Diwani wa CCM, wanachama 100 wajiunga CUF

Diwani wa CCM, wanachama 100 wajiunga CUF

chaikavu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2015
Posts
760
Reaction score
473
diallo-620x308.jpg

HALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na wanachama zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).

Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa wimbi la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA.

Diwani na wanachama hao kutoka matawi mbalimbali ya CCM, walieleza chanzo na sababu za kutimkia CUF, kuwa chama hicho kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na undugu kitendo kinachosababisha kukosekana kwa demokrasia ya kweli.


Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa kushika madaraka na kusababisha watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.

Wanachama hao wakiongozwa na diwani huyo, walipokelewa leo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Chakechake, Nyamagana.

Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na kukosekana kwa demokrasia.

"Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka waachane na wizi wao.

"Niliwania udiwani kwa mara nyingine tena, hila na tamaa ya CCM walinikata jina kwa sababu nilikuwa napingana nao, walipolazimisha fedha za miradi ya wananchi tuzitumie kwa mambo ya chama," amesema Fashion.

Kwa upande wake, Jeremiah amesema kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo, sasa umefika wakati wakaipisha UKAWA kuingia `magogoni` ili kutatua kero za watanzania.

mwanahalisi online
 
Viva CUF...go go go go Lowassa GO......
 
Huyo nu mtu mdogo sana kwenye siasa za Tanzania, ni sawa na punje ya mchele ndani ya ccm. Ccm haiwezi kuanguka kisa wapuuzi wachache.
 
Hahaa.....kwakwel..mwaka huu ukawa ...inatishaaa
 
CCM wamebaki wangapi? Kila siku wanachama wanahama. Cha ajabu utasikia CCM wanatamba kuwa wameongezeka! wanachachua mpaka namba ya wanachama wao. Karibuni UKAWA tupate mabadiliko.
 
Ukawa inapasua anga tu....Wataisoma mwaka huu
 
wela wela Cuf mwaka wa shetani kwa magamba.Cuf na Ukawa mwaka wetu
 
Huyo nu mtu mdogo sana kwenye siasa za Tanzania, ni sawa na punje ya mchele ndani ya ccm. Ccm haiwezi kuanguka kisa wapuuzi wachache.
bt thamani ya kura yake ni kubwa kuliko unavyofkir
 
Huyo nu mtu mdogo sana kwenye siasa za Tanzania, ni sawa na punje ya mchele ndani ya ccm. Ccm haiwezi kuanguka kisa wapuuzi wachache.
Ushawishi kwa wapiga kura wanaomzunguka ndilo la muhimu, come on man!
 
Cuf wapelekeshe magamba mpaka wajinyeeeee.Makomeo yuko na mapanya buku shimoni lumumbaaaaa
 
Back
Top Bottom