Diwani wa CHADEMA Mbweni ni jipu

Njaa Mbaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
666
175
Ni dhahiri kabisa CHADEMA wana wakati mgumu sana, diwani wa Mbweni ameshindwa hata kushughulikia madimbwi ya maji. Wananchi wamemfuata mara nyingi wakiwa tayari kuchangia uboreshaji wa miundombinu amekuwa akipiga chenga.

CHADEMA mnafuatilia viongozi wenu maana huyu jamaa watu wamemchoka hajui hata anapaswa kufanya nini, kweli Mbweni tumepata bahati mbaya sana kwa kuwa na huyu diwani.
 
Hata mwaka moja baado meanza kulialia je mlioka zaidi ya miaka 50 mlifanya nini?
Ndugu yangu suala si muda gani CCM wamekaa, hivi kiongozi watu wako wanakuambia tuko tayari kuchangia uboreshaji diwani anakuambia hebu mjiorganize wenyewe mimi niko bize jamaa anaboa sana nadhani kama ungekuwa wewe sijui ungefanya nini. Nakuomba kama ni mdau wa CHADEMA hebu wasaidie maana huyu jamaa huku kakimaliza kabisa chama watu hawamtaki
 
Binafsi sijawahi kumuona diwani wa chadema anayejitambua.
Ndugu yangu katika wote huyu ni kiboko, kwanza anatoa matusi bila aibu, aisee CHADEMA wametia aibu sana sijui nani anawasimamia kujua utendaji wao huyu jamaa ni zero kabisa sijui walimuokota wapi, pita mbweni mabarabara yote ni makorongo jamaa hana habari anapita bila aibu tumepata balaa wakazi wa mbweni
 
Kabla yake alikuwa nani? Aliyekuwa diwani hapo kabla hayo makolongo hakuyaona au hamkuyaona? Kwanini hamkujioganize kipindi hicho akiwepo huyo Diwani wenu wa C.C.M unayemsema alikuwa mzuri kuliko huyu wa CHADEMA? NA KAMA HUYO DIWANI WAKO WA C.C.M ALIKUWA MZURI NA NI DIWANI BORA, KWANINI HAMKUMCHAGUA TENA? Kijana acha unafiki
 
Kabla yake alikuwa nani? Aliyekuwa diwani hapo kabla hayo makolongo hakuyaona au hamkuyaona? Kwanini hamkujioganize kipindi hicho akiwepo huyo Diwani wenu wa C.C.M unayemsema alikuwa mzuri kuliko huyu wa Chadema? NA KAMA HUYO DIWANI WAKO WA C.C.M ALIKUWA MZURI NA NI DIWANI BORA, KWANINI HAMKUMCHAGUA TENA? Kijana acha unafiki
Kwa hiyo aliyekuwepo kama alikuwa mbaya basi huyu asifanye kazi kwa kuwa aliyemtangulia alikuwa mbaya nimeshindwa kujua unataka nini. Ninachojua huyu diwani ni jipu na linapaswa kutumbuliwa na CHADEMA wenyewe kama wanataka heshima ya chama
 
Anamuda gani tangu aingie na yule wa CCM ALIKAA KWA MUDA GANI BILA KUTATUA KERO HIYO? KAMA WA CCM ALIKUWEPO TANGU UHURU NA HAKUWEZA KUITATUA KERO HIYO IWEJE HUYU ALIYEKAA MIEZI TU AWE AMEMARIZA KERO ZOTE KWA WAKATI MMOJA? We unafikiri tatizo ni moja tu la barabara? Na unafikiri pesa zipo tu zimewekwa? Si mpaka zitafutwe?
 
Mtoa mada nadhani unaeza kuwa na sura mbili za maelezo yako;
a) kupigania maendeleo ya Kata
b) kuponda chama.
Kila Kata ina bajeti za utekelezaji wa shughuli zake na nadhani ingekuwa vizuri upatiwe ufafanuzi na mhusika iwapo ana bajeti au la. Na akupe maelezo kwa maandishi ndo uje uku na hiyo taarifa. Na hata kama mlitaka kujichanga kufanya maendeleo tuonyeshe bajeti yako na commitment yenu ya kufanya hilo zoezi. Raia tunaoishi eneo husika tusipende blabla na hadithi za barazani. Kama tuna nia ya kusaidia serikali ya Mtaa mkakati uwepo na taarifa rasmi zifikishwe ili idhini ipatikane
 
Back
Top Bottom