Diwani wa CHADEMA ashusha bendera ya CCM na kupandisha ya Taifa

Ni haki yake kikatiba, ofisi ya serikali ya kijiji why bendera ya CCM?
 
anatafuta cheap popularity hana lolote huyo eti na yeye atokee kwa gazeti na tv

kama CCM na watu kama wewe hamuwezi kutambua udhaifu wenu mtawezaje kutatua matatizo ya watanzania? Mtawezaje kutekeleza ile kauli mbiu yenu ya kitapeli "maisha bora kwa kila mtanzania"? Kweli CCM imechoka mno; kazi wanayojua ni kuvamia mikutano ya vyama vingine(hasa CDM), kutesa na kuuwa watu wanaotofautiana nao kimtazamo.
 
Hicho kijiji nakifahamu sana kina mwamko mkubwa sana wa kimaendeleo, nadiriki kusema, nini moja ya vijiji ambacho wananchi wake walikua na maisha mazuri sana, kabla ya miaka ya 2000, lakini uongozi mbovu na kuendekeza wawekezaji hewa ulisababisha watu wakanyang'anywa mashamba ya mpunga pamoja na vyanzo vya umwagiliaji, sasa hali ni mbaya sana na vijana wengi wamekimbilia mijini, hii kata ipo chini ya CHADEMA kwa sasa na huyo diwan anajaribu kufanya reforms
 
safi naona wapare nao wamechoka kutumiwa kama toilet na ccm!natamani uchaguzi uwe kesho ccm haina pa kujificha ipo hoi
 
Big up Albeto, nakukumbuka sana msimamo wako toka ukiwa UDsm. keep on tupo pamoja
 
Hao polisi wamefanya jambo la kipuuzi kabisa. Yaani hawajui kwamba hilo sio kosa. Kwani hapo ni shina la wakereketwa? Kwani hiyo ni ofisi ya ccm? Hawajui kwamba walitakiwa wamkamate aliyeipandisha hiyo bendera ya ccm kwenye ofisi ya umma? Au wanajitia wazimu tu!? Sasa wanamshtaki kwa kosa gani!? Kweli ndio maana kesi ya Zombe walimwacha mtuhumiwa wakaambiwa wakamkamate! Wanamwacha aliyepandisha bendera mahali si pake wanamkamata anayeishusha...! Kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
 
Hongera sana diwani tunakupongeza sana kwa kufuata sheria za nchi yetu.Kwa kushusha bendera ya CCM NA kupandisha Bendera ya Taifa umefuata Sheria za nchi.Waliotakiwa kushtakiwa ni wale waliopandisha bendera ya chama kwenye ofisi ya Serikali.NAKUPONGEZA SANA KAMANDA.
 
Jamaaa namkubali sana kwa ujasiri huu..

"Nipo Kituo cha Polisi Moshi nikiandika maelezo kuhusu tuhuma za kushusha bendera ya CCM kwenye ofisi za serikali ya kijiji chekereni na kupandisha bendera ya Taifa! Niko tayari sana kwa hatua zitakazochukuliwa".


Alberto Msando through Facebook
Diwani wa CHADEMA Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini
Ukishaandika statement, fungua mashtaka kwa aliyepandisha bendera ya CCM katika ofisi za serikali.
 
[h=6]Jamaaa namkubali sana kwa ujasiri huu..

"Nipo Kituo cha Polisi Moshi nikiandika maelezo kuhusu tuhuma za kushusha bendera ya CCM kwenye ofisi za serikali ya kijiji chekereni na kupandisha bendera ya Taifa! Niko tayari sana kwa hatua zitakazochukuliwa".
[/h]Alberto Msando through Facebook
Diwani wa CHADEMA Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini

hi mate fanya ukasaidiane na zitto na halima pale mjengoni chemba inawasumbua
 
Jamaaa namkubali sana kwa ujasiri huu..

"Nipo Kituo cha Polisi Moshi nikiandika maelezo kuhusu tuhuma za kushusha bendera ya CCM kwenye ofisi za serikali ya kijiji chekereni na kupandisha bendera ya Taifa! Niko tayari sana kwa hatua zitakazochukuliwa".


Alberto Msando through Facebook
Diwani wa CHADEMA Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini
nenda hapo KATC kuna makamanda wengi sana watatoa msaada wa kutosha! ila tuna hasira sana na Komu alivouza jimbo!!
 
Kama kijiji hakina ofisi ya chama, ingekuwa bora kazi zao wafanyie chini ya mti, jioni washushe bendera yao ikakae kwa katibu wa chama wa kijiji. hii inataka kufanana na yule mmbunge wa zamani wa Nyamagana aliyechukua samani za ofisi na kudai ni mali ya chama chake.
 
Wanabodi, nawashukuru wote kwa kusema ukweli. Ofisi ya serikali ya kijiji ni ofisi ya wananchi. Sikubaliani na kitendo cha CCM kuweka bendera yao kwa madai ofisi hiyo walijenga wao. Ni upuuzi kung'ang'ania jengo la ofisi badala ya kufanya shughuli za maendeleo. Anayesema natafuta 'cheap popularity' namsamehe bure. Kutokea kwenye gazeti au TV ningeenda na waandishi polisi. Sikuhitaji hilo. Na wala sihitaji. Inasikitisha sana tulipofikia ila muda umefika. Ni lazima tulete mabadiliko ya fikra. CCM haiwezi kuendelea kutumia wananchi. Watake wasitake imefika mwisho. Kata ya Mabogini itakuwa Kata ya mfano!
 
Mkuu msando kuna swala kuhusiana na mgao wa maji ya umwagiliaji kati ya chekereni na mabogini nikero ya muda mrefu hebu fafanua kidogo kuhusu hili
 
Back
Top Bottom