Dizasta Vina a.k.a Maradona

ukiacha track ya SHAHIDI, Ngoma ya KANISA aliandika akiwa ametuliza Sana akili walau angekua kwenye hiyo class kwenye ngoma zingine Kama tano ningemshindanisha na Nikki mbishi lakini bado ajipange
Mwambieni dogo atupe taulo chini akaze gemu sio lelemama na kusifiwasifiwa Insta na Twitter kunamlemaza, ukifanya kweli mboni utasifiwa hata na asiekujua kwamba huyu mwamba ni kisanga kingine, Disasta najua upo humu kaza acha kulewalewa sifa tutakusahau toa mtiririko wa vyuma vikali, Niki Mbishi - Mama Luciya ndio naisikiliza hapa mda huu
 
Kwanza hao kina boshoo ndo hamna kila kitu. Uwezo wao ni hamna ni dhaifu Ila hamna namna ndo maana Nikki mbishi kwenye ngoma ya maji Ni uhai Kuna mstari anasema "naaumia kujua chin bees ndo Yule King Kong" yaani kina chin bees wanaonekana ndio warithi wa kina chid Benz.. Sasa fikiria Leo hii kina boshoo ndo replacement ya Langa, Jay Moe, Solo thang, professor Jay... [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Si aibu mkuu tuwe seriously...
Walau Lunduno members/Tamaduni music ndo wasanii wangu wa mwisho kabisa baada ya hapo sitaki kabisa kusikiliza kizazi kilichofata....

Msikilize Bando mc anakwambia eti "demu wako akilala na Dera jua Kuna mtu anaenda kuchambwa ndotoni" Sasa kweli huu Ni mstari????

Kwenye ngoma ya TEMANOLEJI ya Fid Kuna mstari anasema "nikisikiliza hip-hop ya bongo si-gain na-lose vitu/ mamc wote waongo na wananiiuzi kilasiku... Mistari Yao Ni Kama mfano wa kile kisichofaa kuandikwa/ sauti zao si za michano walipaswa wajiunge misifa...." [emoji16]

Jamani jamani hip-hop bongo imekosa watu kabisa Kama young Lunya anaonekana n msanii bora wa hip-hop si Ni aibu kwa taifa
 
Dizasta kulinganisha na Raptcha Ni utani Raptcha na genge lake la kina Lunya,bill nas, manengo na wengine wote waalitakiwa wafunguliwe kesi ya kujinufaisha kupitia hip-hop hao sio wasanii wa HIP-HOP Bali n kichekesho...
 
Sikupangii lakini ukimtoa Young killer na Dizasta hao wengine sijawai ona Kama Wana kitu Cha kunifanya niwafatilie nao nawaunganisha kwenye kundi la kina Lunya tu...
Toxic fuvu Ni mkali but Ni upande wa freestyle... Huko ndo nilimkubali Sana
 
Sikupangii lakini ukimtoa Young killer na Dizasta hao wengine sijawai ona Kama Wana kitu Cha kunifanya niwafatilie nao nawaunganisha kwenye kundi la kina Lunya tu...
Toxic fuvu Ni mkali but Ni upande wa freestyle... Huko ndo nilimkubali Sana

Take your time kamsikilize Ghafla
Anaandika councious sana thou kweli hajafika level za akina dizasta or young killer lkn kuna vitu utapata..!

Kama ulikubali ngoma ya kontawa-champion


Basi Ghafla alikuwa nazo hizo kitambo
 
sauti zao si za michano walipaswa wajiunge misifa / young Lunya anaonekana n msanii bora wa hip-hop si ni aibu kwa taifa..
Nimekuelewa nimekuelewa Ila wapo ambao hawajakuelewa utofauti wa vizazi nilimwambia Jana mwamba humu ampe Disasta title ya wimbo aiite VIZAZI HAVIFANANI kisha atengenezee story atembee ndani hio title mwanzo mwisho na ilete maana
 
Naam Kuna siku nilisema inabidi afanye ngoma ambazo zitapenya mainstream wakanidiss kua sijui kitu Mara kichwa panzi... Nikacheka sana. Kwani mbona kina solo thang, roho Saba, Rado, kalapina walikua wanafanya ngumu lakini zilikua zinaimbwa kina Kona [emoji16]

Kumbuka enzi zile kikosi Cha mizinga walikua wanatoa ngoma ngumu kinyama we kumbuka tu mstari wa mbele au moja Ni nguvu Ni ngoma ambazo zilitikisa kinyama na n ngumu zenye panchi kinyama au Nako 2 Nako walikua wanashusha Mapini magumu lakini yanahit Hadi kina dada wanakariri mistari nakumbuka enzi hizo tuko skuli unakuta demu anaweza kukuachania Hawatuwezi, niaje Ni vipi, au kimbia fasta ya babuu w akitaa Hadi unaona aibu... Sahivi sio rahisi mtu ambaye sio shabiki lialia wa hi-hop kuchana hata mistari mitatu tu ya Dizasta.

Fikiria wakati Stamina ametoa ngoma ya kabwela ilikimbiza kila Kona hadi wamama walikua waniimba je yenyewe sio ngumu? Kuna demu flani hivi aliwahi kuchana ngoma ya Nikki mbishi "kill your self" kwenye audition ya bongo star search Hadi majaji wakapagawa..

Hakuna aisiyemkubali Dizasta labda mwehu lakini ajifunze na akaze bado ana safari ndefu Sana.
 

Track11:nyota ya mchezo bonge la ngoma

Ofcoz naunguna na nyinyi kabisa
Hatuwezi kumfikisha dizasta level za akina fid hata nusu bado hajafika.fid ana kila kitu mpaka flow yake ni [emoji91][emoji91]

Ongeza piaa last album yake ya “KITAALOJIA”

Ngoma zote ni hit huwa na skip “intro” tu

Halafu nkifika kene “ulimi mbili” naweka [emoji681]
 
Take your time kamsikilize Ghafla
Anaandika councious sana thou kweli hajafika level za akina dizasta or young killer lkn kuna vitu utapata..!

Kama ulikubali ngoma ya kontawa-champion


Basi Ghafla alikuwa nazo hizo kitambo
Hiyo ngoma ya kontawa sijawahi ikubali Ina mistari ya kijinga tu kwanza kontawa Ni komediani sizani Kama n msanii...
Ye si ndo alisema huko kwao hakuna aliyetoboa zaidi ya kutoboa sikio??? [emoji23][emoji23]
Kweli huyu naye tunapaswa kumjadili au kumuacha akafie mbele
 
Yap tukiacha ushabiki Fid Q atabaki kua Icon ya Hip-hop ya bongo....
We sikiliza ngoma Kama ielewe mitaa...
"Usiache ulichotaka maishani ghafla tu na kufata kile ulichotamani..!" Ni mstari wenye maono na maonyo mengi Sana...
Ifike mahali wasanii hao wanaotakiwa kua warithi wajifunze kwanza kwa ngosha ze swagger don
 
Ndio hivyo inabidi akaze msuli asilewe misifa

Fid kuna line alisema "japo miluzi ni mingi lakini Jibwa sipotei...."

Sasa Disasta atoe vitu vikali miluzi itampoteza, kuna ngoma moja ya XPlastaz inaitwa Ushanta (Masai Hip Hop) mule ndani kuna storylines anatiririka Father Neli mpaka basi, alafu kuna nyingine inaitwa Ahaa! Daah ngoja nitulie kwanza
 
Mwanangu Kama unaijua ushanta we unajua ngoma hahahhahahahahahhahahahha umenifurahisha Sana hujui tu ungekua karibu ningekutunuku kreti tatu za bia na demu mmoja...
Kuna jamaa Alikua mwanaapolo akaanguka mgodoni anafungwa kudu kutolewa shimoni alivotoka wakati analilia Wana Waka mchana "Chali yangu unalala utafanywa kafala yerewiii"... Da you made my day [emoji28][emoji1787] [emoji106]
 

Mzee lakini unajua mziki umebadilika si sawa kulinganisha zama za akina Prof Jay ,Solo thang

Time flies and thing changes

Zamani bongofleva ilikuwa imebebwa na hiphop

Nowdays new generations media na mashabiki wanataka trap ngoma flani midundo wa kupigwa club

Na hapo ndo beef ya sugu na Ruge ilianzia
Kama ulifatilia Anti-Virus

Lakini turudi mpk tamaduni watu kama maalim Nash-kuwa na beef na media kubwa ambazo ndo zilikuwa zinaendsha biashara ya muziki

Hawa tamaduni wengi walishindwa kwenda na kasi na matakwa ya media enzi hizo that’s why wachache sana walifika mainstream

Kasikilize kivyovyote-one incredible

Amekupa summary nachokizungumza

So swala la young lunya kuwa mainstream na kutoa hit song ambazo zinaumbwa na kupigwa mtaani daily haimaanishi uwezo ni mkubwa kuliko walioko underground..!
 
"japo miluzi Ni mingi lakini jibwa sipotei..." Hapo Ni hayo tu... Kuna mstari fid anasema "hii Ni high level sio eye level ndo maana hunioni" bonge moja la punchline
 
😂😂😂 Ushanta!
 

Rest in Peace father Nelly
 
We ndo hujanisoma Kama unakumbuka zamani hip-hop ndo ilikua haipewi kabisa kipaumbele na ulikua unaonekana mziki wa kihuni.... Hadi pale genius Professor Jay alipokuja kutoa ngoma ya CHEMSHA BONGO enzi zile anajiita nigger Jay akiwa na kundi la hard blaster crew HBC.. hii ngoma sio Siri iliyafanya mapinduzi makubwa Sana ndo watu wakaanza kuitazama hip-hop kwa jicho lingine.. enzi zile muziki uliokua unabamba bongo Ni dansi kina mumini mwijuma na takeu za kina mr. Nice ndipo kina fid wakaibuka.

Kubali kataa Ni utunzi tu mzee mtu akiandika ngoma inayoigusa jamii lazima atapata airtime kubwa.

Dizasta nilianza kumfatilia alipotoa ngoma ya KANISA. lakini hakua na consistency ya vitu Kama hivo....

Young Lunya Ni msanii wa mchongo tukianza kuzungumzia hip-hop labda kategori nyingine kuvuma n Jambo la kawaida hata mandonga n superstar au hamorapa.... Lakini huwezi sema ni wasanii

Swala Ni moja tu wanahiphop wenyewe ndo wamekubali kutumika vibaya...

Mtu Kama Nash unakuta anauza albamu insta na hataki kuziweka kwenye platform zingine we unazani mtu ambaye hamjui Nash atamjuaje!? Sawa Ni swala la mapato je kwanini baada ya muda asiziachie? Mfano albamu ya diwani ya maaalim Hadi leo sijui Kama Kuna ngoma iliwahi kupigwa redioni... Hii sio nzuri kabisa msanii lazima uwe na brand... Sizani kama Tupac angejulikana angetumia hii njia... Nash mcee n msanii mkali lakini kwa staili hiyo n ngumu kuacha alama
 
"japo miluzi Ni mingi lakini jibwa sipotei..." Hapo Ni hayo tu... Kuna mstari fid anasema "hii Ni high level sio eye level ndo maana hunioni" bonge moja la punchline
Hio ipo kwenye album ya Fid Q inaitwa VINA MWANZO KATI NA MWISHO niliweka nyimbo zake zote kichwani kila ngoma nilikua nachana hata ukiniwekea beat kavu na-flow na sitoki nje ya beat, enzi hizo album inatoka mahome tunatumia Radio Cassatte bro akanizawadia Tape kilichofuata ni hakuna kuruka nyimbo maana nyimbo zote kali
 
[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my CPH1989 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…