Diwani wa mungaa/singida - CHADEMA afyeka ng'ombe miguu

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Diwani wa kata ya mungaa MATEO ALEX KIANGO, katika jimbo la singida mashariki linaoongozwa na mbunge wa chadema Tundu Lissu yupo mahabusu kituo kikuu cha polisi Central singida tangu siku ya jumanne kwa kosa la kukatakata miguu ng'ombe sita na kufyeka shamba la alizeti ekari 2 la mwananchi kijijini mungaa.

Mh.Tundu Lissu alifika mjini singida jana kushughulikia dhamana lakini wananchi wenye hasira kali wamemtahadharisha kuwa wakimuona diwani huyo wanatenganisha kichwa na kiwiliwili.

polisi walimkamata na kumuweka ndani ili pamoja na mambo mengine, kunusuru maisha yake..Atafikishwa mahakamani wakati wowote.

MY TAKE. KIONGOZI NI MFANO WA KUIGWA, AKANYWE KUACHA TABIA HII YA KIKATILI NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE KUKOMESHA VITENDO KAMA HIVI.
 
kitendo kilichofanywa ni cha kinyama lakini ni vyema wananchi waepuke kujichukulia sheria mkononi kulipiza kisasi
 
Aisee Hili sakata niliona juzi kupitia startv. Ng,ombe kakatwa mguu wa nyuma yaani inasikitisha.Mama mwenye ng,ombe anasema ni heri angemkata yeye kuliko ng,ombe wanaomfanyia shuhuli zake. Lakin sakata hili lisihusishwe kwa vyovyote na CDM. Kwani ni yeye kama yeye hata akiwa ni kiongozi cdm
 
huyo atakuwa mhuni tu, kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kwa kura zao, hawezi kufanya unyama kama huu
 
Tatizo ndani ya cdm hakuna demokrasia hawachagui viongozi wanapendekeza ktk kugombea nafasi utawezaje kupima tabia ya mtu kuiongiza jamii. Ndg zangu mh. Lissu anapaswa kuacha kutetea maovu haya,uanasheria wake usiwe wa kitetea wezi na magaidi km hawa ili aoneshe maadili ya uongozi. Sisi tumeshuhudia ni unyama umefanyika wananchi tuungane kukemea bila kujali itikadi.
 
ni kweli mkuu, kwa kitendo kama hiki, mh tundu lissu alipaswa kuungana na wananchi badala ya kuungana na muovu, watu wataanza kuhoji uzalendo wake
 
huyu ni diwani pekee wa chadema aliyebaki katika jimbo la la tundu lissu baada ya yule kujiuzulu na kurudisha kadi ya chadema..alipaswa aenende kama kiongozi wa chama kichanga cha upinzani, matokeo yake amekichafua chama chake, kajichafua yeye pamoja na tundu lissu anayemtetea naye amejichafua
 
Ndg wana JF,
Naungana na wachangiaji wengine kupinga vikali kitendo kilichofanywa na huyu Diwani. Katika viwango vyovyote vile hakivumiliki na wala hakikubaliki.
Pamoja na haya yote napenda tu kuwakumbusha kwamba pamoja na unyama wote huu mtuhumiwa bado ana haki ya kisheria ya kupata dhamana maana makosa anayotuhumiwa nayo yanadhaminika. Na napenda tuelewe kwamba kitendo cha Mh. Lisu kumsaidia mshitakiwa kupata dhamana hakimaanishi kwamba Mh. huyu anasapoti na kukubaliana na kilichotendwa na mtuhumiwa, bali dhamana inabaki kuwa Haki ya mtuhumiwa kama kosa linadhaminika.
Tukilichukulia jambo hili katika mlengo huu wa kutambua haki ya dhamana kwa mujibu wa sheria basi mtakubaliana nami kwamba Lisu hapaswi kuonekana kama mtu anaekubaliana na kitendo cha huyu mhalifu.
Naomba kutoa hoja.
 
Aisee Hili sakata niliona juzi kupitia startv. Ng,ombe kakatwa mguu wa nyuma yaani inasikitisha.Mama mwenye ng,ombe anasema ni heri angemkata yeye kuliko ng,ombe wanaomfanyia shuhuli zake. Lakin sakata hili lisihusishwe kwa vyovyote na CDM. Kwani ni yeye kama yeye hata akiwa ni kiongozi cdm

kwa hiyo na Yule anaemaliza Tembo wetu asihusishwe na chama chake?.. nimeuliza tu....nisamehe kama nimekosea!!
 
mii ni CDM ila nasema huyu jamaa anyongwe! Yani ng'ombe anamkata mguu! kah!?
 
Tatizo ndani ya cdm hakuna demokrasia hawachagui viongozi wanapendekeza ktk kugombea nafasi utawezaje kupima tabia ya mtu kuiongiza jamii. Ndg zangu mh. Lissu anapaswa kuacha kutetea maovu haya,uanasheria wake usiwe wa kitetea wezi na magaidi km hawa ili aoneshe maadili ya uongozi. Sisi tumeshuhudia ni unyama umefanyika wananchi tuungane kukemea bila kujali itikadi.

Amekusikia.
 
huyu ni diwani pekee wa chadema aliyebaki katika jimbo la la tundu lissu baada ya yule kujiuzulu na kurudisha kadi ya chadema..alipaswa aenende kama kiongozi wa chama kichanga cha upinzani, matokeo yake amekichafua chama chake, kajichafua yeye pamoja na tundu lissu anayemtetea naye amejichafua

Mbona mnakurupuka uliambia Lissu alikwenda kumtetea.Kilichompeleka Lissu ni kutaka kujua kwanini amefanya hvyo ili ikibainika kosa basi chama kimchukulie hatua kali sana kama ilivyo desturi kwa cdm.
 
Ni kawaida kwa viongozi wa chadema kufanya vitendo vya kihalifu halafu bado washabiki wao wanawaona malaika
Nasikia hata yule afande bwire aliekata mapanga mwanawe alikuwa agombee udiwani kupitia chadema
 
Mabere Marando na Tundu Lissu wapo watamtetea atatoka Chadema makao makuu Kinondoni tumejipanga!
 
Ni kawaida kwa viongozi wa chadema kufanya vitendo vya kihalifu halafu bado washabiki wao wanawaona malaika
Nasikia hata yule afande bwire aliekata mapanga mwanawe alikuwa agombee udiwani kupitia chadema

Una akili. Mkuu una akili ya kukutosha peke yako. Hongera sana. Go ahead!
 
Kila mtu ana mapungufu yake,. Kama sikosei kuna mh. mmoja wa ccm alimgonga na gar mwanamke ucku wa manane ktk purukushani za kukimbizana na kesi ilimalizika..
Kweli ni jambo baya ila tusilichukulie kisiasa..
 
Wewe unaona mbali. Kwani CHADEMA ndiyo imemtuma kufanya huo uhalifu?. Hapana.
 
Back
Top Bottom