Diwani: Wengi hatujawahi kuona katiba

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,598
2,000
Diwani: Wengi hatujawahi kuona katiba


Na Suleiman Abeid, Meatu

WAKATI mjadala wa kuishinikiza mabali ya katiba, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Shinyanga wameomba kupatiwa nakala ya katiba kila mmoja kwa kuwa wengi wao hawaifahamu.Walisema wakipatiwa nakala hiyo
wataweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu.Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita mara baada ya kuapishwa rasmi kuanza kazi ambapo walisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifanya shughuli zao bila kuwa na katiba.

“Mheshimiwa mwenyekiti tuna ombi moja la msingi, tunaomba tupatiwe nakala ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maana wengi wetu hapa hatuifahamu, sasa iwapo tutakuwa na katiba ni wazi kuwa tutafanya shughuli zetu kwa uhakika na kwa kuizingatia.

“Ni vigumu kutekeleza suala zima la utawala bora iwapo hatuifahamu katiba yetu. Tunaisikia tu, wengine hatujapata hata kuiona katiba hiyo machoni inafananaje, sasa tutafutiwe katiba na kila diwani apatiwe nakala moja, hata kama ni kwa kuzinunua tupo tayari kufanya hivyo,â€� alieleza mmoja wa madiwani hao.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu, Bi. Upendo Sanga aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo la madiwani na kueleza kuwa ni jambo linalowezekana.“Mheshimiwa mwenyekiti, suala la katiba ni suala muhimu, ni vizuri viongozi wetu wakaongoza kwa kuzingatia katiba ya nchi, bila ya kuwa na katiba, ni wazi kuwa
utekelezaji wa dhana nzima ya utawala bora utakuwa mgumu, naahidi kulifanyia kazi ombi hilo mapema iwezekanavyo,� alieleza Bi. Sanga.

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Meatu mwishoni mwa wiki liliwachagua Bw. Pius Machungwa kuwa mwenyekiti na Bw. Bassu Kayungilo kuwa makamu wake.

 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,598
2,000
Unapoona viongozi wa ngazi ya Udiwani wanalalama hawana katiba ya nchi na kuchangia washindwe kutekeleza majukumu yao je rai wa kawaida ikoje hii?

Hivi mchakato wa katiba mpya utafanyika kwa ushirikishi kweli wa raia kama hata hii iliyopo haifahamiki........raia atajuaje maeneo yapi ya kuborosha kama hata hafahamu haki na wajibu aliopewa na hii katiba?

Mchakato wa katiba mpya uende sambasamba na kuhakikisha nakala za kutosha za katiba iliyopo zinasambazwa kwa raia ili wazisome na kuzitafakari Ibara zake kama zilivyo hivi sasa.....................
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,636
1,195
Diwani ameongea ukweli wake, lakini kwa rank yake katika jamii nadhani ni muhimu kuitafuta kuisoma vinginevyo hakuna atachokuwa anawatetea wananchi ambao wengine hata kusoma kwaoni shida!
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
@Ruta... mkuu hawa wawakilishi wa wananchi mitaani wanatakiwa kwenda na wakati hasa kipindi hiki cha utandawazi..... haihitaji nguvu nyingi sana kupata copy ya katiba.... nategemea kuwa kama wao ndio wameona mbali zaidi na kuamua kupata dhmana ya kuwakilisha wenzao basi hata mara moja kwa wiki wange attend hata internet cafe` zilizo karibu na sehemu zao.... nazingatia wengine wanatoka remote areas.... kwa hilo wangeweza kupata yanayojiri katika kufungua gurudumu la maendeleo ya wananci wao pamoja na kupata nyaraka muhimu kama katiba ya nchi

ushauri wangu ni kwamba kwenye regional libraries ziwekwe copies za katiba pamoja na kamwanasheria kamoja ka katiba aweze ku stipulate acts and sections....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom