Diwani wa Chadema akamatwa na Bunduki

Hata mbele ya sheria mahakamani wengi huwa wanakana makosa mbona amekuwa mwepec kiasi hicho. Ametoka katika kikao, pili kuulizwa hapo hapo akakiri na kuwapeleka polisi kwenye chimbo aliloliweka moto! Je, inaingia akilini kweli bandugu
 
Mbona kwa maeneo yao ya Serengeti na Tarime kuwa na siraha ni jambo la kawaida tu. Wajaribu kufanya upekuzi kwenye mashamba na makazi ya wakazi wa huko waone. karibu kila kaya in mashine! Kama unabisha subiri mapigano ya kikabila yaanze uone, kila mtu anakuja na mashine!
 
Nina wasi wasi huyu anaweza akawa pandikizi la ccm. Kwa nini ikawa kirahisi rahisi kukubali na kwenda kuonyesha ilipo na kukiri?

Naona sasa CCM wanaingia kwenye territory ya mwaka 2005 ya Mahita na visu vya CUF. Ila ninawapa tahadhari moja kuwa Tanzania yetu tunataka amani, tupingane kwenye hoja na kama ukishindwa hoja kaa kimya. Naona sasa wanaanza ku-cross the line. Wajue kuwa Polisi na askari jeshi hawatoshi kulinda kila mwanasiasa, amani ni mindsets za watu, pindi wakiona uonevu na uongo unazidi wanaweza kukosa uvumilivu.

Hakuna kitu cha hatari sana kama kuwa na Taifa la watu waliokata tamaa - J K Nyerere

Unapoanza kucheza na akili za watu waliokata tamaa tegemea the worse, Amani ya Tanzania itavunjwa na CCM katika hatua zake za mwisho za kukata roho. CCM tafadhali kama gamba jipya ndiyo ki hivi basi mjue kuwa hilo gamba jipya ni kama baruti juu ya kiberiti, inasubiri msuguano na njiti ili pawake moto, Please msitafute msuguano huo kwa sasa. Haiingii akilini Mkuu wa mkoa kwenda kukamata silaha, huu ni mpango mahususi ama wa kupandikizia ili kumkomoa huyu diwani na kutaja CDM kwenye negative side au mmemshawishi diwani kwa pesa ili akubali na kuhusisha silaha na CHADEMA. Tunapokuwa na viongozi wa nchi wenye mawazo kama haya basi hili ni kundi la kigaidi period, maana soon wataanza ku-plant milipuko na kutisha wananchi huku wakisingizia CHADEMA. Kama mmezidiwa kwa hoja ujanja mzuri ni kuzichukua hoja zilizowazidi na kuzifanyia kazi, huo ndiyo uongozi - J M Kikwete
 
Mkuu ungekuwa wewe ungekataa kuonyesha silaha? Diwani kaona bora niwapeleke chimbo aliloweka silala asiwasumbue polisi, hongera Diwani kwa kujivua gamba
 
Mkuu ungekuwa wewe ungekataa kuonyesha silaha? Diwani kaona bora niwapeleke chimbo aliloweka silala asiwasumbue polisi, hongera Diwani kwa kujivua gamba

Soma habari vizuri mkuu, hii kazi haikufanywa na polisi. Ilifanywa na mkuu wa mkoa kanali mstaafu Mfuru, akiwa anarekodiwa tangu mwanzo hadi mwisho na kamera za Channel Ten.

Jambo pekee alilosikika anamtishia mtuhumiwa ni kwamba atamweka ndani hadi Rais aje kumtoa kama hatakiri kwamba anamiliki silaha. Jamaa naye kwa haraka kabisa akasema ndiyo anamiliki silaha eti lakini alipewa na 'jamaa mmoja"
 
and why do u associate chenge,lowasa and rostam with cccm?? bogus kabisa wewe
Kawaida yako kada wa Chi-Chi-Em kukemea wote wanaotaka kuharibu mchuzi wako. Pole, taratibu utatambua kwa nini unapoteza muda kutetea upuuzi unaofanyika ndani ya chama chako na serikali mliyounda kwa kuiba kura.
 
huyo walimseti hata kama angekuwa mwizi wa kweli asingejirahisisha kiasi icho na kuionyesha haraka, yote kwa yote ningefurai kama angetuletea huku arusha ssiku ile ya maabomu:alien:

Mkuu wa mkoa anakaimu nafasi ya kamanda wa polisi wa mkoa wa mara? Sielewi mkuu wa mkoa anahusikaje kwenye tukio la kumfuata na kumtoa kwenye kikao diwani wa Chadema!!!! Ningependa kusikia huyo Diwani amehukumiwa na amefungwa kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria!!! Lakini nina imani hatutafika huko!!! Lengo limetimia, ataachiwa kishikaji tu!!!

Tiba
 
Wenye akili wanaelewa,how come RC afanye kazi ya OCD?
Au huko hakuna OCD?vilaza wasiojua kupembua pumba na mchele ndio wanaochukulia kilahisi lahisi,kwa hiyo mmeona hiyo ni inshu muhimu sana eeh,kuliko ufisadi,
 
Ukifuatilia kwa makini,huyo "Jamaa Mmoja" aliyetoa silaha lazima atakuwa ni ccm
 
Hata mimi ninayo alinirithisha babu yangu,waje wanikamate! Au hamtakuja kwakuwa sina status ndani ya chadema kwa sasa?
 
Hata kama mtadelete comment za watu, Narudia tena kuandika kuwa chadema inavyoonekana wengi ni majambazi. Hivi yule diwani wa chadema aliyekuwa rumande kwa kosa la mauaji ameshatoka?
 
Hakukamatwa na silaha bali aliikabidhi silaha kwa mkuu wa mkoa kwa kukubali mwenyewe.Kuwa na siraha kinyume na sheria ni kosa, ila kuna hili la kutangaziwa kwamba wenye siraha kinyume na sheria wazikabidhi sehemu fulani la sivyo wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria, wakikabidhi yameisha, kama wale wa epa waliambiwa wakabidhi fedha yaishe.Sijui mamlaka haya huwa yanatoka wapi,kwamba kabidhi yaishe,nafikiri sio ya kisheria, lakini imezoeleka tu.
 
Hata kama mtadelete comment za watu, Narudia tena kuandika kuwa chadema inavyoonekana wengi ni majambazi. Hivi yule diwani wa chadema aliyekuwa rumande kwa kosa la mauaji ameshatoka?
Hivi yule Meya wa CCM Mwanza aliyekuwa rumande kwa tuhuma za mauaji ya katibu wa ccm ameshatoka??
 
Kama ni kweli, hilo ni kosa la huyo Mh. Diwani kama yeye. Kwa vyovyote vile hilo kosa halina uhusiano na dhehebu lake la dini au itikadi yake katika chama chochote.

Tuache ushabiki, tusimamie ukweli penye ukweli.

ubarikiwe ndugu kwakuwa na mtazamo mzuri. kwakuwa chama hakiwaambii watu waishi kinyume cha sheria. hata dito alipiga mtu risasi hawakusema mwanachama wa chama fulani kauwa mtu walitaja jina lake na cheo tu. jambo la pili yule siyo diwani wa chadema ni diwani wa kata fulani. kitu cha msingi ni kosa iwapo atapatikana na hatia anastahili adhabu kama mtu yeyote yule!.
 
Hapo lazima kuna kitu Ccm wamefanya, lazima!!
Duh kuwa mwanachadema raha, yaani unapata excuse kwa kila kosa, ukisababisha watu wauawe ni kosa la Ccm kuchakachua, kukamatwa na silaha ni sisiem wamepanga njama, kiongozi kuhamia Ccm ni mafisadi wamemhonga.
Halafu yakifika shingoni dawa ni kumkana tu. "Ni mwananchi mhalifu tu huyo haihusiani na Chadema" which is true, sema tatizo hiyo busara hujitokeza pindi Mchadema anapolitinginya tu. Siyo Msisiem...

ni sawa lakini ni linin kazi ya RC imekuwa kamata kamata! je mapapaa wangapi hapa Tanzania walio ccm wamekuwa wakihusishwa na uuzaji wa siraha haramu kule kongo na rwanda?na ni Rc yupi aliyejitokeza kuwakamata ?idiwani kama amevunja sheria asulubiwe ila inawezekana alinunua kujilinda tu! nchi imeoza.
 
Hivi yule Meya wa CCM Mwanza aliyekuwa rumande kwa tuhuma za mauaji ya katibu wa ccm ameshatoka??

ndugu avatar yako inanikumbusha mbali sana. wewe inawezekana ulipenda kuiweka kwa ajiri ya kuigiza. ndugu zungumza sana lakini omba usiwemo kwenye kundi la watu wa hivo. ila nazani unaweza hisi nimetoka mazingira gani!
 
and why do u associate chenge,lowasa and rostam with cccm?? bogus kabisa wewe
kashaga walipwa sh. Ngap na chama cha magamba{ccm}? Mbna umekuja na kasi sana af unatetea uovu? Nani asiyeyajua maovu ya chama kilichokutuma? Uwe unawaza wanao watakuja kuishi vipi katika nchi unayoibomoa kwa mikono yako mwenyewe,kwa kupewa vipesa vidogo na kukufanya usahau harufu ya shida ulionayo? Unahitaji kubadilika wewe ni kijana gani mwenye akili za kushikiwa?yani makamba kujiengua ndo mnatembea kifua mbele kana kwamba mmefanikisha kuinusuru nchi kutoka gizani,ufisadi,rushwa,ushikajilization, na magamba mengine mengi.uwe unafikiria mambo ya kuchangia kama hauwezi uwe mtazamaji.
 
Back
Top Bottom