Diwani wa CHADEMA Simiyu mbaroni kwa tuhuma za rushwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linamshikilia diwani wa CHADEMA katika kata ya Kimari wilayani Meatu,mkoani Simiyu aitwaye Peter Bukarasa 38 kwa tuhuma za kutoa rushwa ya shilingi milioni tatu kwa Askari Polisi ili shitaka lake lisipelekwe mahakamani.

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu ,Jonas Mahanaga ameambia ITV kuwa diwani huyo alikamatwa Septemba 15,mwaka huu majira ya saa 11 jioni huko katika kijiji cha paji wilayani Meatu na Askari Polisi kwa kushirikiana na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili,KDU kutoka wilayani Manyoni na kwamba baada ya kuhojiwa alikiri kuwa ana meno ya tembo yenye uzito wa Kg 250 ambayo alikuwa ameyahifadhi katika kijiji cha paji.

Kaimu Kamanda huyo amesema kuwa wakati wa mahojiano na polisi ndipo diwani huyo alipomshauwishi askari huyo,mwenye cheo cha mkaguzi aitwaye Mathias ili ampe rushwa ya shilingi milioni tano na askari huyo alikubali na kuwataarifu Takukuru ambao waliandaa mtego na ndipo diwani huyo alipowapigia simu ndugu zake ambao walileta kiasi cha shilingi milioni 3 huku akiahidi kumaliza nyingine mbili,na ndipo walipomkata na kumpeleka kwa mlinzi wa amani ambapo alikiri.

Kwa mjibu wa Kaimu Kamanda huyo diwani huyo atafikishwa mahakamani kwa kosa la awali la kukiri kuhifadhi meno ya tembo ambapo baadaye pia Takukuru itamfikisha mahakamani kwa kosa la kutoa rushwa.

Chanzo: ITV
 
Hahahahah sikubaliani kwenye hili nakataa kata kata,hizi ni kati ya kesi zinazobambikiwa watu kwa sababu ya itikadi zao.Ndiyo yale yale
 
Kesi imeshapelekwa Mahakamani tayari. Namna pekee ya kupinga kwenye hatua hii ni kumtafutia Wakili akamtetee huko, sio humu!
 
Sijapinga nimekataa,kama ni hivyo aliyeileta humu angeiacha ilipokuwa.Kaileta ili tuijadili
 
M
Sawa kabisa, tena afungwe kifungo kirefu sana maana chadema hatuungi mkono vitendo hivi
Mbona hata hapa Arusha diwani mmoja anatuhumiwa kukusanya Mil.300 kwa makada wa Chadema ili kugawa maduka na kupokonya waliojenga Stendi ndogo?
 
Ndio maana nikakuambia kwamba namna bora ya kulipinga ambako ndiko kulikataa kosa ni kumtafutia Wakili.

Unategemea hana wakili?Nimesema na bado nitasema sikubali hilo kosa kwa asilimia 100 ni la kubambikizwa tu
 
Kesi imeshapelekwa Mahakamani tayari. Namna pekee ya kupinga kwenye hatua hii ni kumtafutia Wakili akamtetee huko, sio humu!

Aliyeleta hoja alisema ukichangia lazima ukatafutae wakili?Ndiyo sababu watanzania tunaambiwa tunatumia 1% ya akili zetu kufikiri
 
Unategemea hana wakili?Nimesema na bado nitasema sikubali hilo kosa kwa asilimia 100 ni la kubambikizwa tu
Kwa faida ya Wana JF wengine. Jamani kuna watu tuliofuatilia jambo hilo tangu jana, tunazo taarifa kwamba alishafikishwa Mahakamani na akakosa Wadhamini wawili waliotakiwa kusaini bond ya Tshs 10 mil kila mmoja. Mpaka sasa yuko gerezani kama Mahabusu akisubiri tarehe ya Kesi itakapokwenda Mahakamani kwa usikilizwaji wa awali. Kama kuna mtu yeyote mwenye mawasiliano na Viongozi wa Chadema Mkoa wa SIMIYU na Wilaya za huko, basi asaidie mawasiliano ili ipatikane namna bora ya kumpatia msaada wa kisheria kamanda huyu.
 
Aliyeleta hoja alisema ukichangia lazima ukatafutae wakili?Ndiyo sababu watanzania tunaambiwa tunatumia 1% ya akili zetu kufikiri
Na huu ndio ukomo wa fikra zako kamanda wa keyboard.
 
Kwa faida ya Wana JF wengine. Jamani kuna watu tuliofuatilia jambo hilo tangu jana, tunazo taarifa kwamba alishafikishwa Mahakamani na akakosa Wadhamini wawili waliotakiwa kusaini bond ya Tshs 10 mil kila mmoja. Mpaka sasa yuko gerezani kama Mahabusu akisubiri tarehe ya Kesi itakapokwenda Mahakamani kwa usikilizwaji wa awali. Kama kuna mtu yeyote mwenye mawasiliano na Viongozi wa Chadema Mkoa wa SIMIYU na Wilaya za huko, basi asaidie mawasiliano ili ipatikane namna bora ya kumpatia msaada wa kisheria kamanda huyu.

Sasa ndiyo umetoa ufafanuzi ambao mtu anaweza kuufanyia kazi.Anyway kuna watu nimewauliza hawajanipa information.Nitakuinbox
 
habari ni nzuri,lakin iko kishabiki zaidi..kwan tumevaa miwani ktk sheria zetu kuwa mtoa na mpokea rushwa wote ni walewale?habari inaongelea mtoa rushwa tu,je mpokea rushwa?napata tabu sana kuelewa uwelewa wa watz,au mahaba niue?dah,kazi kweli kweli.
 
Sawa kabisa, tena afungwe kifungo kirefu sana maana chadema hatuungi mkono vitendo hivi
Afadhali,Juzi Diwani wa Mivinjeni chadema kadhulumu nyumba,leo utapeli diwani wa chadema simiyu...juzi Geita wananchi walipiga kura kutokuwa na imani na mwenyekiti wa serikali ya mtaa...hakika kama wangekuwa na raisi...hii nchi si wizi wa mali tu bali hata wizi wa binadamu ungetamalaki.
 
Back
Top Bottom