Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, akutana na madiwani wa jimbo la Singida Mashariki

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
20180325_210617-620x330.jpg



MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, leo Jumapili amekutana na madiwani wa jimbo la Singida Mashariki, linaloongozwa na Tundu Lissu.

Katika mkutano huo uliofanyika mjini Ikungi, Kubenea alikutana pia na viongozi wa Kamati tendaji jimbo na wilaya, pamoja na diwani pekee wa CHADEMA kwenye jimbo la Singida Magharibi, Emmanuel Jingu.

Kwenye ziara hiyo, Kubenea aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Kati, Alphonce Mbasa; katibu wa Kanda, Iddi Kizota na mbunge wa Viti Maalum, mkoani Singida, Jessica Kishoa.

Mkutano kati ya mbunge huyo na viongozi hao, ulilenga kusikiliza matatizo ya madiwani hao yaliyotokana na kutokuwapo kwa mbunge wao.

Aidha, mkutano huo ulilenga kupanga mikakati ya kukabiliana na hujuma za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na madiwani kupata taarifa sahihi ya maendeleo ya Lissu.

Hatua ya Kubenea kufika jimboni jimboni Singida Mashariki, imefuatia kuombwa kwake na Lissu kukutana na madiwani wake na viongozi wake wa chama.

Kubenea na viongozi wenzake waliwaeleza madiwani na viongozi hao wa kata kuwa wanalo jukumu kubwa la kukilinda chama na kumtetea mbunge wao kwa gharama yeyote ile.

Naye Lissu akizungumza kwa njia ya simu ya video, aliwaeleza madiwani na viongozi wake maendeleo ya afya yake na kutokubali kughiribiwa.

Alisema, “kwa kweli, ninaendelea vizuri. Afya yangu inazidi kuimarika. Nawahakikishia, nitarudi nikiwa mzima na ninayetembea.”

Aliongeza: “Ninawaamini sana. Sina mashaka yeyote na ninyi. Naomba pigeni kazi ili kulinda heshima yenu na hadhi zenu mlizopewa na wananchi.”

Lissu alitumia mkutano huo kumshukuru Kubenea kwa upendo wake kwake na kumuomba yeye na viongozi wengine kufika kwenye jimbo hilo mara kwa mara kuongea na wananchi wake.

Naye Mbasa – mwenyekiti wa Kanda hiyo – alimshukuru Kubenea kwa uamuzi wake kutembelea jimbo hilo.

Alisema, “uamuzi huu ni mzuri na unapaswa kupigiwa mfano. Ninakushukuru wewe na nawashukuru wote uliongozana nao katika safari hii.”

Kwa upande wake, katibu wa Kanda alisema, ziara ya Kubenea imeleta faraja kubwa kwa wananchi wa Singida Mashariki na Kanda ya Kati kwa ujumla.

Jessica Kishoa – akizungumza katika mkutano wa madiwani na viongozi hao wa jimbo, wilaya, mkoa na Kanda, alimhakikishia Kubenea kuwa mbegu aliyoipanda leo watailinda na hivyo itadumu.

Nao baadhi ya madiwani wamemshukuru Kubenea kwa hatua yake ya kufika jimboni humo na kumhakikishia kuwa watailinda heshima hiyo waliyopewa.
 
Uongozi wa Chadema unafaa kuteua mbunge yeyote wa viti maalum akaimu kwenye nafasi ya Tundu Lissu katika kuwakilisha matatizo ya wapiga kura wake.
 
Back
Top Bottom