Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Diwani: Wengi hatujawahi kuona katiba
Na Suleiman Abeid, Meatu
WAKATI mjadala wa kuishinikiza mabali ya katiba, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Shinyanga wameomba kupatiwa nakala ya katiba kila mmoja kwa kuwa wengi wao hawaifahamu.Walisema wakipatiwa nakala hiyo
wataweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu.Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita mara baada ya kuapishwa rasmi kuanza kazi ambapo walisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifanya shughuli zao bila kuwa na katiba.
âMheshimiwa mwenyekiti tuna ombi moja la msingi, tunaomba tupatiwe nakala ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maana wengi wetu hapa hatuifahamu, sasa iwapo tutakuwa na katiba ni wazi kuwa tutafanya shughuli zetu kwa uhakika na kwa kuizingatia.
âNi vigumu kutekeleza suala zima la utawala bora iwapo hatuifahamu katiba yetu. Tunaisikia tu, wengine hatujapata hata kuiona katiba hiyo machoni inafananaje, sasa tutafutiwe katiba na kila diwani apatiwe nakala moja, hata kama ni kwa kuzinunua tupo tayari kufanya hivyo,â� alieleza mmoja wa madiwani hao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu, Bi. Upendo Sanga aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo la madiwani na kueleza kuwa ni jambo linalowezekana.âMheshimiwa mwenyekiti, suala la katiba ni suala muhimu, ni vizuri viongozi wetu wakaongoza kwa kuzingatia katiba ya nchi, bila ya kuwa na katiba, ni wazi kuwa
utekelezaji wa dhana nzima ya utawala bora utakuwa mgumu, naahidi kulifanyia kazi ombi hilo mapema iwezekanavyo,â� alieleza Bi. Sanga.
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Meatu mwishoni mwa wiki liliwachagua Bw. Pius Machungwa kuwa mwenyekiti na Bw. Bassu Kayungilo kuwa makamu wake.