Diwani wa vijibweni - kigamboni asusiwa mkatano baada ya kukataa kuulizwa maswali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa vijibweni - kigamboni asusiwa mkatano baada ya kukataa kuulizwa maswali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAZIMOTO, Jul 22, 2012.

 1. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DIWANI WA VIJIBWENI - KIGAMBONI ASUSIWA MKATANO BAADA YA KUKATAA KUULIZWA MASWALI

  Diwani wa kata ya vijibweni Suleiman Mathew ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa yanga na Tukuyu star aliitisha mkutano leo saa 8 mchana lakini akafika saa 10 jioni eneo la njia ya bomba la mafuta ya Tazama. Wengi wameuchukulia mkutano huo kama mkusanyiko kwa sababu wananchi walipoomba kuuliza maswali alikataa kwamba hadi mfungo Ramadhani utakapoisha atarudi kujibu maswali na kwamba atakuwa na mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine ndungulile.


  Wananchi wengi wamechukizwa na kitendo cha kutangaza kwamba kutakuwa na mkutano wa diwani ambapo wengi waliamini anakuja kutoa ufumbuzi wa mgogoro wake na mbunge hasa tuhuma za rushwa ambazo mbunge alimtuhumu diwani na madiwani wa Tungi, Kibada, vijibweni na Kigamboni.

  Mkusanyiko huo ulikuwa na watu wasiozidi 100 ambapo akina mama walikuwa asilimia 95. diwani alianza kugawa tenki moja ya maji ya lita 400 kwa kikundi cha akima mama, sepetu mbili na mipira ya kumwagia maji 5 kila mmoja una mita 40 na jezi za timu ya vijana, na komputa 4. kitendo hiki kiliwachuliza wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye juu ya mradi wa kigamboni.

  kuna wananchi wanasema kuna vijana wahuni akiwemo mmoja maarufu kwa jina la Mayuku na mtoto wa mzee Dororo walikwenda kumwomba mipira kwa ajili ya kumwagia mchicha na vikundi vya akina mama wenye njaa. swali ni kwa nini alitangaza ni mkutano wa wananchi?? kwa nini hakwenda kukabidhi vifaa hivyo katika maeneo ya vikundi hivyo, kwa mfano, jezi angekwenda uwanjani na tenki angewafuata akina mama kwenye eneo la mradi wao. wapo walisema amekuja kusafisha nyota baada ya tuhuma.

  Amewatumia wazee kumpamba akiwemo mzee maarufu, Mzee Mkani anayeishi karibu na kwa msomali. kipindi hiki wananchi wanapenda kusikia hatima ya mradi na wengine wanauliza diwani anaanzisha miradi ya kugawa tenki la maji wakati hawana uhakika na mradi huo, ambapo hawana uhakika wa kubaki.

  Amekuja na waandishi wa habari wakimemo Star TV na chanel 10 ambao waliuliza maswali watu waliokuwa wamepangwa na diwani. Wananchi hao wakaomba watu wa TV kuhoji na wengine hawakujali hisia zao wakaendelea kuhoji wachache ambao walikuwa wanatoka kwenye viti kama mpango maalum na kuacha waliokuwa wanalilia kuhojiwa.

  wananchi wanasema hao ni aina ya waandishi wa habari ambao wananunuliwa kwa kazi maalum na wanategemea vyombo vya habari kumpamba diwani kuwa kafanya mkutano na wananchi kwa kishindo na mambo kadhaa wa kadhaa.
   
 2. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananchi wamechukia aliwaambia mkutano utaanza saa 8 lakini ukaanza saa 10 hadi saa 11 ametumia saa moja. Ni kama amekuja kuwasalimia tu watu wapambe na Mc ndio walikuwa wanaongea mwisho akasema wananchi msiwe na wasiwasi na mradi lakini akakataa maswali?

  kuna waliosema diwani ameogopa kufanya mkutano kwenye uwanja wa mzimu uliopo eneo analoishi kwa hofu ya kutokea fujo. Wananchi wa eneo hilo hawana subira kwa makanjanja lakini pia eneo la magengeni kisiwani hapakuwa pazuri kwa mkusanyiko wa kukwepa maswali. kapeleka mkusanyiko huo mahali ambapo sio uwanja ni barabara ya nguzo za umeme na bomba la Tazama linapita hapo.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,789
  Likes Received: 36,804
  Trophy Points: 280
  sasa naona dhahiri hawa madiwani wamepewa rushwa kuwauza wananchi wa kigamboni kwa mkoloni mweusi.
   
Loading...