabisha na niko tayari kubishana na Millard Ayo juu ya hili. It's NOT true, hakuna redio kubwa Marekani inayopiga nyimbo za Bongo, msiwe wajinga kihivyo. Kuna madj wa Tanzania wanaopiga nyimbo za Tanzania kwenye redio za mitandao na zinawalenga wabongo tu. Nani Zaidi ya East Africans anaongea Kiswahili Marekani? Waanfrika wenyewe waishio Marekani hawapigi nyimbo za watanzania kwenye redio zao za community.
 
Back
Top Bottom